Mramba azidi kumkandamiza Mkapa mahakamani

Ha ha ha ha ah! Lakini MKAPA ana KINGA YA KUTOKUSHTAKIWA KWA MUJIBU WA "KATBA". Hivi hamuoni huu mchezo CCM wanaowafanyia watanzania?

Yaani in short, wakubwa wanapanga haya madudu strategically, waiibie nchi then issue zikifutuka kama hivi, wasingizie ilikuwa ORDER kutoka juu wakijua vizuri (si walipanga wenyewe) kwamba huyo wa juu ana KINGA. Mkapa mwenyewe, Mramba, Yona, et. al wanajuai vizuri sana wanachokifanya na tusitegemee lolote.

Issue ya Mahalu ilikuwa hivi hivi - KINGA YA KUTOSHTAKIWA kwa Rais Mstaafu. Ukiona Rais au Rais Mstaafu anapandishwa kizimbani ujue mchezo umeisha, hakuna kesi hapo.

KATIBA MPYA izuie kabisa hii kitu inaitwa KINGA KWA RAIS MSTAAFU - ni ufisadi mtupu.

For sure huu ni mchezo wa mda mlefu sana. Bahati mbaya mchezo huu umekuwa ukifanywa na wajaja wachache waliosomeshwa kwa fedha za walala hoi, maskini na wasio elimishwa juu ya haki zao. Hata hivyo 'time will tell'
 
Kama ilivyokua kesi ya Mahalu,hata hii ilifunguliwa kulipa visasi. Mramba tayari ameisha chomoa hapo,anayebisha aendelee kubisha,lakini ukweli ndiyo huo!
 
...Wote wezi tu Mkapa mwizi na Mramba mwizi sijui hao jamaa alioshinikiza walipwe mapesa chungu nzima walimwekea kiasi gani katika bank account yake ya nje. Huwa wanaapa kwa kushika vitabu vitakatifu kama usanii tu wakishashika madaraka wanakuwa busy kujaza mabenk account yao na mifuko yao kwa pesa haramu bila kujalia maslahi ya nchi.

kana kwamba wakati wa kula kiapo hakuapa kwa Mungu moja kwa moja bali kupitia kwa Mkapa!

 
Back
Top Bottom