Elections 2010 Mrejesho wa barua ya mwanakijiji tume ya uchaguzi, Membe apata mpinzani

Mheshiwa Mwanakijiji

Heshima yako mkuu. Naomba tupe mrejesho wa majibu ya barua yako tume ya uchaguzi kuhusu wagombea waliopita bila kupingwa.

Leo nimesikia mgombea wa tlp amerejeshwa uwanjani kumvaa membe. Heko NEC.
 
Kama NEC wamerudisha mgombea wa TLP then ilitakiwa sheria impe nafasi ya kufanya kampeni ya kutosha maana kwa sasa atakuwa na muda kidogo. hakuna fair play hapo mtama.
 
Habari iliyoko hapa chini inaonyesha kuwa bernard membe ataanza kufanya kampeni. Dhidi ya mgombea wa tlp. Kwa kuwa muda ni mdogo na inaonekana kifisadi taarifa hizo zilifichwa muda wa maandalizi wa huyu wa tlp haupo.

Nawaomba lipumba au dr. Slaa waende lindi kwa pamoja wamfanyie kampeni mgombea wa tlp kwa helkopta katika vijiji vyote:

Demokrasia tanzania inauawa na wenye pesa. Mtu uamuzi umefanyika mapema mwezi wa tisa lakini zikiwa zimebaki takribani wiki mbili ndio wolfgang anajua kuwa anagombea.
 
headline_bullet.jpg
NEC yamrejesha mpinzani wake wa ubunge
headline_bullet.jpg
Kulazimika kupiga kampeni kutetea kiti


Zikiwa zimebakia siku 18 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, mbunge wa CCM aliyemaliza muda wake wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliyekuwa amepita bila kupingwa sasa atalazimika kutoka jasho kutetea kiti chake.

Hali hiyo inatokana na maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya kurejesha jina la mgombea ubunge jimbo hilo kupitia Chama Cha Tanzania Labour (TLP), Ndaka Isack Wolfgang, baada ya kutengua pingamizi lililowekwa na Membe wa CCM.

Membe alikuwa anasubiri kuapishwa baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu, kutokana na kukosa mpinzani hivyo kutangazwa kuwa mbunge mteule.

Barua waliyotumiwa viongozi wa TLP mkoani Lindi, kutoka NEC yenye kumbukumbu namba AE/74/14162/51 ya Septemba 4, mwaka huu na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa NEC, V.A Mkwizu, inaonyesha kuwa Septemba 3, mwaka huu, NEC ilikutana kupitia rufaa ya mgombea wa TLP na kubaini kuwa mgombea huyo amedhaminiwa kihalali na watu 28, ambao wote wapo katika daftari la kudumu la wapigakura.

Barua hiyo pia, inaeleza kuwa msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Lindi alithibitisha kuwepo kwa majina ya wadhamini hao katika fomu zake za uteuzi wa mgombea huyo.

Uamuzi huo wa NEC kutengua pingamizi hilo, umemrejesha mgombea wa TLP katika kinyang'anyiro hicho.

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa viongozi na wanachama wa TLP hawakuamini kama jina la mgombea wao lingerudi katika kinyang'anyiro hicho, baada ya Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Lindi, Hijob Shenkalwah, kumtangaza Membe kuwa amepita bila kupingwa.

Msimamizi huyo aliliondoa jina la Wolfgang kwa madai kuwa saini za watu waliomdhamini zilikuwa za kughushi, jambo ambalo lilimfanya mgombea wa TLP kukata rufaa NEC kupinga uamuzi huo.

Akizungumza na NIPASHE, Mwenyekiti wa TLP mkoani Lindi, Mohamed Mfaume, alisema pamoja na NEC kuikubali rufaa yao, bado kumekuwa na urasimu mkubwa wa kupata barua ya maamuzi ya kumrejesha mgombea wao tangu uamuzi uliotolewa Septemba 4 hadi 18.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa hali hiyo imechelewesha maandalizi ambayo yangetakiwa kufanywa na chama chake.

Mfaume ameyataja mambo hayo kuwa ni kuwasilisha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa gharama za uchaguzi, ambayo mwisho wake ilikuwa Septemba 6 pamoja na maandalizi ya kampeni.

