Mpokea Rushwa ndiye anatakiwa kupewa adhabu. Hiyo ndio namna Bora ya kupambana na Rushwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
Habari zenu Wakuu,

Nafikiri tuwe Serious kidogo kama tumedhamiria kupambana na Rushwa. Ili Rushwa iondoke lazima mmoja kati ya Mla Rushwa na Mtoa Rushwa mmoja wapo ndiye apewe adhabu huku mwingine akiachwa salama. Hii itasaidia Kwa kiwango kikubwa kukabiliana na tatizo la Rushwa.

Huwezi kupambana na Rushwa kwa sheria inayosema Mla Rushwa na mtoa Rushwa wote ni Wakosaji. Hapo automatically umeshawapa jinsi ya kujihami, na kujilinda, pia umewapa umoja ambao kwao ni nguvu.

Ni lazima Kanuni ya Divide and Rule itumike pia kwenye jambo hili ili kulilidhibiti. Kumfanya mmoja kuwa mhanga huku mwingine kuwa mkosaji ni kuwagawanya na kuwafanya wasiwe wamoja. Hii ni rahisi kudhibiti Rushwa.

Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Mabepari na Mabeberu siku zote huwa ni wapuuzi. Upuuzi wa kujifanya, wanayoyafanya hayana athari na madhara.
Watoa Rushwa wanyongwe kwanza halafu tuwashugulikie walwa rushwa kwa kuwataifisha mali zote zilizotokana na Rushwa waliozipata. Kwa hayo tutaona kupunguzika kama sio kukomesha Rushwa na wale wanaofikiri wana njia za kufanya Ufisadi kwa kutanguliza Rushwa, vilevile kutoa matamanionya wala Rushwa kuona kuwa hakuna watakalo faidika nalo kwa kupokea rushwa.

Hakuna njia moja peke yake.
 
Back
Top Bottom