MOTO waunguza nyumba na kusababisha vifo vya watoto watano

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,906
6,909
Very sad news- MWANZA.

Usiku wa kuamkia leo, majira ya 01;00hrs, maeneo ya BUGANDO HOSPITAL, jijini mwanza, nyumba moja imeungua moto na kugharimu maisha ya watoto watano. Chanzo cha moto huo ni mshumaa ambao uliwashwa na mama mzazi wa watoto watatu kati ya watano waliofariki na kuutelekeze na kutokomea kusikojulikana. Mama huyo alipigiwa simu na wapangaji wenzie usiku huo wa manane, alipofika na kushuhudia miili ya watoto, alizimia mpaka sasa amelazwa BUGANDO HOSPITAL.

Watoto walifariki katika ajali hiyo, ni LATIFA 9YRS; MAYIWA 7YRS; JOSHUA 7YRS; LAURA 3YRS NA ERICK 3YRS. Watoto hawa ni kati ya saba waliokuwa ndani ya chumba hicho, wawili kati yao ni msaidizi na mtoto mmoja wa mama huyo waliookoka na dhahima hiyo.

MUNGU AWAPUMZISHE WOTE WOTE WALIOFARIKI KATIKA TUKIO HILI. NA wazazi tuwalinde watoto na majanga ambayo tukijipanga tunaweza kuyazua, tuache mazoea.

updates.

Chanzo halisi cha tukio hilo, imebainika kuwa huyu mama wa watoto alikuwa ameolewa na ana mme wake wanaishi pamoja. lakini baadaye akaamua kutifuana na mme wake. mwanamme akaona isiwe ugomvi ndani ya nyumba akamua kuhama na kwenda mbali na nyumbani kwake ili ampe uhuru mke wake afanye aliyoyakusudia.

siku ya tukio, ilikuwa ni wiki moja baada ya mwanamme kuondoka, mwanamke akaenda kwa hawara wake mpya kupata huduma ya kikubwa, ndipo mauti yalipowakuta watoto wake, naye kuitwa saa saba usiku na kuja akitokea kwa hawara alikoenda kula uroda

 
duh.pigo kubwq sana...mwanga wa milele uwaangazie na uwatie matumaini wafiwa
 
yani najiskiaga vibaya sana kuskia mtoto anakufa kwa uzembe kama huo, huyo mama aliwasha mshumaa na alienda wapi usiku wote huo? R.I.P MALAIKA
 
yani najiskiaga vibaya sana kuskia mtoto anakufa kwa uzembe kama huo, huyo mama aliwasha mshumaa na alienda wapi usiku wote huo? R.I.P MALAIKA

wa mama siku zote mna mambo yenu ambayo hamtaki yafuatiliwe agel. na inavyo onekana mama huyu hajaolewa, ni mama wa mjini tu
 
Ma-mama ya siku hizî ni kero tupu! Ukute mb.ny imewashwa usiku likaenda kuoshwa! Nyamb..f limeacha watoto wanakufa kwa uzembe! Linazimia kitu gani badala ya kufa kabisa?
 
Mwanamke ni mlinzi wa nyumba na mume wake ,sasa huyu mama sijui usiku wote alienda fanya biashara haramu au la!
 
Ma-mama ya siku hizî ni kero tupu! Ukute mb.ny imewashwa usiku likaenda kuoshwa! Nyamb..f limeacha watoto wanakufa kwa uzembe! Linazimia kitu gani badala ya kufa kabisa?

pengine anajutia maamuzi yake ya kutoka usiku na kuwatelekeze wanae. na sijui kama alikuwa na li baba fulani litajisikiaje.... mauaji makubwa tu
 
Hii ilishawahi kutokea hapa Songea mjini mtaa wa Bombambili! mama wa watoto wawili aliwasha mshumaa, kisha akawafungia chumbani watoto wake wakiwa wamelala, akapeleka chakula kwa hawara yake! wakati bwana wake akiwa anawahangaikia kutafuta chochote cha kujikimu! mshumaa ulipoisha ukashika kwenye godoro watoto waliungua vibaya sana! mazishi yao yalikuwa na majonzi sana! ni kati ya miaka 3 au 4 iliyopita, leo tumeshasahau yamejirudia tena huko Mwanza!
Haya yote kwa upande mwingine yanasababishwa kutokuwepo kwa umeme wa uhakika!
ENYI AKINA MAMA na TANESCO, TUONEENI HURUMA! mtatumaliza!!
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi,
 
Hii ilishawahi kutokea hapa Songea mjini mtaa wa Bombambili! mama wa watoto wawili aliwasha mshumaa, kisha akawafungia chumbani watoto wake wakiwa wamelala, akapeleka chakula kwa hawara yake! wakati bwana wake akiwa anawahangaikia kutafuta chochote cha kujikimu! mshumaa ulipoisha ukashika kwenye godoro watoto waliungua vibaya sana! mazishi yao yalikuwa na majonzi sana! ni kati ya miaka 3 au 4 iliyopita, leo tumeshasahau yamejirudia tena huko Mwanza!
Haya yote kwa upande mwingine yanasababishwa kutokuwepo kwa umeme wa uhakika!
ENYI AKINA MAMA na TANESCO, TUONEENI HURUMA! mtatumaliza!!
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi,

ni kweli kuwa ukitafuta sababu za yote hayo, kutokuwa na wanaume wa uhakika ni chanzo. lakini kwa nini mwanamke aamue kuzaa wakati hana mme wa kusaidiana kulea watoto? si atumie njia za uzazi wa mpango kama anashindwa ku abstain?

tatizo la wanawake, wanataka kutumia watoto kama kitega uchumi chao, kwa hata kama mwanaume amekuktaa, akizaa naye atawaonea huruma wanawe na kutoa hela, dhana ambayo ni potofu kwelikweli
 
Kwanza Mungu azipumzishe roho za malaika hao salama. Mama wafiwa poleni sana pia.

