Mrejesho baada ya kuanzisha biashara: Mambo 15 ya kuzingatia kwa kijana

Financial Analyst

JF-Expert Member
Nov 27, 2017
1,605
2,749
Habari Vijana wenzangu, Nimeamua kushare na nyie MAMBO 15 niliyejifunza baada ya kujikita katika uanzishaji wa biashara kwa mara kwanza katika maisha yangu mwaka jana (2018)

1: Kamwe usiombe ushauri wa uchaguzi wa biashara gani inayofaa wewe kufanya.

2: Usianzishe biashara kwa kuwa unahisi unaweza kuwa na biashara au kwa sababu wengine wameweza kuanzisha biashara. Anzisha biashara kwa kuwa ni muda muafaka katika maisha yako na ukiwa na utayari kielimu, kiafya, kisaikolijia,..n.k

3: Njia nzuri ya kupata hamasa na muongozo juu ya biashara unayotaka kuianzisha ni kumfikia yule aliyetangulia/aliyewahi kuifanya hiyo biashara. Unaweza kumuomba awe muongozaji wako (Mentor).

4: Usijifunze vile unavyohitaji kujua..Jifunze vile unavyopaswa kujua na vile usivyovijua kuhusiana na biashara. Kama wewe ni mzito wa kusoma vitabu angalau soma makala, blogs, websites zinazohusiana na biashara.

5: Kwa wale wanaojitegemea, Linganisha Biashara yako utakayotaka kuanzisha na gharama ya maisha unayoishi. Ni either ubuni biashara yenye faida kubwa (siyo mapato makubwa) ili ikidhi gharama zako kubwa za maisha au upunguze gharama za maisha ziendane na hali ya faida ya biashara yako ili usije ukaikandamiza biashara yako.

6: Jifunze uhusiano na utofauti kati ya mali na dhima (assets na liabilities), pesa za uendeshaji na pesa za mzunguko ( working capital na cashflow) mapato na faida (earnings na profit), mapato halisi na umiliki wa pesa (net income and wealth). Hii itakusaidia katika usimamizi wa fedha zako na pia uwekezaji wa pesa zako.

7: Fanya uchunguzi wa kina wa jamii inayozunguka eneo lako la biashara. Ni vizuri ukifahamu kujua kuhusu hali yao kiuchumi, nguvu ya manunuzi, ladha na upendeleo (taste and preference).

8: Epuka kasumba ya "pata eneo lenye mzunguko watu au watu wengi".. Hii haileti mantiki kabisa, unaweza pata eneo lenye watu wengi ila lisiwe rafiki juu ya aina ya biahara yako. Pata eneo lenye uhitaji au uhaba wa bidhaa au huduma unazotaka kuziweka sokoni.

9: Fanya juu na chini uelewe zaidi kuhusu washindani / wenye biashara kama unayotaka kuanzisha. Baada ya kufahamu kuhusu endeshaji wa biashara zao, itakubidi utengeneze mkakati (business strategy) wa kuweza kuingia katika ushindani (bei, ubora, after-buying service, free delivery, ujazo...nk)

10: Kabla ya yote fanya makadirio ya bei ya ya uzaaji, mapato, gharama ya uendeshaji na faida au hasara itakayopatikana, then uangalie kama faida itapatikana kweli na kama faida itakuwa rafiki kutokana na uwekezaji wako.

11: Kumbu kumbu na mahesabu. Uwe na sehemu sahihi ya kuaandaa nakala juu ya uendeshaji, mihamala na gharama tofauti. Hii itasaidia kukujuza jinsi unavyo perform na wapi unaelekea.

12: Usiwekeze mtaji wako wote unapoanzisha hiyo biashara. Weka akiba ya pesa kwa ajili ya ku-update biashara yako na ununuzi wa bidhaa zitakazohitajika zaidi.

13: Weka mpango mkakati juu ya pesa za faida ya biashara yako. Njia nzuri ni kuhifadhi asilimia ya faida yako kwa ajili ya kukuza biashara yako mbeleni au kufanya uwekezaji mwingine.

14. Jifunze mwenendo wa kiuchumi na majira na jinsi vinavyo affect biashara yako kwa nyakati tofauti. Hii itakupa uwezo mkubwa kutabiri (speculate) na kufanya maamuzi kabla ya majira kufikia.

15: Usianzishe biashara kwa mategemeo ya kuwa tajiri, kupata pesa nyingi.... N.k, Anzisha biashara kwa mategemeo ya kutengeneza faida na kuepuka hasara then hivyo vingine vitafata.

BONUS: Kitakachoendelea kuturudisha nyuma zaidi watanzania ni ulimbukeni, minyororo ya imani zisizokuwa na maana, fitna na kutopenda kujifunza kwa kina. Naamini tukiyashinda haya.. Tutapata uepesi katika safari za kujiajiri / kuanzisha biashara.

AHSANTE!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameandika facts, shida itakuja tu pale ye mwenyewe hana biashara wala mtaji ila ameamua tu kushusha ndoto za bussness administration, kongole mkuu
 
Ameandika facts, shida itakuja tu pale ye mwenyewe hana biashara wala mtaji ila ameamua tu kushusha ndoto za bussness administration, kongole mkuu
Ndio kawaida ya wabongo kama nyie...

Roho mbaya inakuwa juu juu na mchanganyiko wa fitna na wivu.

On wht evidence do u have that i am not an entrepreneur ....natoa hapa mada kwa ajili ya kusaidia na kuhamasisha watu, sio kwa ajili ya wenye negative thinking kama wewe.

Grow up...or u will remain stupid.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio kawaida ya wabongo kama nyie...

Roho mbaya inakuwa juu juu na mchanganyiko wa fitna na wivu.

On wht evidence do u have that i am not an entrepreneur ....natoa hapa mada kwa ajili ya kusaidia na kuhamasisha watu, sio kwa ajili ya wenye negative thinking kama wewe.

Grow up...or u will remain stupid.


Sent using Jamii Forums mobile app
Acha story nyingi,unafanya biz gani?

Mbona ni swali rahisi tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom