Mpango mkuu wa Waislamu wenye itikadi ya kuinua Khilafa (yaani utawala wa Kislamu)

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,301
3,411
Mpango mkuu wa Waislamu wenye itikadi ya kuinua Khilafa (yaani utawala wa Kislamu)

Mpango huu una mafiga makuu matatu ambayo ni;

1) Kuitwaa Makka
2) Kuitwaa Yerusalemu
3) Kuitwaa Kostantinopo

Mekka

Unaweza kuuliza mbona, Mekka ipo chini ya Waislamu tayari? Ni kweli lakini inashikilia na familia ya kifalme ya ibn Saudi. Uislamu hauna ufalme bali Khalifa. Na zaidi Uislamu wa Saudia ambao ni wa Kiwahabi haupatani na Uislamu mwingine. Mekka kwa mujibu wa dini ilipaswa kuwa ya Waislamu na si kuwa ya kitaifa. Na zaidi Waarabu sasa hawana mpango wa kuwa na khilafa, itawabidi wauwe tawala zao za kifalme na zingine za kidemokrasia kwa maslahi ya khilafa. Jambo ambalo lina kigugumizi.

Kuanzia mnamo karne ya 16 Mekka ilikuwa chini ya Othoman (dola la kislamu la Kituruki). Waothoman waliiweka Mekka katika utaratibu wa kislamu, lakini Waarabu hawakuwataka Waturuki. Baadae katika vita vya kwanza vya dunia, Waarabu wakaungana na Uingereza na Ufaransa na kuiangusha Othoman. Hivyo Othoman ikalazimishwa kuachia mashariki ya kati mnamo 1917 na Khilafa ikaanguka mnamo 1924 kupitia mapinduzi ya Kemal Ataturk ambaye aliunda taifa la Kituruki la sasa.

Waarabu wakataka wakatiwe maeneo ya utawala kama malipo ya umamluki, na hivyo wakaulizwa wanataka aina gani ya utawala, wakachagua ufalme. Waingereza hawakutaka ufalme lakini hao mamluki wa Kiarabu waliwashawishi Wazungu kwamba Waarabu ni watu wa shingo ngumu, hivyo wanahitaji utawala mkali ili kuwadhibiti. Wakaruhusiwa kuanzisha ufalme. Ndipo yakaanzishwa mataifa kama Iraq, Saudia Arabia, Siria, Iraq, Bahrain, UAE ambayo yakatoa ahadi ya uaminifu kwa Muingereza na Ufaransa. Tokea hapo Mekka ikawa chini ya familia ya Ibn Saudi, wanapiga pesa tu za sadaka na hija.

Yerusalemu

Ilitwaliwa na Warumi kutoka kwa Wayahudi mnamo 70 B.K. Na mnamo 325 B.K Rumi ikabadilika ikawa ya Kikristo, hivyo Yerusalem ikawa mji wa Kikristo hadi mnamo 638. Mnamo 570 alizaliwa kijana wa Kiarabu huko Hijaz, akawa nabii wa Waarabu, akaamka asubuhi na kusema ameota ndoto, kwamba ametoka Makka hadi Yerusalemu akiwa juu ya Buraq mnyama mwenye kasi, na kuwasalisha manabii 124,000 katika msikiti wa Alaqsa (ingawa haukuwepo) na kutokea hapo akapaa juu hadi mbingu ya 7 kuonana na Allah. Jambo hili liliufanya Yerusalemu uwe kibra ya kwanza ya Waislamu na ukawa katika ajenda ya kutwaliwa. Hivyo baada ya kufa kwa Muhamad, mnamo 638 B.K waikaitwaa Yerusalemu kutoka katika mikono ya Wakristo wa Kiorthodoksi. Hivyo kwa muda wa miaka 400 Yerusalem ikawa chini ya Waislamu wa kiarabu. Wakajenga msikiti wa Alaqsa na dome of the rock katika ardhi takatifu ya mlima wa hekalu. Majengo hayo yamekuwa chanzo cha vita kati Wayahudi na Waislamu. Mnamo 1070 Waturuki waliosilimu wakaitwaa Yerusalem na kuanzisha zama za vita vya msalaba. Maana ilifika mahali Waarabu, Wayahudi na Wakristo walianzisha mapatano ya kila mmoja afanye ibada katika maeneo ambayo kila mmoja anaamini ni matakatifu. Waturuki walipokuja wakaondoa azimio hilo na kuzuka mapigano makali kati ya Wakristo na Waislamu. Na mnamo 1099 Yerusalemu ikaanguka tena mikononi mwa Wakristo wa Kikatoliki. Waislamu na Wayahudi wakafukuzwa. Ilipofika 1187 Ilianguka tena mikononi mwa Waislamu. Mnamo 1229 hadi 1244 kwa amani ikaanguka mikononi mwa Wakristo wa Kikatoliki kupitia makubaliano kati ya Federiki mfalme wa Roman takatifu (the holy Roman empire) na Al Kamil, Sultan wa Ayyubid wa Misri. 1244-1247 Watatar wakaivamia na kuwaondoa Wakruseda. 1248 -1517 ikawa chini ya dola la kislamu wa Mamluki wa Misri. Mnamo 1517 Waturuki wa Othoman wakaitwaa hadi 1917. Hivyo kwa miaka 500 ilikuwa chini ya Othoman.

