Ni kama vile hakuna jambo lolote la kuhuzunisha na kusitikitisha lililotokea wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, mpaka sasa hakuna kilichofanyika kwa wafiwa si kwa serikali ya ngazi ya wilaya au mkoa wa DSM.
Kutokana na mkanyagano huo , Familia moja jijini Dar Es Salaam iliepoteza watu sita katika mkanyagano uliotokea wakati maelfu ya wakaazi wa jiji hilo walipojitokeza kuuaga mwili wa Rais John Magufuli. Kijana mmoja kwa jina la Dennis Mtuwa amepoteza mke wake, watoto wawili, na wapwa zake wawili. Walienda kumuaga aliyekuwa Rais wao jana Jumapili katika Uwanja wa Uhuru, lakini hawakurejea tena nyumbani, lakini cha kushangaza serikali ipo kimya si wakati wa msiba na hata baada ya mazishi gharama zote zimetolewa na familia iliyopata maafa.
Serikali iangalie Familia hizi zilizopoteza wapendwa wao , sio jambo tu la RPC kutaja majeruhi pamoja na idadi ya vifo kama vile ni sherehe , lakini pia familia hizi zijue zina haki zao kisheria zikiweza zitafute mwanasheria msomi hili zifungue kesi.
Msimamizi wa shughuli yote ya kuaga mwili wa hayati JPM alikuwa serikali lakini kutokana na uzembe walieshindwa kujipanga kuweka mazingira mazuri ya usalama wa Raia , matokeo yake kusababisha maafa.
Wanasheria mnasemaje kuhusu hili?