Hapa kuna kitu ambacho nataka nikieleze kwa umakini zaidi kwa mtazamo wangu wa kiualimu. Mara kwa mara wazazi ndio walinzi wa kwanza wa watoto kabla hata ya mtu yeyote. Inaonekana majukumu haya yanakuwa magumu miongoni mwa wazazi wote yani wakike na wakiume. Na hii intokana na mambo megi sana ikiwepo ugumu wa maisha au kuwajibika katika kusaka hela zaid lakin kubwa zaid ubinafsi wa wazazi wenyewe. Sisemi haya kama kufurahisha bali kama kuutoa ukweli niuonao katika jamii wa fikira mgando ambazo hata siku moja hazitujengi.

kutokana na tabia za wazazi kama hizi tumejikuta akila mara tunapoteza watoto kwa njia ambazo zinzsikitisha sana kwa mfano kupigwa na kunyanyaswa, kutolewa kafara(japo hawasemi hadharani) na hata kwa majanga ambayo wangeweza kuepukwa.

Hebu tujiulize miaka ya 1995-1999 si kumbuki mwaka vizur kuna familia iliwahi kupoteeza watoto 4 ndani ya nyumba kwa kusuffocate baada ya kuekewa jiko la mkaa chumbani huko Machame mkoani Kilimanjaro. Ukweli ulikuwa kwamba watoto walivuta hewa ya Co kwa hivyo wakakosa O2. Je hapa tulijifunza nini juu ya kuwalinda wanetu? manake baba na mama walikumbatia mablanket ya gharama wakawaacha watoto na vijishuka na jiko je huo si ubinafsi? Lakini baadae ilikuja kusemekana kuwa wazazi wale walitaka mali na ilithibitika baada ya wale wazazi kupata mali nyingi sana baada tu ya ue msiba mkubwa. hilo tuliache

mwaka juzi kuna watoto walifia kwenye ukumb wa disco huko tabora nafikir tena ilikuwa wamekwenda disco toto katika ukumbi ambao ventilaation ilikuwa poor. hapa tena nilijiuliza hivi mzazi unaweza kumwambia mwanao aende disco wewe ukiwa umekaa nyumbani tu?kama unania ya kumfurahisha mtoto si unaenda naye kwa usalama zaidi?

haiishii hapo yapo mengi sana ambayo nikiyaandika hayawez kuisha leo, ila turudi tuangalie hili la leo. Mama amewafungia watoto ndani na mshumaa yeye akatoka, bahati mbaya mshumaa ukawasha nyumba sasa hapa nina maswali kadhaa ya kujiuliza
1) je huyu mama anajua tabia za mshumaa. ni dhahiri kuwa anajua na ndio maana hajawah kuuwasha kisha akaishia usingizini akiwa ndani. kwa maana hiyo napata hisia kuwa alitaka haya yatokee.
2) je kwa yeye kutoka ndani na kuwaacha watoto peke yao aliwaza nini juu ya usalama wa watot? au yeye alifikiria tu kile kinachompeleka huko anakokwenda? huu ni ubinafsi
3)je baba wa hawa watoto alikuwa wapi? au ni marehem? au ni ile staili yetu ya single parented? hapa pia naona Mungu ameruhusu hili kwani alijua dhahiri kuwa kuendelea kuwaweka hai hawa watoto basi wazazi hawataweza kuwalea wafikie pale alipokusudia wafike bali wanatengeneza kizazi cha watoto wasiokuwa na maadili ambao watakuja kulaumiwa wakati kosa ni la mzazi. hapa nina focus moja kwa moja watoto kama akina LULU

USHAURI KWA WAZAZI
Jamani tubadilike. tuone kuwa watoto ni amana ambayo tumepewa na inabidi tuitunze ili iongezeke thamani manake mwenye nayo ambayo ni taifa atakuja kutuuliza. hebu jifikirie kma ni wewe mama yako angekuacha kwenye hatari je ungekuwa hivyo ulivyo hai? pengine ungekuwa umekufa au ungekuwa ni kilema. hebu tuwapende watoto wetu na tuwalee kama kitu cha thamani kwetu.
 
Ama kweli imenitouch sana!
Imenikumbusha tena janga kama hili iliyotekea hapa A town mtaani kwangu miezi nne iliyopita hapa mtaani kwetu kwa mama kuwafungia watoto wawili ndani na yeye kwenda kurusha roho huko anakojua na ndipo kurudi akakutana janga hilo na leo tena yamejirudia,
ama kweli wamama wanatugharibu nyakati hii na kutupotezea Taifa la kesho!

MUNGU WETU WA HURUMA,wape rehema yako wanao na MWANGA WA MILELE UKIWAANGAZIA PAMOJA!
 
This reminds me almost seven years ago one day before the election 2005 when our family friend lost a mother and 2 kids by fire. May their soul rest in peace :rip::crying:
 
je na baba wa watoto hao alikua wapi?

taarifa zilizopatikana waligombana na mme wake wiki moja iliyopita baada ya mwanamke kupata hawara mwenye nazo kidogo. mwanamme aliamua kuepusha ugomvi akajing'atua; na siku ya tukio mwanamke alikuwa ameenda kwa hawara yake kupata mamboz
 
Back
Top Bottom