Moto mkubwa unawaka maeneo ya Mwenge kwenye Stendi ya Mabasi

iGodmanhustler

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
609
337
#BreakingNews

Kuna moto unaendelea kuwaka Mwenge ndani ya kituo cha mabasi..


MOTO MKUBWA UKIENDELEA KUWAKA HUKU KUKIWA HAKUNA MSAADA WOWOTE WA FIRE

HIVI NDIVYO BAADHI YA MADUKA YANAVYO ENDELEA KUWAKA MOTO SASA HIVI

GARI LA ZIMA MOTO LIKIWA LIMEFIKA KWA KUCHELEWA ILI KUZIMA MOTO HUO
 
Moto mkubwa umezuka kiyuo cha mabasi cha Mwenge huku kukiwa hakuonekani dalili zozote za zima moto.

Vibaka wanajitwalia kila wakionacho mbele yao na taharuki ni kubwa maana magari yanakimbia hovyo kuondoka mahali hapo.

Ziko wapi jitihada za uokoaji. Kama mjini hali ni hivi vipi huko vijijini.
 
nini kinawaka hapo mkuu mabasi au yale maduka yanayoizunguka stendi ya mabus!
 
Naskia vibaka wanatumia fursa hiyo kujipatia chochote, jana ilikuwa PPF , leo MWENGE, tuwaskie akina Sele Kova wanasemaje!!? kama hawajatuambia ni hujuma za CHADEMA sijui....
 
Na kulivyoo na mbanano, hakuna miundo mbinu ya uokuaji, pole zao wahanga wote!
 
ni moto mkubwa xana aisee, umeanzia kwenye maduka ya vipodoz na unaendelea kusambaa ovyo. Vibaka wanaiba mali polic wanasambaza wa2 kwa mabomu, hali c shwari jaman. Ni vurugu mtafutano! MOTO WAZIDI KUWAKA KUSAMBAA
 
Unaunguza kuanzia maeneo ya vibanda hivi vya urembo sasa unaelekea maeneo kunakofanyika biashara za mitumba. Mpaka muda huu bado hakuonekani juhudi zozote za kuuzima. Wenye maduka wanalia tu hapa yaani ni taharuki.
 
duh..jana moto ppf towe leo moto mwenge...hivi idara ya zimamoto iko chini ya jiji au chini ya wizara ya mabo ya ndani..?
 
ni moto mkubwa xana aisee, umeanzia kwenye maduka ya vipodoz na unaendelea kusambaa ovyo. Vibaka wanaiba mali polic wanasambaza wa2 kwa mabomu, hali c shwari jaman. Ni vurugu mtafutano! MOTO WAZIDI KUWAKA KUSAMBAA

POLISI BANA, hayo mabomu hawaoni yatasambaza moto sehemu nyingine ,si avazali wangetumia hata maji ya kuwasha kwani yangechangia kuzima moto
 
Eeee jamani kila siku ni moto, Mwenyezi Mungu tuangalie wengine hatuna hatia jamani
 
Back
Top Bottom