Mpya: Tume ya Rais ya EPA yalonga

Wandugu: Ni wapi wamesema baada ya kurudisha mali hawatachukuliwa hatua za kisheria in regards to their actions?

sasa wachukuliwe hatua kwa kosa gani? na hizo mali wanarudishwa kwa amri ya chombo gani? Na ni nani ameamua ni mali ipi irudishwe?
 
Be specific kinachoruhusiwa hapa!


Soma hii

Ndani yake kuna hili limeongelewa kwamba kifungu cha 42 -2 kinampa mamlaka mwanasheria mkuu, uwezo wa kuiomba mahakama inayomtia hatiani mshutumiwa wa kosa la rushwa kutoa amri ya kutafisha mali aliyopata mtu huyo kwa rushwa (corruption) na wala sio bribing.

Nadhani waliendelea zaidi na ilikuwa ishawekwa wazi kabisa kwamba wakati wa uchunguzi PCCB ina mamlaka ya kufunga bank account etc
 
Waungwana wenzangu, knowing what our RULERS are mi nadhani something is better than nothing. Ni kweli hawa watuhumiwa wangefikishwa/inabidi wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria, lakini kama kweli atleast tume imeweza ku-salvage chochote mi nadhani ni Heri KWA WATANZANIA. MAANA TUMEONA TUME ZIKIUNDWA NA KUTUMIA MABILLION YA KODI ZETU NA SISI KUAMBULIA PATUPU!

Kwa hiyo kama wamerudisha hata kiasi fulani, mi nadhani its far better kuliko tungepewa report ambayo itawekwa kwenye shelf na kupigwa vumbi!

Tungekuwa na akina Hosea na Mwanyika Makini hapa ndo wangeanzisha investigations na kuwachukulia hatua. Kifupi mi nafurahi kweli kama atleast wamesevu kiasi hicho na wanampango wa kukamata hizo mali zisizohamishika za watuhumiwa. Please mwenye habari awapigie simu!

Naelewa sentiment za wengi humu, lakini waungwana, tumepewa report ngapi mpaka leo ambazo hatujaona kitu? Hivi mnajua kwamba mpaka leo bado tunalipa ile 152M kwa siku ya Richmond? ingekuwaje kama ule mkataba kwanza ungevunjwa ndo tukaendelea na uchunguzi kuhusu Richmond?

All in all its a right step cha muhimu ni kuweka pressure hawa wezi wafunguliwe jinai na uhujumu uchumi! when it comes to the war against corruption and mafisadi, History is not on our side! so we better save what exist before we try to go to court...you all know this-though its very sad.

Ila nawapongeza hii kamati kwanza kwa kuwa na courage ya kudeal na hawa jamaa mpaka wakarudisha some money! Who knows...tunaweza pata Zahanati somewhere Kasulu na Mpanda kwa hiyo hela! swala la Prosecution ni MWANYIKA NA HOSEA..WATAWEZA? MI NA WEWE HATUJUI!
 
Soma hii

Ndani yake kuna hili limeongelewa kwamba kifungu cha 42 -2 kinampa mamlaka mwanasheria mkuu, uwezo wa kuiomba mahakama inayomtia hatiani mshutumiwa wa kosa la rushwa kutoa amri ya kutafisha mali aliyopata mtu huyo kwa rushwa (corruption) na wala sio bribing.

Nadhani waliendelea zaidi na ilikuwa ishawekwa wazi kabisa kwamba wakati wa uchunguzi PCCB ina mamlaka ya kufunga bank account etc

Hili suala halina uhusiano na rushwa,kilichofanyika hapa ni watu wametumia nyaraka za kugushi ili kujipatia pesa.HUU NI WIZI, ni sawa na mtu yeyote anayetumia cheki bandia kujipatia pesa ktk benki yoyote ile.

Lakini turudi nyuma kidogo,hili suala la kufoji vitu kwa utawala wa ccm na serikali yake kwao ni kitu cha kawaida au ni sifa ya kuwa mwanachama bora ktk chama na serikali,rejea sakata la mbunge wa buchusa yule aliyefoji vyeti ilikupata ubunge si serikali wala chama waliomshughulikia mpaka sasa.ndio maana hata hawa waliojipatia pesa kwa njia ya udanganyifu hakuna chombo chochote kilicho washugulikia,zaidi ya kuwahadaa wananchi.