Waingereza nao wakaja na kuitwaa kutoka mikononi mwa Othoman mnamo 1917. Yerusalemu kwa miaka 30 ukawa mji usio na mtu (no man land). Muingereza akaanzisha serikali ya kikoloni iliyoitwa mandate of Palestina ikijumrisha na Yordan pia. Wayahudi wengi wakahamia wakaongeza idadi ya waliokuwepo, hivyo idadi yao ikawa juu ya Waarabu. Muingereza akawa katika shinikizo ya kumuachia nani nchi, hasa swali la Yerusalemu. Mzozo ukawa mkali sana juu ya Yerusalemu, ibakie kwa nani, waarabu au Wayahudi. Muingereza akabakia katikati, maana angewapa Wayahudi angepoteza washirika wake wa Kiarabu, na angewapa Waarabu, angekuwa amevuruga kwa madoni wa Kizayuni kina Rothchild waliodhamini vita vya kwanza vya dunia. Hivyo Yerusalemu ikabakia hewani bila kuwa mali ya mtu hadi zama za mwisho wa vita vya pili vya dunia, mvutano ukawa mkali kati ya Wayahudi na Waarabu, hivyo mnamo 1947 Muingereza akalihamishia swali la Yerusalemu kwenye umoja wa mataifa. Huko wakahafikiana Yerusalemu uwe mji huru wa kimataifa chini ya UN. Waarabu walipinga, na mnamo 1948 Israeli ikatangaza uhuru wake jambo ambalo likazua vita kati ya Israeli na Waarabu na kuishia katika mgawanyiko wa mji wa Yerusalemu. Mashariki (mji wa zamani) ukawa chini ya Waarabu wa Jordan, na eneo la magharibi, eneo tupu likawa chini ya Wayahudi. Wayahudi wakaendelea na shughuli zao, hivyo Yerusalemu magharibi ukapiga hatua kubwa sana za maendeleo, ukawa mji wa kisasa. Mnamo 1967, Yerusalemu yote ikaanguka mikononi mwa Wayahudi baada ya Israeli kuwashinda umoja wa Waarabu katika vita vya siku 6. Waarabu waliita nchi yote na Yerusalemu yote na kuwaangamiza Wayahudi milele. Hadi sasa Yerusalemu ipo mkononi mwa Wayahudi, na idadi kubwa ya wakazi wa Yerusalemu ni Wayahudi. Hamas, ni moja ya ajenda ya kuitwaa Yerusalemu. Sasa wanapigana na Israeli kwa makali ya moto, Hezbollah nao wakiwa upande wa Hamas.

Kostantinopo/ Istanbul

Mji huu ulijengwa na Kaisari Kostantino na ukawa kao kuu la dola la Roma mnamo 330 B.K. Hivyo uliitwa kwa jina lake. Mji huo ndio ulikuwa jiji la kisasa la wakati ule hadi zama za kati. Jina lingine unajulikana kama Roma ya pili. Ufalme wa Kostantinopo baadae ulijulikana kama Byzentine, jina la Kigiriki la eneo hilo, maana eneo ulipojengwa mji huo, lilikuwa eneo la Wagiriki. Warumi walikuwa ni wajuzi sana wa ujenzi, hivyo Jiji la Kostantinopo lilikuwa linang'ara sana na sifa zake zilisikika kote katika dunia ya wakati ule, tuseme ilikuwa New York ya wakati ule. Baadae mjukuu wa Kostantino, Kaisari, Justinian wa pili, akajenga kanisa kubwa sana, akaliita Hagia Sophia. Lilikuwa ndilo kanisa kubwa ulimwenguni lenye nakshi za kuvutia. Habari za jiji la Kostantinopo na Kanisa hilo zilifikia hadi katika jangwa la Hijaz katika familia ya kifugaji inayokaa katika mahema huko Makka. Muhamad kijana wa Abdulah kwa zile sifa za Kostantinopo akautamani, alipopata nguvu akatafuta njia ya kuuteka, akashindwa. Hivyo akatabiri kuwa Kostantinopo itaanguka na itakuwa mali ya Waislamu.

