Movie za kibongo huwa zinaniboa hapa

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,553
3,070
1. Lugha zinazotumika, wakati mwengine kingereza si kingereza kiswahili si kiswahili. Mwengine hajui kizungu nae anataka aongee kizungu kwenye movie. Mwengine hajui tofauti ya "L" na "R". Gali badala ya gari, ushauli badala ya ushauri,

2. Neno "MR" hili neno wanapenda kutumia eti unakuta mtu ana mu adress rafiki yake kama MR, sasa toka lini mtu rafiki yako unamwita "Mr Benson" usimwite jina la kwanza , au ndio kuonesha ana hela ,jamani Mr sio cheo :embarassed2:

3. Subtitles mbovu sana! , siku hizi zinaoneshwa kwenye Africa Magic yani unaweza kuzima kwa hasira TV ukakimbia. Kama hawana watu wa kuandika kingereza vizuri basi naomba wasiweke sub titles.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Bado unaangalia hizo tamthilia,wenyewe wanaita"Senema"! Bora uangalie zile za enzi zileee za akina "Cafenol na Aspro!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Mnao ziangalia huwa mnakosa cha kufanya bora niende kuzibua vinyesi kuliko kuangalia Movie za bongo.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Suala la matatizo katika matamshi si la sinema/filamu ni la Watanzania. Si ajabu katika nchi hii kukutana na mtu kapendeza ama mrembo lakini hajui tofauti ya L na R.

Kwa upande wa sinema lawama ni kwa waongozaji (directors) ambao ndiyo makocha wa filamu husika. Director anatakiwa kuwa na ufahamu wa mambo kadhaa ya filamu, lugha n.k. Ila kwa kuwa wanaandikwa magazetini na kubabaikiwa na warembo wasiojitambua (ikiwa ma-director ni wanaume) basi wenyewe roho zao "kwatu"!

Mambo bado.
 
kinachoniudhi zaid ni watu kuigiza badala ya kuvaa uhusika.(JB pekee ndo huwa anaweza kuvaa uhusika wengine huwa wanaigiza)
 
Kweli tumetofautiana..mm huwa siangalii muvi za kibongo ht.
 
BIG UP JB WENGINE WOTE PUMBA! Unakuta CD imeandikwa TRUE LOVE lakini ukiinunua ni ya kiswahil kabisa....WHY? Kwa nini? STUPID!
 
Hizi movie niliacha kuziangalia kitambo maana napataga taabu sana kuzielewa unaweza ukashtuka mtu anakuwa tajiri halafu usijue ni kitu gani kimemfanya awe tajiri. Wanaigiza kwa kiswahili lakini cover la movie limeandikwa kiinglishi. Wanaigiza kwa jazba mda wote utadhani wamefumaniana
 
Mmeulizwa mseme kama uwa mnaangalia au hapana? Yaan wabongo bana. Sasa sisi kujua kama mnaangalia au hamuangalii inatuhusu nin!! Tanzania itaendelea kuwa maskini pamaja nga utajiri wote tulionao just because watanzania
1. Ni walalamikaji tu na si watu wa kuchukua hatua stahiki.
2. Tunawivu wa kipumbavu (I MEAN IT) na si wivu wa maendeleo (if you doubt of what i say just pass through the comments on this thread utadhan wametukanwa kutajiwa tu bongo moves. Kwa hali hii kweli hyo industry itakuwa??)
3. Wepesi wa kukata tamaa
4. Tunamtaukuza mgeni na kumsahau mzawa etc, na tabia hii ni mpaka kwa viongozi wetu. Just to look on the film industry mnayo iponda sasa hapa bongo. Haina sapot kbsa ktoka central government ukilinganisha na nchi zingine. Leo hii akitokea mzungu anakuja kuwekeza ktk film industry Tanzania, utaona jinsi serikali itakavyo geuzia macho, pua na masikio kwake. Chukulia mfano kwenye madini. Ki2 kibaya zaidi kinakuja kwa mashabiki. Huko ndo usiseme, hawanunui kazi, utakuta wanapangana tu kwenye vibanda ku-burn movies. Sasa hapo mtu anafaidika vp na lini atatoa kazi nzuru imfaidishe. Remember every thing under the sun is busness pale tu pesa inapoingilia kati, na ktk busness hakuna anaye tegemea kutoa kitu bora ili kiishie tu mikonon mwa wajanja/wajinga wachache, kwakuwa kila kilicho bora kinagharimu. Binafsi siwalaumu. Nailaumu jamii nzima ya tz+viongozi wake na kazi zao nanunua na nnazpenda. By the way filam ya kiswahl kuwa na title ya kingereza sioni tatizo provided English is an international language na filamu si kwa ajili ya wabongo tu.
 
tatizo ni dogo sana, PROFFESIONALISM. people dont turn it as a proffesion, wanaishia kuigiza kwa uzoefu. Wenzetu wa Nigeria na Kenya wamesomea, cheki South Afrika yenyewe, that is the fact, tulitupilia mbali masomo ya sanaa za maonyesho enzi za ujamaa tukidhani yanapoteza muda kumbe ndio ajira tarajiwa za vijana wengi.
 
Title nyingi ni za kiingereza...halafu kwa uchunguzi wangu zinazoanzia na neno "FAKE" ni nyingi...mara FAKE....., FAKE LOVE, FAKE PASTOR etc
 
Back
Top Bottom