Kwa nini benki kuu isiwafikishe hawa wateja wao mahakamani kwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu au hizi pesa si zao ?
 
yaani wamerudisha mali ili yaishe kimya kimya. Basi si waambiwe tu warudishe mali yaishe. Maana kutakuwa na umuhimu gani wa kuwafikisha mahakamani wakati wamesharudisha mali?

Mwanakijiji, hapa sikuelewi yaani na wewe unaunga mkono mambo yaishe kimyakimya?

Inabidi tuzingatie hili hili na EPA na kwamba Balali lini anarudi Tanzania ili ajibu tuhuma, ingawa bado naona Balali anaongoza kwa mabao mawili kwa bila dhidi ya Serikali.
 
Soma hii

Ndani yake kuna hili limeongelewa kwamba kifungu cha 42 -2 kinampa mamlaka mwanasheria mkuu, uwezo wa kuiomba mahakama inayomtia hatiani mshutumiwa wa kosa la rushwa kutoa amri ya kutafisha mali aliyopata mtu huyo kwa rushwa (corruption) na wala sio bribing.

Nadhani waliendelea zaidi na ilikuwa ishawekwa wazi kabisa kwamba wakati wa uchunguzi PCCB ina mamlaka ya kufunga bank account etc

Nadhani katibu tarafa amekujibu vizuri hapo juu. Ni kifungu gani ambacho kinafanya hili jambo kuwa corruption na sio wizi kamili kama wizi mwingine? Hata kama hii ni corruption or whatever the name itatumika, hii haisemi kuwa wakirudisha mali basi inatosha na hivyo wasishtakiwe au kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na hatimaye kuadhibiwa.

Ukisoma maswali yangu hayapo tu kwenye kurudisha mali, yapo kwenye what then.....
 
Naomba mrudie tamko la Rais kuhusu EPA na ule uchunguzi halafu muone kuwa kile kinachofanyika sicho kinachotakiwa kufanyika.
 
Wandugu: Ni wapi wamesema baada ya kurudisha mali hawatachukuliwa hatua za kisheria in regards to their actions?

Na ni wapi wamesema watuhumiwa hao watachukuliwa hatua hasa ikizingatiwa kwamba hadi sasa hawajachukuliwa hatua?Kama mafisadi wa Richmond bado wanapeta,Ditopile bado yuko huru,Mwanyika na Hosea bado wako ofisini,ni mzembe wa kufikiri tu ndie anayeweza kuwaza kwamba watachukuliwa hatua.
 
Mzee mwanakijiji you should know this better than anybody! Tangu lini Tanzania kauli za viongozi zikaendana na matendo yao?

Mzee kwa swala hili la Rushwa na mafisadi, kwa mara ya kwanza NASEMA Iam more interested in the results than the process!

Kama tunaweza kupata hiyo pesa iliyokwibwa EPA (irrespective imerudishwa vipi) nadhani ni vizuri, process ya kuwashtaki na kuwasweka Keko watuhimiwa..ni nyingine and it may take years!

We need our money back!
 
Soma hii

Ndani yake kuna hili limeongelewa kwamba kifungu cha 42 -2 kinampa mamlaka mwanasheria mkuu, uwezo wa kuiomba mahakama inayomtia hatiani mshutumiwa wa kosa la rushwa kutoa amri ya kutafisha mali aliyopata mtu huyo kwa rushwa (corruption) na wala sio bribing.

Nadhani waliendelea zaidi na ilikuwa ishawekwa wazi kabisa kwamba wakati wa uchunguzi PCCB ina mamlaka ya kufunga bank account etc

Mwanasheria Mkuu huyo ni huyu Mwanyika au mwingine?Ok,let's put that aside.Lini huyo AG kaiomba mahakama hicho kibali/ruhusa....na hiyo mahakama iliyowatia hatiani watuhumiwa ni ipi?

Hapa kinachofanyika ni usanii tu,I doubt kama kuna shilingi moja iliyorejeshwa.If so,why no names?how much has been returned so far?Kuamini hili ni sawa kabisa na kuamini kwamba Richmond ingeweza kuzalisha umeme.
 
