Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 44
Pamoja na kuwa kauli mbiu ya hamasa ya Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke ilibuniwa na Mwenyekiti Mbowe wakati wa kampeni, nataka kukanusha hapa kwamba mtu anayejiita Mpaka Kieleweke hapa Si Mbowe. Pamekuwa na jitahida sana za kumhusisha mwenyekiti wetu na Majina mawili hapa mtandanaoni, wakati Chinga alianzisha uzushi kwamba Mbowe ni Philimom Michael, Bwana FMES yeye ameanzisha Mpaka Kieleweke ni Mbowe. Nimekuwa nikifuatilia mienendo na michango ya watu hawa wawili na napenda niweke wazi kwamba hakuna Mbowe kati ya watu hao wawili.
Philemon Michaeil ni mwanahabari ambaye mpaka sasa yuko Dar es salaam.
Mpaka Kieleweke ni kada wa CHADEMA anayezunguka kati ya Dar es salaam na Dodoma.
Hata wakati ambapo mwenyekiti Mbowe akiwa nje ya nchi hawa mabwana wawili wameendelea kutoa michango yao kutoka Dar es salaam. Mathalani kwa sasa Mwenyekiti Mbowe yuko kikazi mashariki ya kati lakini bado mpaka kieleweke anaandikia michango yako toka Dodoma.
Kwa mchambuzi yoyote wa michango ya watu humu atagundua kuwa michango ya Mpaka Kieleweke haiendani kabisa na maoni na misimamo ya Bwana Mbowe katika masuala mbalimbali na kwa ujumla bwana Philemon Michael hana undani wa masuala ya kisiasa hususani yale yanayoihusu CHADEMA.
Nawakatia kheri
Asha