Mpambano kati ya Mzee Steven Wassira vs Tundu Lissu kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya pamoja na tume yao ya uchaguzi

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,022
Huu ni mjadala ambao ulihusisha wanazuoni mbalimbali wa Afrika Mashariki, lakini hoja za Steven Wassira na Tundu Lissu ndizo zilizosababisha cheche ktk mjadala huo.

Wanzuoni walioshiriki mdahalo huo ni pamoja na Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga, Mh.Zitto Kabwe, Dr.Ahmed Yassin, Bi.Benadheta Kafuko, Bi.Fatma Karume, Fr.Kitima, Mzee Steven Wassira, na Tundu Lissu.

Maelezo ya Mzee Wassira yanaanzia ktk dakika ya 3:14. maelezo ya Lissu ni kuanzia saa 1:26:26 ktk link hapo chini.
 
Huyu Mzee Stephen Wassira anasema Tume Huru huonekana kwa vitendo na jinsi mchakato mzima unavyoanza na kuhitimishwa, huku akijaribu kuisifia NEC Tume ya Uchaguzi ya Tanzania eti inafanya kazi vizuri zaidi ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC ya Kenya.

Wakati tunajua uchaguzi wa 2020 nchini Tanzania uliosimamiwa na NEC Tume ya Taifa ya Uchaguzi ulifanyiwa uchafuzi wa wazi kuanzia mchakato wa kampeni za uchaguzi, kurejesha fomu, wagombea wa upinzani kufutiwa haki yao ya kugombea n.k n.k

Nashindwa kumueleza huyu Mzee Stephen Wassira ambaye kumbukumbu za uchaguzi wa Tanzania,wa 2020 ulivyotekwa nyara na serikali ya chama cha CCM ulionekana waziwazi kabisa huku Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Tanzania ilishiriki kikamilifu kuharibu uchaguzi uliohusisha vyama vingi vya siasa vilivyosajiliwa Tanzania kisheria na kikatiba kugombea kuchukua dola kwa njia ya demokrasia iliyo huru na haki kwa vyama vyote na wagombea wote.
 
..huu ni mjadala ambao ulihusisha wanazuoni mbalimbali wa Afrika Mashariki, lakini hoja za Steven Wassira na Tundu Lissu ndizo zilizosababisha cheche ktk mjadala huo.

..wanzuoni walioshiriki mdahalo huo ni pamoja na Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga, Mh.Zitto Kabwe, Dr.Ahmed Yassin, Bi.Benadheta Kafuko, Bi.Fatma Karume, Fr.Kitima, Mzee Steven Wassira, na Tundu Lissu.

..maelezo ya Mzee Wassira yanaanzia ktk dakika ya 3:14. maelezo ya Lissu ni kuanzia saa 1:26:26 ktk link hapo chini.

Thanks for this
P
 
wasira hawezi ku argue na Lisu! Na ni nani alimkaribisha chekechea? wasira ni chekechea
Mkuu Retired , heshima kitu cha bure, usimuite hivi huyu Mzee wetu tupo akina sisi wenye heshima kwa wote wakubwa kwa wadogo, kumuita Mzee Wasira chekechea kisa ni kumlinganisha na Lissu, sio kumtendea haki!.

Lazima tufike mahali Watanzania tujue kutofautisha uongeaji wa ujengaji hoja na upayukaji!. Jijifunze managing diversity kwa kuyakubali maoni ya wengine hata kama hatupendezwi nayo!.

Tena jf ina hazina kubwa ya watu humu ni vile tuu watu humu hawajui!. Tuna watu humu ni waalimu wa Lissu kwenye somo la uongeaji!, kuongea na kujenga hoja, Lissu amejifunzia kwenye school debate za Ilboru, ila hawajisemi humu!. Vurugu za Bungeni: Mhe.Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.

Kuna wengi walimshuhudia Lissu akimkabili JPM kwenye uchaguzi wa 2020, si wengi wanaojua hata huko kwa Lissu kumkabili JPM, kuliumbwa na kauli umba hii Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Jee unaijua sababu au huo uwezo uliozungumzwa hapo?.
P
 
Huyu Mzee Stephen Wassira anasema Tume Huru huonekana kwa vitendo na jinsi mchakato mzima unavyoanza na kuhitimishwa, huku akijaribu kuisifia NEC Tume ya Uchaguzi ya Tanzania eti inafanya kazi vizuri zaidi ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC ya Kenya.

Wakati tunajua uchaguzi wa 2020 nchini Tanzania uliosimamiwa na NEC Tume ya Taifa ya Uchaguzi ulifanyiwa uchafuzi wa wazi kuanzia mchakato wa kampeni za uchaguzi, kurejesha fomu, wagombea wa upinzani kufutiwa haki yao ya kugombea n.k n.k

Nashindwa kumueleza huyu Mzee Stephen Wassira ambaye kumbukumbu za uchaguzi wa Tanzania,wa 2020 ulivyotekwa nyara na serikali ya chama cha CCM ulionekana waziwazi kabisa huku Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Tanzania ilishiriki kikamilifu kuharibu uchaguzi uliohusisha vyama vingi vya siasa vilivyosajiliwa Tanzania kisheria na kikatiba kugombea kuchukua dola kwa njia ya demokrasia iliyo huru na haki kwa vyama vyote na wagombea wote.
Hawa Wazee design za Wasira ndiyo wamewaharibu vijana wengi wa CCM... Wao hakuna baya kwa CCM. Ule uchafuzi wa 2020 kuna mtu kweli mwenye akili timamu anayeweza kutetea.... Atakuwa na undungu na Mahera huyu. Siyo bure.
 
Mzee huyu amekubali kukaa upande wa kushoto dhidi ya HAKI Kwa kubadilishana na siku zake chache zilizobaki.
 
Back
Top Bottom