Baada ya kufa kwa Muhamad, vita vikubwa vililipuka kati ya Waarabu na Warumi wa Byzentine. Akili ya Waislamu ikaelekea Yerusalemu na Kostantinopo. Wakafumuka kama Nzige toka katika jangwa kavu la Arabia na kutua Siria, Iraq na Yerusalemu, wakazitwaa. Lakini Kostantinopo ilifanikiwa kuzua mashambulizi ya Waarabu toka karne ya 7 hadi karne ya 15. Lakini mambo yalibadirika baada ya kuinuka kwa Wapagani wa Kituruki toka Asia ya kati, Wakasilimu, na mnamo 1299 wakaunda dola la Kislamu la Othoman, wakameza itikadi ya Muhamad ya kuitwaa Kostantinopo, wakapigana na Warumi kwa miaka 154, na hatimaye mnamo 1453 Kostantinopo ikaanguka mikononi mwao. Na kanisa la Hagia Sophia ikawa msikiti. Hivyo ndoto za Muhamad zikatimia. Lakini historia ya kale ya Warumi, Wagiriki na Wakristo ikafa kwa kumezwa na Waislamu. Hadi leo uchungu unawapata Wakristo hasa wa Orthodoksi. Warusi ambao ni Waorthodo ksi walishajaribu kuutwaa mji huo enzi za Peter mkuu na kuendelea lakini hawakufanikiwa kuumiliki ingawa walifanikiwa kuuteka. Lakini baadae ukarejeshwa chini ya Othoman katika kikao cha Paris baada ya Urusi kushindwa na Muingereza, Italia na Ufaransa waliokuja kuisaidia Othoman iliyodhoofu.

Sasa Waislamu wakawa na Makka, Yerusalemu na Kostantinopo. Wakatukuka sana. Lakini sielewi hadi leo utakatifu wa Kostantinopo upo wapi hadi Waislamu wautolee jasho, naona kama ni tamaa ya jiji hilo la kale la Wakristo.

Lakini mnamo 1924 Khilafa ikaanguka mazima hadi leo kupitia mapinduzi ya Kemal Ataturk aliyeondoa dola la Othoman na kumtia nguvuni Sultan mnamo 1922. Akavunja utamaduni wa Kislamu (wa utawala wa sharia) na Kiarabu na kuunda serikali ya jamhuri ya Kituruki isiyo na dini (secular state). Na Kanisa la Hagia Sophia ambalo lilifanywa msikiti na Masultan likafanywa jumba la makumbusho la mambo ya historia. Mwaka juzi, Edrogen rais wa Uturuki akairudisha Hagia Sophia kuwa msikiti. Lakini bado Yerusalemu, Mekka na Kostantinopo hazina hadhi ya utawala wa sharia maana hakuna khilafa. Na ukizingatia Uturuki ipo Nato ambayo imeundwa na nchi zenye historia ya Ukristo.

Sasa ipo harakati inayoendelea ya kuunda khilafa, ni harakati ambayo imeanza kwa kueneza Uislamu duniani kote kwa njia ya miadhara pamoja na kujenga misikiti na kuoa Wakristo hasa Wazungu ili kuongeza uzao wa kislamu katika nchi zenye nguvu za magharibi. Ili baadae waislamu waweze kushika nyadhifa kwenye mataifa hayo na kusimamisha khilafa. Hamas nao ni sehemu ya ajenda katika eneo la Yerusalemu. Lakini Waislamu wengine wanaona khilafa haitaweza kusimama hadi aje Imam Mahd na Issa bin Mariam, ambao ina aminika kuwa watapigania Uislamu na kuwashinda Wayahudi na Wakristo na kuikomboa Yerusalemu, Makka na Kostantinopo na kisha kuunda dola la khilafa dunia nzima.

Na Jeff Massawe
 
Umeandika vizuri, kuna sehemu katikati hapa unaona kabisa hizi dini za uislam na ukristo ni falsafa na tamaduni za watu na sio kwamba zimetoka kwa MUNGU, sisi weusi tunapelekwa tu na tumemezeshwa tamaduni za watu, tupo kama wapagazi tumebeba mizigo ya watu ambao hatujui wanaelekea wapi!!
 
