ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
Very sad news- MWANZA.
Usiku wa kuamkia leo, majira ya 01;00hrs, maeneo ya BUGANDO HOSPITAL, jijini mwanza, nyumba moja imeungua moto na kugharimu maisha ya watoto watano. Chanzo cha moto huo ni mshumaa ambao uliwashwa na mama mzazi wa watoto watatu kati ya watano waliofariki na kuutelekeze na kutokomea kusikojulikana. Mama huyo alipigiwa simu na wapangaji wenzie usiku huo wa manane, alipofika na kushuhudia miili ya watoto, alizimia mpaka sasa amelazwa BUGANDO HOSPITAL.
Watoto walifariki katika ajali hiyo, ni LATIFA 9YRS; MAYIWA 7YRS; JOSHUA 7YRS; LAURA 3YRS NA ERICK 3YRS. Watoto hawa ni kati ya saba waliokuwa ndani ya chumba hicho, wawili kati yao ni msaidizi na mtoto mmoja wa mama huyo waliookoka na dhahima hiyo.
MUNGU AWAPUMZISHE WOTE WOTE WALIOFARIKI KATIKA TUKIO HILI. NA wazazi tuwalinde watoto na majanga ambayo tukijipanga tunaweza kuyazua, tuache mazoea.
updates.
Chanzo halisi cha tukio hilo, imebainika kuwa huyu mama wa watoto alikuwa ameolewa na ana mme wake wanaishi pamoja. lakini baadaye akaamua kutifuana na mme wake. mwanamme akaona isiwe ugomvi ndani ya nyumba akamua kuhama na kwenda mbali na nyumbani kwake ili ampe uhuru mke wake afanye aliyoyakusudia.
siku ya tukio, ilikuwa ni wiki moja baada ya mwanamme kuondoka, mwanamke akaenda kwa hawara wake mpya kupata huduma ya kikubwa, ndipo mauti yalipowakuta watoto wake, naye kuitwa saa saba usiku na kuja akitokea kwa hawara alikoenda kula uroda