Mrejesho: Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba

Mkuu asante sana ushauri wako naufanyia kazi,pia kuhusu wateja wa humu JF nimepata aisee sihaba.

Lakini tatizo lakutaka kumuweka mtu nikuwa sasa naingia mwaka wa tatu course yenyewe ni ngumu Mechanical eng ndio maana nilikuwa nataka nifanye biashara ambayo sintoisimamia sana.Pia nilitaka nichangie kumsomesha dogo maana hali mbaya hom ingawa kafauru vizuri na course yake priority lakini ndio hivo mkopo hamna.
Ni sawa mkuu ila kwa hizo busness zinaweza kukuongezea stress kuliko kupunguza, niliwahi kuwa na idea ya saloon na hiyo ya bodaboda ila baada ya kufanya utafiti nikagundua ina stress kuliko nilivyofikiri hasa kupitia kwa baadhi ya rafiki zangu waliofanya hizo biashara, biashara ya duka ndiyo nafanya sasa hivi na inanilipa sana ila inatokana na kuwa wife ndo mtu anayeshinda dukani na tunaelewana sana. Njia nyingine unayoweza kufanya kwa sasa au baadae ni kununua hisa katika mashirika yanayopata profit, unakua unapata gawio kila mwaka japo linaweza kuwa kidogo ila capital yako inakua salama. Ila ngoja tuone na michango mingine ya watu waliopractice hizo biashara hope mwisho wa siku utapata wazo zuri.
 
mechanical eng chuo gani?hapa dar nahitaji kuonana naww tafadhari
 
Anaweza Pata ilaa hesabuu ya kwa day yakumpelekea bosi wake wengiwao n elfu 7000 mpk 10000 cjui utampata wapi wa 22 kwa day hata wa mkataba hapati, ajaribu biashara nyinginee mkuu wangu
Mkuu soma vizuri thread nimesema bodaboda 2.
 
Ni sawa mkuu ila kwa hizo busness zinaweza kukuongezea stress kuliko kupunguza, niliwahi kuwa na idea ya saloon na hiyo ya bodaboda ila baada ya kufanya utafiti nikagundua ina stress kuliko nilivyofikiri hasa kupitia kwa baadhi ya rafiki zangu waliofanya hizo biashara, biashara ya duka ndiyo nafanya sasa hivi na inanilipa sana ila inatokana na kuwa wife ndo mtu anayeshinda dukani na tunaelewana sana. Njia nyingine unayoweza kufanya kwa sasa au baadae ni kununua hisa katika mashirika yanayopata profit, unakua unapata gawio kila mwaka japo linaweza kuwa kidogo ila capital yako inakua salama. Ila ngoja tuone na michango mingine ya watu waliopractice hizo biashara hope mwisho wa siku utapata wazo zuri.
Asante mkuu nimekusoma vizuri na nimekuelewa.
 
Salama wakuu.

Miezi kama mitano nilikuja hapa na thread hii hapa chini.

Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba. Nawe waweza jaribu mahali unapoishi

Ingawa nimepata faida ya kutosha mpaka sasa lakini nilitaka nibadilishe au nipanue biashara yangu kidogo.Katika biashara nilizotaka nifanye ni hizi hapa chini.Nimeamua nibadili aina hii ya biashara ili niweze pia kumsomesha mdogo wangu wa amekosa mkopo.

Ningeomba mawazo yatakayotolewa yajikite katika biashara hizi tatu,nisingependa mtu atoke nje ya biashara hizi tatu.

1.Ninunue boda boda mbili niwape watu wasimamie kisha watakuwa wananiletea elfu 22 kwa siku.

2.Nifungue saluni BABER SHOP ya million 4(kwa siku hapa nipewe tu elfu 15)

3.Au nifungue kiduka cha rejaleja cha mtaani cha million nne(changamoto hapa nikumpata muuzaji muaminifu) hapa pia ntaendelea kufanya biashara yangu ya mchele.

NOTE:
Pesa niliyonayo mpaka sasa ni 4m Baada ya kupata msaada wa member mmoja wa Jf wa Million moja baada ya kutembelea na kuona biashara yangu.
Mkuu naomba uni pm kama huto mind...maana najaribu kuku pm afu inagoma
 
Ongeza mtaji na uboreshe biashara uliyonayo sasa ya mchele...nyingine achana nazo mpaka umalize chuo
 
Mkuu nakushauri ungeongezea mtaji kwenye biashara ya mchele ambayo unaimanage vizuri, kikubwa unachoweza kufanya ni kuongeza soko la bidhaa zako, naamini kwa kuweka namba zako humu utapata wateja wengi zaidi. Hizo idea za biashara unazotaka kuzifanya sio mbaya kama utakua na usimamizi wa karibu ila hazina faida kama hazina usimamizi wa karibu sana(sababu kubwa ni uaminifu, hatuna watu waaminifu katika familia zetu kwa sasa). Ila nafaka ni biashara nzuri na rahisi kuimanage. Sana sana unaweza kuongeza bidhaa nyingine tofauti za nafaka, kama maharage, ulezi n.k

Yaah hata mimi nilidhani hivyo. Tayari una uzoefu katika eneo hilo, concentrate nguvu na akili zako hapo, in fact unachoweza kufanya cha ziada katika eneo/biashara hiyo, ni ku ADD VALUE kwenye mchele huo unaouza labda kwa kufanya packaging hususan kwa wateja wa hapo "Chuoni" ulipo. Lenga hata walimu wako na staff wengine kwa kufanya packaging ya kawaida tu, siyo sophisticated! Hiyo faida, weka akiba for a rainy day!
 
Kwa kuongezea tu aweke packaging ya uzito tofauti km kg 1, 2 na 5 then awe ameshauchambua kabisa. Anaweza kuvutia wateja zaid.
 
Biashara ya uhakika hapo ni kiduka cha reja reja, maana itakua rahisi Ku monitor biashara yako. Pia jitahidi uwe karibu.

Boda boda ni pasua kichwa sana, utaishia kuziuza kwa hasara, pia risk yake ni kubwa, ikiibiwa manake imepotea mazima.

Barber shop sijui kiundani, lakini nayo kama haupo mwenyewe nadhani inasumbua.
 
Back
Top Bottom