Mungu akijenga Madhabahu yake hapa Shetan nae ujenga Shrine yake pembeni ili kupoteza watu.
The world it was at peace until 567 Shetan brought Islam the rest you know.
Asomae na afahamu.
Nani aliivamia iraq, syria,afghanistan na libya na kuua mamilioni ya watu? Siyo hao wazungu unaowapenda? Congo hadi leo kuna vita anaofadhili hawa waasi ni muislamu? Jifunze kufikiria kidogo sio kufuata mkumbo tu
 
Mungu akijenga Madhabahu yake hapa Shetan nae ujenga Shrine yake pembeni ili kupoteza watu.
The world it was at peace until 567 Shetan brought Islam the rest you know.
Asomae na afahamu.
Dah,soma historia..wahindi wekundu,biashara ya utumwa,mauaji australia,new Zealand,namibia,botswana,nagasaki, and hiroshima,latin america,rome empire,mauaji ya uingereza kule china..orodha ni ndefu,kabla bush hajaingia madarakani 2000,dunia haikua hivi,ilikua tulivu,sana sana ni angola na sierra leone ambako vurugu zilikua na mikono ya wazungu, waislam walikua wakifunga na kuswali tu..
 
Dah,soma historia..wahindi wekundu,biashara ya utumwa,mauaji australia,new Zealand,namibia,botswana,nagasaki, and hiroshima,latin america,rome empire,mauaji ya uingereza kule china..orodha ni ndefu,kabla bush hajaingia madarakani 2000,dunia haikua hivi,ilikua tulivu,sana sana ni angola na sierra leone ambako vurugu zilikua na mikono ya wazungu, waislam walikua wakifunga na kuswali tu..
Huyu hana anachojua zaidi ya chuki zinamsumbua tu, anayeanzishaga mauaji kila siku ni magharibi na hata hii ya ukraine ni hao hao , ukiacha mavita yote aliyosababisha na kuua mamilioni ya watu bila ya sababu
 
Hizo nyepesi nyepesi nilizipata ndo maana wanaanzisha vita nchi za kwao baadae hawakimbilii kwa waarabu wenzao wanakimbilia ulaya huko watazaana na wazungu baadae waje kushika nchi,,,,, ndo maana kituo fulani kimekomalia sana tamthilia za wakina Sultana,,, kwa chini wana agenda zao
 
Huyu hana anachojua zaidi ya chuki zinamsumbua tu, anayeanzishaga mauaji kila siku ni magharibi na hata hii ya ukraine ni hao hao , ukiacha mavita yote aliyosababisha na kuua mamilioni ya watu bila ya sababu
Alilioongea jamaa lipo sio stori ya kusadikika
 
Hizo nyepesi nyepesi nilizipata ndo maana wanaanzisha vita nchi za kwao baadae hawakimbilii kwa waarabu wenzao wanakimbilia ulaya huko watazaana na wazungu baadae waje kushika nchi,,,,, ndo maana kituo fulani kimekomalia sana tamthilia na wakina Sultana,,, kwa chini wana agenda zao
Nani anayeanzisha vita ? Vita zote za nchi za kiarabu zimeanzishwa na marekani hata hapo libya tu kaanzisha yeye kwa manufaa yake , elimu yetu inadhida sana kama mtu mzima hata kitu kama hiki pia unashindwa kudadavua
 
Nani anayeanzisha vita ? Vita zote za nchi za kiarabu zimeanzishwa na marekani hata hapo libya tu kaanzisha yeye kwa manufaa yake , elimu yetu inadhida sana kama mtu mzima hata kitu kama hiki pia unashindwa kudadavua
We pinga ukitaka vimba upasuke ila hio mipango tunaijua na tumeisikia kwa wahusika kabisa
 
Khilafa ni Nini?
Neno "Khalifa" linamaanisha kiongozi au mrithi, na linaweza kutumika katika muktadha tofauti.

1. Khalifa katika Uislamu

Katika Uislamu, "Khalifa" inahusu viongozi wa Kiislamu ambao walirithi majukumu ya uongozi wa Kiislamu baada ya kifo cha Mtume Muhammad. Khalifa wa kwanza alikuwa Abu Bakr, na kisha walifuatia Khalifa wengine wanne (wanaojulikana kama "Khalifa waongofu"). Khalifa huyu aliwakilisha uongozi wa kidini na kisiasa wa Umma wa Kiislamu. Baada ya kipindi hicho, kulikuwa na makhalifa wengi wa kihistoria katika madola tofauti ya Kiislamu.

2. Khalifa katika muktadha mwingine

Nje ya muktadha wa Uislamu, "Khalifa" inaweza kutumika kumaanisha kiongozi au mtawala wa kisiasa katika dola au jamii fulani. Kwa mfano, katika historia ya Kiislamu, Khulafa'a al-Rashidun (Khalifa waongofu) walikuwa viongozi wa kisiasa na kidini wa Waislamu. Pia, "khalifa" inaweza kutumika katika muktadha wa viongozi wa kiimla au watawala katika nchi nyingine, nje ya dini ya Kiislamu.

Faiza fox nyingine atajazia.
 
Back
Top Bottom