Alisema kitendo kilichofanywa na NEC na msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Lindi kukalia barua yao kinaonyesha ni jinsi gani kulikuwa na lengo la kutaka kukihujumu Chama chake.

"Ndugu mwandishi kwa mujibu wa barua tuliyoletewa inaonyesha kikao cha kupitia rufaa yetu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa Septemba 3 na kuandikwa Septemba 4 kisha kutumwa nakishi inayoonyesha Sptemba 16 na hapa ofisini tumeletewa Septemba 18, ebu fikiria muda wote huo ilikuwa ikifanya kitu gani kama sio urasimu wa makusudi?" alihoji Mfaume.

Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Lindi, aliliondoa jina la mgombea wa TLP kwa kile alichodai kuwa saini zilizowekwa na wadhamini katika fomu za mgombea huyo zilikuwa zimeghushiwa na mtu mmoja.

Uamuzi huo ulipingwa vikali na TLP kwa maelezo kuwa hakuna mtaalamu aliyekuwa amezipitia kuhakiki saini hizo.

Uamuzi wa NEC katika jimbo la Mtama unafanana na ule wa jimbo la Nyamagana, Mwanza ambako Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha naye alikuwa amepita bila kupingwa baada ya kumwekea pingamizi mgombea wa Chadema, Ezekiah Wenje. Pingamizi hilo lilitengeuliwa na NEC.

Kwa maamuzi ya Nec, sasa idadi ya wabunge wa CCM waliokuwa wamepita bila kupingwa imepungua.

Baadhi ya waliopita bila kupingwa ni pamoja na mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM, Januari Makamba (Bumbuli) Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Mlele), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro) na Celina Kombani (Ulanga Mashariki).

Wengine ni William Lukuvi (Isimani), Deodatus Philikunjombe (Ludewa), Gregory Teu (Mpwapwa), Anne Makinda (Njombe Kusini), Phillipo Morogwa (Songwe) na Job Ndugai (Kongwa).

CHANZO: NIPASHE
 
Lipumba na Dr Slaa anatoka wapi tena hapo, wao waache kupambana na URAIS wa vyama vyao waende kwa TLP. Kwani Mrema mzee wa kiraracha si yupo?
 
Mheshiwa Mwanakijiji

Heshima yako mkuu. Naomba tupe mrejesho wa majibu ya barua yako tume ya uchaguzi kuhusu wagombea waliopita bila kupingwa.

Leo nimesikia mgombea wa tlp amerejeshwa uwanjani kumvaa membe. Heko NEC.

Ghiliba na werevu ulio na ncha wa Bw. Membe sasa umefikia tamati mbele ya wananchi ambao anataka kuwaongoza bila ya ridhaa yao
 
Hapa tatizo liko kwa Tume, Tume inayo kila njia ya kuhakikisha barua kwa mgombea wa TLPv kwa wakati. Tena njia rahisi ingekuwa kuipeleka makao makuu ya TLP ambayo yako Dar na nakala ikapelekwa kwa huyo Msimamizi wa Uchaguzi jimboni. Tume itakuwa na sehemu kubwa ya lawama.

Hata Membe atakuwa amevurugwa pia na uamuzi huu,sioni mantiki ya Tume kukaa na rufani za watu kwa muda mrefu kwa kuwa inaathiri muda wao wa kampeni. Kwa vyovyote vile muda huu uliobaki muathirika mkubwa ni mgombea wa TLP. Pengine hakupata hata muda wa kukusanya rasilimali za uchaguzi.

Maoni yangu ni kuwa Tume hii itakuwa imefikia kikomo cha maisha yake( outlive) manake makamishna wale wamekaa muda mrefu na wanalalamikiiwa kila kona,pengine wamefikia kikomo cha ubunifu na wanaendesha mambo kwa mazoea
 
Hapa tatizo liko kwa Tume, Tume inayo kila njia ya kuhakikisha barua kwa mgombea wa TLPv kwa wakati. Tena njia rahisi ingekuwa kuipeleka makao makuu ya TLP ambayo yako Dar na nakala ikapelekwa kwa huyo Msimamizi wa Uchaguzi jimboni. Tume itakuwa na sehemu kubwa ya lawama. Hata Membe atakuwa amevurugwa pia na uamuzi huu,sioni mantiki ya Tume kukaa na rufani za watu kwa muda mrefu kwa kuwa inaathiri muda wao wa kampeni. Kwa vyovyote vile muda huu uliobaki muathirika mkubwa ni mgombea wa TLP. Pengine hakupata hata muda wa kukusanya rasilimali za uchaguzi.
Maoni yangu ni kuwa Tume hii itakuwa imefikia kikomo cha maisha yake( outlive) manake makamishna wale wamekaa muda mrefu na wanalalamikiiwa kila kona,pengine wamefikia kikomo cha ubunifu na wanaendesha mambo kwa mazoea
 
Hay, WanajamiiForums.

I've an Interesting Question?

Napata kigugumizi kujua, JE, Majina na Picha za Wagombea (uRais, uBunge, uDiwani) kama bado yanaendelea kuchapichwa though juzi tumepokea conssignment ya karatasi hizo toka Uingereza! JE, Huyu Mgombea alopata idhini ya kufanya kampeni 18days before election KARATASI ZILIZOPOKELEWA ZINA PICHA YAKE? Au nielewe karatasi inakuwa na majina na picha za wooooooote walioomba hata kama hawakufuzu?

Pls HELP!
 
  1. Mh. sana Laurence Masha alisha tangazwa ampita bila kupingwa kwa mizengwe. Wenje na chadema wangenyamaza, ilikuwa imetoka hiyo.
  2. Naomba dhana hii ilaniwe na wale wote waliopitia dirisha hili kuingia bungeni, warejeshwe uwanjani. ngoma ichezwe dakika 90.Naamini kuna watu watatolewa nishai. Masha ametuonyesha njia.
 
Kweli kabisa,huyu jamaa alikwisha jihakikishia ushindi na hata JK nae akamtangaza kuwa amepita na sasa kibao kimegeuka.
Hongera mbunge mteule wa Chadema kwa kuonesha njia.
 
Nafikiri Ngandema hii hoja umeaicha hewani na mimi naomba niipanue zaidi kidogo. Hii kitu inayoitwa kapita bila kupingwa nafikiri imedhihirika kuwa hakuna mtu anayepita bila kupingwa kabla ya kura hazijapigwa. Sheria zetu zinaruhusu mapingamizi kuwekwa pale inapobainika sheria au kanuni za uchaguzi hazikuwekwa. Na kama pingamizi likiwekwa na kukubaliwa na tume ya uchaguzi na kama kulikuwa hakuna mgombea mwingine, basi huyo aliyeweka pingamizi na wakati ni mgombea anakuwa kapita bila kupingwa. Lakini ukweli ni kwamba kama kura zingepigwa ingejulikana kama kweli anakubalika kuwa mwakilishi wa wananchi au la. Mie nilikuwa nafikiri, kwa wale wanaopita bila kupingwa on 'TECHNICAL REASONS' basi sheria iruhusu wapigiwe kura ya ndiyo au hapana. Wale ambao watapita bila kupingwa kwa sababu hakuna mgombea aliyejitokeza basi huyo ndio ahesabiwe kama kapita bila kupingwa.
 
hii dhana ya kupita bila kupingwa inaniudhi sana. kwani inanyima watu haki yao ya kuchagua mwakilishi wao. katika kufuatilia hili nikaelezwa ipo kwenye sheria ya uchaguzi na imepitishwa na bunge ingawa ipo kinyume cha katiba. sasa najiuliza mwanasheria wa serikali hakuwepo? na je waziri wa sheria na katiba hakuwepo? kama mtu kama mimi ambaye sijui sheria naweza kugundua kuwa hapa hakuja kaa sawa wao je watakuwa wamefanya makusudi kwa maslahi yao na wakijua wana kinga. kuna mambo mengi ya kufanya ili maendeleo ya kweli yaje kwenye nchi yetu. cha kuanza ni sisi kama watanzania kushirikiana na wabunge wanapopingwa vitu vya msingi bungeni kwa ushirikiano wa asasi za kiraia na za haki za binadamu. kwa kuanza kuomba hicho kipengele cha kupita bila kupigwa kwenye sheria ya uchaguzi kitolewa kwani kina vunja katiba. huyo mbunge anawakilisha nani kama hajachaguliwa?
 
Back
Top Bottom