Mrejesho: Wiki ijayo naoa In Shaa Allah

Wakuperuzi

JF-Expert Member
Mar 31, 2023
2,077
4,673
Habari zenu ndugu,

majirani zetu na marafiki tusiofahamiana nje ya JF kama tunapatikana humu, isipokuwa wachache wanaofahamiana JF na nje ya JF. Poleni na mihangaiko ya kutwa nzima na wale ambao ndio kumekucha Mungu abariki harakati zenu usiku wa leo.

Mrejesho kuhusu thread niliyoleta humu kuhusu mwenzangu kupata teuzi kada ya afya wiki hii aliripoti halimashauri ya wilaya husika alikopangiwa, baada ya kumaliza zoezi lake la uhakiki wa vyeti ametakiwa kuripoti kazini tarehe mbili ya mwezi wa 7.

Baada ya kukamilisha zoezi hili ameniomba arudi tukamilishe swala la ndoa ili atakaporipoti kazini awe rasmi ni mke wa mtu.

Sitaki nishauriwe, nimeshahiyari kuoa ila kama yupo wa kunirahisishia connection huyu kiumbe akapata uhamisho kuhamia mjini nitashukuru.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom