Mpina: Mawaziri wapatikane kwa njia ya Ushindani siyo Uteuzi ili tupate Mawaziri Bora badala ya Bora Mawaziri!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,009
142,042
Mbunge wa Kisesa mh Luhaga Mpina amependekeza Mawaziri wapatikane kwa njia ya Ushindani badala ya Uteuzi kama ilivyo sasa

Mpina amesema hatua Hiyo itapelekea kupata Mawaziri wenye viwango siyo mizigo

Kwanini Serikali isiache utaratibu wa ajira kwa njia ya uteuzi ili kupata watu wenye uwezo ambao hawatiliwi mashaka, ajira ipatikane kwa njia ya ushindani iwe kwa viongozi, watendaji, Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na watendaji wengine Serikalini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Paschal Katambi akajibu “Kwa sasa Katiba yetu ya Mwaka 1977 inaeleza mfumo wa uendeshaji wa Serikali na inatambua mifumo ya uteuzi na ushindani kulingana na nafasi zinazohitajika.”
 
Source: Mwanahalisi Digital
Hebu tujikumbushe kidogo, wakati yeye anawapima samaki pale Bungeni, akiwa ni waziri wa Mifugo, alikuwa amepambanishwa na nani?!
 
Luhaga mpina aache ujuaji mwingi usio na maana yoyote ,kakoselewa na Daktari wa uchumi aache kuupapalakia uchumi anaendeleza makasiriko.

Kila mtu akijiona ni mshauri na huku ushauri anaotoa ni wa hovyo unafanya Taaluma za watu zionekane bure
 
Mpina na katiba mpya ni Kulwa Na doto.........over
Mpina anaungana na Watanzania kudai Katiba mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Hatimaye Ule upuuzi wa wataalamu kuacha shughuli zao na kukimbilia Bungeni kuvizia Uwaziri utakoma,

Hatimaye WAZIRI hatatokana na mbunge.

Makundi mengi yanaungana kudai ktb mpya.

Aaamen
 
Ila kivyovyote huwezi sema mawaziri wawe wanashindanishwa, vipi mpinzani akishinda ? Inamaana serikali itakuwa na ajenda nyingi ko ubaki hivi hivi tu huu mfumo labda ndani ya chama wawe wanasema mtu afanye kuomba then raisi aangalie na kuwahoji kisha maamuzi ya mwisho afanye raisi kwa utashi wake

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Mbunge wa Kisesa amehoji
Kwanini Serikali isiache utaratibu wa ajira kwa njia ya uteuzi ili kupata watu wenye uwezo ambao hawatiliwi mashaka, ajira ipatikane kwa njia ya ushindani iwe kwa viongozi, watendaji, Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na watendaji wengine Serikalini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Paschal Katambi akajibu “Kwa sasa Katiba yetu ya Mwaka 1977 inaeleza mfumo wa uendeshaji wa Serikali na inatambua mifumo ya uteuzi na ushindani kulingana na nafasi zinazohitajika.”
 
Aliyeshindwa ujumbe wa NEC ya CCM anaamini anaweza kushinda uwaziri akishindanishwa, kuna tatizo kubwa sana kwenye ufikiri wa watu? Kubali tu uongozi ni kupokezana kijiti , usiumie wala kunung'unika unapoachwa
 
Anaye mpinga Mpina ni mpumbavu,

Katika mchakato wa ushindani hata yeye hana uhakika wa kuwa waziri ila wazi ni kupata mawaziri makini
 
Mbunge wa Kisesa mh Luhaga Mpina amependekeza Mawaziri wapatikane kwa njia ya Ushindani badala ya Uteuzi kama ilivyo sasa

Mpina amesema hatua Hiyo itapelekea kupata Mawaziri wenye viwango siyo mizigo

Kwanini Serikali isiache utaratibu wa ajira kwa njia ya uteuzi ili kupata watu wenye uwezo ambao hawatiliwi mashaka, ajira ipatikane kwa njia ya ushindani iwe kwa viongozi, watendaji, Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na watendaji wengine Serikalini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Paschal Katambi akajibu “Kwa sasa Katiba yetu ya Mwaka 1977 inaeleza mfumo wa uendeshaji wa Serikali na inatambua mifumo ya uteuzi na ushindani kulingana na nafasi zinazohitajika.”
Yuko sahihi tumeona bimkubwa akimzawadia mkwewe uwaziri kisa anamridhisha binti yake
 
Back
Top Bottom