Hili suala halina uhusiano na rushwa,kilichofanyika hapa ni watu wametumia nyaraka za kugushi ili kujipatia pesa.HUU NI WIZI, ni sawa na mtu yeyote anayetumia cheki bandia kujipatia pesa ktk benki yoyote ile.
definition ya rushwa unayotumia ni ipi? rushwa kwa maana ya corruption, au rushwa kwa maana hongo!
 
Ahsante JK kwa uongozi wako, wenye macho tunauona na wenye masikio tunausikia. uzi huo huo, tunakuombea Mwenyeezi Mungu akuepushe na mahasidi wasioona unachokifanya kwa roho zao mbaya na akuepusha na fitna na majungu na visasi vya hao unao-washughulikia.

Haya wale wanaolonga longer humu waanze kuonyesha uzalendo wao, namba hizo.

Ahsante JK kazi tunaiona. Wengine waanze kukaa mkao wakula zamu yao inakuja.

Kwikwikwikwikwikwi!!Hahhahahahahaha!! Tendawiliiiiii.Chali Pwa.Pua.
 
Wait a minute!

Uchunguzi uliofanywa na E&Y ulikuwa ni kuhusiana na pesa za BOT-EPA. Hizi ndio pesa za kina Kagoda, KERNEL na madudu mengine.

Pesa zilizoanzwa rudishwa BOT ni ile mikopo ya pesa ya Japan za Commodit Import Support maarufu kama CIS.

Sasa cha kuuliza ni je pesa ganio zinazorudishwa? Kama ni za EPA, hizi ndizo zinazohotajika watu wafikishwe mahakamani maana hizi $133m zimeshapotea katika vitabu.

Kama ni za CIS, je wanaorudisha mikopo wamelipa mtaji na riba kwa serikali? Infact pesa za CIS ni karibu 10% ya pesa za EPA!

Lets be objective and stay focused. Tusije laza damu kesi ya uhujumu wa EPA ikasawazishwa kwa malipo ya CIS!
 
Naomba mrudie tamko la Rais kuhusu EPA na ule uchunguzi halafu muone kuwa kile kinachofanyika sicho kinachotakiwa kufanyika.

mwanakijiji i hope umepewa na wewe freq inayotumika// ahahahha

wananchi tuwe watulivu na habari za kutoka ndani ni kuwa wahujumu wameambiwa lipeni hizo hela itawasaidia baadaye.

sasa kama umekubali kulipa pesa ulizoiba, ukifunguliwa kesi ya wizi mbeleni unaweza kusema oh mimi sikuiba///

tusubiri tu na wakitaka kuleta za kuleta kazi itakuwa kubwa
 
Nafikiri mwenyekiti wa tume hayuko makini kabisa. Tunataka kuona report ya kazi aliyopewa ikiainisha bayana matokeo ya uchunguzi wao. Hebu fikiria, inatia akilini kweli kusema wezi wameanza kurudisha mali na kuomba watu ..whistleblowers..wawapashe habari za mafisadi! Nahisi kuna mapungufu makubwa kwenye utaratibu ambao mkuu wa tume anataka kutumia. Na mwisho wa siku tunataka kupata habari za wahusika na hatua zitakazochuliwa juu yao.
 
Nadhani tumesahau nini Rais aliagiza. Ngoja niwakumbushe kidogo.

4. Rais amewaagiza; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Inspekta Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kuchunguza na kuchukua hatua zipasazo za kisheria kwa makampuni na watu waliohusika na uhalifu huu. Rais amewataka watumie ipasavyo mamlaka na madaraka waliyo nayo kwa mujibu wa sheria. Aidha, amewataka wakamilishe kazi hiyo katika kipindi cha miezi sita.

Amemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe kiongozi wa kazi hii.

Amewataka wahakikishe kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.


- Sasa kwa mujibu wa taarifa ya Rais ni kuwa kilichofanyika ni uhalifu na ushahidi wa uhalifu huo wao Ikulu wanao ndiyo maana wamezeza kusema pasipo kujiuma kuwa kilichofanyika ni "Uhalifu" na siyo "kupitiwa, kusahau, bahati mbaya, ajali" n.k

- Sasa kama kilichofanyika ni "Uhalifu" basi kinachotakiwa hapo siyo kuundwa Kamati au tume yenye wajumbe kadhaa; kinachofanyika ni "kuamuru kukamatwa kwa wamiliki wote wa makampuni haya, na kufikishwa mahakamani mara moja ili wajibu tuhuma mbalimbali dhidi yao."

- Baada ya kukamatwa Rais angemuagiza "Mwanasheria Mkuu kusimamia kesi dhidi ya watuhumiwa hawa ili kuhakikisha kuwa adhabu ya juu kabisa dhidi yao inapatikana.

- Kuagiza mkuu wa uchunguzi wa Makosa ya Jinai, kuanzisha uchunguzi wa kihalifu mara moja ili kujua kina, upana, n.k wa uhalifu huu. Kufikia lengo hilo DCI atapewa ushirikiano na Taasisi ya Scotland Yard na FBI (Financial Crime Unit)ili kuweza kupata ushirikiano wa kitaalamu.

- Ametoa ombi rasmi kwa Interpol kuwaweka watu wafuatao katika rada zao, Jeetu Patel n.k ili wakamatwe na kurudishwa nchini kujibu mashtaka.

Rais hakufanya hayo yote; asingeweza kutoa amri za namna hiyo!! Usiniulize kwanini.
 
Na John Bwire - Raia Mwema

NI habari njema kwamba watuhumiwa wa sakata la ufisadi wa mabilioni ya fedha ndani ya Benki Kuu ya Tanzania BoT kupitia akaunti ya EPA, wameanza kulipa sehemu ya fedha za wakulima na wafanyakazi wa nchi yetu, walizokuwa wamejichotea.

Tayari serikali imeshapokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa watu mbalimbali waliohusishwa na uchotaji wa jumla ya Sh bilioni 133 kupitia akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Fedha hizo zimekuwa zikirejeshwa huku kamati maalum iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete ikiendelea na uchunguzi wake, na ikiwa ni mkakati maalumu wa kuhakikisha ya kuwa fedha zilizoingia katika mikono isiyo halali zinarejeshwa serikalini.

Kama tulivyosema mwanzoni mwa maoni haya kwamba habari kwamba fedha hizo zinarejeshwa ni njema. Lakini, pamoja na uzuri wa habari hizo, tunadhani hatua hiyo pekee ya kurudisha fedha haitoshi.

Tunasema haitoshi kwa sababu kilichokuwa kimetokea ni udanganyifu wa hali ya juu wa kukwapua fedha za serikali; jambo ambalo tafsiri yake ni wizi. Wizi wa fedha za umma ni kosa la jinai na kosa la namna hiyo likifanyika wahusika ni lazima wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Hatuoni sababu ya jeshi letu la polisi kwa mfano kuwachangamkia ‘wezi wa kalamu’ wa Sh 100,000 au vibaka wanaokwapua simu na kuwaacha wezi wa mabilioni ya fedha wakiondoka hivi hivi eti tu kwa sababu wamerejesha mapesa waliyokwiba.

Polisi wanapochunguza kesi ya ‘mwizi wa kalamu’ na kuamini kwamba wizi huo kweli ulifanyika hawamwamuru mwizi huyo arudishe fedha na kufuta kesi dhidi yake. Hufanya juhudi zote za kuthibitisha wizi wake ili mahakama impatie adhabu anayostahili.

Hivyo hivyo mwizi wa simu. Akikamatwa polisi hawamwamuru mwizi huyo amrudishie aliyekwapuliwa simu yake na baadaye ‘kumshukuru’ kwa ustaarabu wake wa kuridhia kurudisha simu, bali humfikisha mahakamani ili apatiwe adhabu yake.

Adhabu hizo huwa fundisho kwa wengine ili wasiwe na mawazo ya kujifanya wajanja wa kuiba kwa kutumia kalamu au kwa kuendesha maisha yao kwa wizi wa simu kiasi cha kuwapatisha taabu raia wenzao wanaovuja jasho kuwa na vitu hivyo muhimu kwa mawasiliano.

