Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
SERIKALI imeweka bayana mkakati mpya wa muda mfupi na mrefu utakaosaidia kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kumaliza kikao na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alisema barabara za Morogoro na Ali Hassan Mwinyi, zitagawanywa ili kupunguza msongamano nyakati za asubuhi na jioni.
Lowassa, alisema nyakati hizo magari katika Barabara ya Morogoro yatakayokuja mjini, yatatumia barabara tatu na moja itatumika kwa magari yanayotoka katikati ya mjini kwenda nje ya mji, na kuongeza kuwa utaratibu huo utafanyika pia kwenye Barabara ya Alli Hassan Mwinyi.
Katika mkutano huo, viongozi hao wamekubaliana kuwa zinunuliwe taa za barabarani kwa vile taa zilizopo sasa ni chakavu na nyingine hazifanyi kazi.
Mkoa wa Dar es Salaam, una taa 3,021 zinazofanyakazi wakati nyingine tisa ni mbovu, hivyo viongozi hao wameiagiza Wizara ya Miundombinu kutumia sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 ili kuweka taa mpya katika jiji hilo.
Kadhalika, wamekubaliana kuongeza idadi ya polisi wa usalama barabarani ili kupunguza tatizo la foleni linalochelewesha ukuaji wa uchumi nchini.
Jamani tatizo la foleni ni letu sote, tushirikiane na mamlaka husika kuwaelimisha wananchi kuhusu matumizi sahihi ya barabara na sheria zake naamini tutapunguza kwa kiasi kikubwa kero hii, alisema Waziri Mkuu.
Aidha, maamuzi ya kikao hicho ni kutowavumilia wapiga debe na kuwataka waondoke, kwa madai kuwa wanachangia msongamano wa magari na kuwataka wenye malori kutopita katikati ya jiji.
Hata hivyo aliutaja mpango wa muda mrefu kuwa ni ule wa ujenzi wa barabara za pembezoni zitakazounganisha wilaya hadi wilaya.
Wakati huo huo, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mizengo Pinda, alisema mradi wa mabasi yaendayo kasi utaanza wakati wowote kuanzia sasa na kwamba serikali imedhamiria kutoa sh bilioni 10 kama mchango wake katika kufanikisha mradi huo.
Pinda, alisema mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia na utatekelezwa kwa awamu sita, na kuzitaja barabara husika kuwa ni Morogoro, Kilwa, Ali Hassan Mwinyi na Kawawa.
Habari Leo??