Kwa kweli kama watuhumiwa wa sakata hili la ufisadi hawatachukuliwa hatua za kisheria, ‘mchezo’ huu utaendelea na itakuwa wazi kwamba nchi yetu iko makini tu kudhibiti wizi mdogo mdogo, jambo ambalo si zuri hata kidogo.

Sheria hazikutungwa kwa ajili ya kuwabana wadogo tu au watu wasiokuwa na nyadhifa zozote katika jamii. Sheria ni msumeno unaokata bila kuangalia wadhifa wa mtu, kabila la mtu au jinsia ya mtu.

Hivyo basi, tunaamini ya kuwa sakata hili la ufisadi katika Benki Kuu halitaishia chini chini baada ya watuhumiwa kurudisha fedha walizokuwa wamekwapua.

Kitendo chao cha kilikuwa kosa la jinai hivyo ni matarajio ya kila Mtanzania kuliona sakata hili likiishia mahakamani baada ya wahusika kukamatwa na kufunguliwa mashitaka.

Ni lazima tujenge utaratibu wa watu kuogopa kuibia serikali. Wawe wanafanya hivyo wakifahamu fika athari zake kama mwizi wa simu anavyofahamu kwamba akikamatwa akiwa ‘kazini’ madhara yake ni makubwa.
 
So let me get is straight and be clear, both EPA and CIS money is being repaid back to BOT?

What will be actions to those who were involved on EPA? Maana pesa za EPA inasemekana ziliibiwa. Pesa za CIS zilikopwa. We need to distinguish the two and I hope our waandishi will push for clarification from BOT and Centra; Governmement.

Kama ni za EPA ambazo zasemekana Zimeibiwa au Kuhujumiwa kwa kuundiwa makampuni ya mifukoni, je ni hatua gani za kisheria zitafuata?

Hizi za CIS, mikopo inarudishwa baada ya zaidi ya miaka 10. Je wakopaji hawa wataruhusiwa kukopa tena? Je BOT na Hazina zitahakikisha vipi kuwa hawa default borrowers do not receive a positive credit rating for future loans from any financial institution? who will give them a guarantee?
 
So let me get is straight and be clear, both EPA and CIS money is being repaid back to BOT?

What will be actions to those who were involved on EPA? Maana pesa za EPA inasemekana ziliibiwa. Pesa za CIS zilikopwa. We need to distinguish the two and I hope our waandishi will push for clarification from BOT and Centra; Governmement.

Kama ni za EPA ambazo zasemekana Zimeibiwa au Kuhujumiwa kwa kuundiwa makampuni ya mifukoni, je ni hatua gani za kisheria zitafuata?

Hizi za CIS, mikopo inarudishwa baada ya zaidi ya miaka 10. Je wakopaji hawa wataruhusiwa kukopa tena? Je BOT na Hazina zitahakikisha vipi kuwa hawa default borrowers do not receive a positive credit rating for future loans from any financial institution? who will give them a guarantee?

Rev nakuunga mkono...usanii umezidi! Tunadanganywa sana.
Hela za Import Support ndio zinazorudishwa hivi sasa, hizi pesa zilianza kurudishwa pale Waziri aliyepita (Meghji) wa fedha alipoingia pale na kuipa kazi hii Tanzania Investment Bank (TIB). Kabla hajaenda bungeni na kutolewa alitoa 90 days kwa kampuni hizo kurudisha pesa au list kuchapishwa hadharani (shaming) na kufilisiwa. Kampuni nyingi za wakubwa imebidi kurudisha pesa kuepuka aibu.

Hili suala la watu kurudisha hela za EPA ni usanii. Naomba wabunge wetu wademand vitu vitatu April:-

(1) External Collectors - kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu kampuni zilizokopa kwenye IS 10 years ago na zimelipa kiasi gani (tunataka kujua ni riba kiasi gani)

(2) Extenal Collectors - kutupa list ya WEZI wa EPA na kiasi gani wamerudisha mpaka sasa.

(3) Wezi wa EPA wachukuliwe hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria zetu. Hatuwezi kuwa na utawala usiofuata sheria. Sheria ziko wazi.

Kinyume cha hapo usanii utaendelea...
 
Back
Top Bottom