Mossad, operation bayonet: Jinsi kisasi kinavyoweza kuwa njia bora ya kupata haki yako

Imenikumbusha ASSASINER mmoja kwenye BIBLIA, kitabu cha "WAAMUZI 3:12-26" anaiwa EHUDI. Dah! Mbinu aliyotumia kumuua Mfalme Egloni ni hatari ...

Hawa jamaa wana kipaji hicho tangu enzi hizo.

Hii operation ya kulipa kisasi cha Munich inajulikana kama "WRATH OF GOD."

Anyways, nisimalize uhondo; Nasubiria umalizie namna walivyolipa kisasi ...
Exact mkuu. Hakuna ambaye aliuepuka huo mkono wa mungu
 
kama mambo ya itaendelea ni ya kizamani kama unavyosema wewe, Leo hii kusingekuwa na tamthiliya/TV series mbalimbali zinazorushwa kila leo huku ya leo ikiwa ni muendelezo wa ilipoishia jana.
Mkuu huwezi mfurahisha kila mtu!! Wewe fanya majukumu ukimaliza njoo uendelee mkuu!!!

BTW hata wanaokutukana usiwalaumu maana ni dalili kisa kimetulia!!
 
Kilichoniuma kwenye revenge hii ni kijana aliyeuwawa kimakosa huku mkewe ni mjamzito.
 
kama mambo ya itaendelea ni ya kizamani kama unavyosema wewe, Leo hii kusingekuwa na tamthiliya/TV series mbalimbali zinazorushwa kila leo huku ya leo ikiwa ni muendelezo wa ilipoishia jana.
Sasa mkuu wale wapo kibiashara kuna faida kubwa wanapata na ndio maana wanawadhamini. Sasa ww mwenzangu na mm zaidi ya kuelimishana na kuburudishana hakuna kingine unachopata! Sasa kwann utufanyie hv!?
 
Kisasi ni neno lisilo na ubinadamu kwa baadhi, lakini kwa wengine ndiyo njia pekee waliyojichagulia kupata haki katika kile wanachoamini ni haki yao. Ni mwaka 1972 katika mashindano ya Olympic yaliyopangwa kufanyika Mjini Munich, Ujerumani.

Maandalizi ya kuweka mandhari ya miundombinu katika hali ya kupokea wageni wanaotarajiwa katika mashindano hayo yakiwa yanaendelea, Upande wa pili katika nchi ya Lebanon wanachama wa kikundi cha kigaidi kilichojulikana kama BLACK SEPTEMBER ambacho ni kilikuwa ni kikundi tanzu cha PALESTINE LIBERAZATION ORGANIZATION (PLO) nao walikuwa wakichukua mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo ya Olympic ambayo kwa mwaka huo yalipangwa kufanyika Ujerumani.

Katika mwaka huo Wapalestina kama yalivyo mataifa mengine, waliandika barua ya kuomba ushiriki wa Olympic, Lakini kwa kuwa halikuwa taifa huru na linalotambulika katika jumuiya ya kimataifa, Maombi yao hayakujibiwa. Na hii ilikuwa na maana nyingine kuwa wamekataliwa. Kutokana na hili PLO wakaamua kupanga kushiriki mashindano hayo kinamna nyingine. Na namna hiyo si nyingine bali Kwenda kufanya tukio la kigaidi katika mashindano hayo ambalo litaishangaza na kuisimamisha dunia.

Ilikuwa ni January 1972 wakati ujerumani wakijiandaa na maandalizi, Nchini palestina Viongozi wanne wa juu wa PLO walipanga kukutana kwa siri nchini Beirut kusuka mpango kabambe wa kutimiza adhma yao ya kufanya tukio la kuisimamisha dunia. Viongozi hao si wengine bali walikuwa ni MAHMOUD YOUSEF NAJAD ambaye alikuwa kiongozi wa tatu kwa ukubwa katika PLO, MOHAMED DAOUD UDE aka ABU DAOUD ambaye alikuwa ndiye msuka mipango wa PLO, ALI HASSAN SALAMEH aka RED PRINCE ambaye alikuwa ndiyo kiongozi ushushushu na ujasusi katika operation hiyo ya BLACK SEPTEMBER , na wa mwisho alikuwa ni ABU IYAD ambaye ndo alikuwa mkuu wa ujasusi wa PLO.

View attachment 442813
Ali Hassan Salameh

Katika kupanga na kusuka mikakati, viongozi hao waligundua kuwa hawatoweza kufanikiwa adhma yao bila kupata taarifa za sehemu ambapo mashindano hayo ya Olympic yalipangwa kufanyika. Na taarifa hizo ingewawia rahisi kuzipata kama wangekuwa na urafiki na watu ambao ni raia na wakazi wa Ujerumani. Ni katika hili wakaomba ushirikiano na kikundi cha kigaidi cha ujerumani kilichojulikana kama RAF.

Kufikia mwezi wa 8, RAF walianza kuwakusanyia taarifa BLACK SEPTEMBER kuhusu eneo ambapo Olympic ilikuwa inatarajiwa kufanyika. RAF walipiga picha za viwanja, majengo, watu na vyote vile ambavyo vilionekana vitakuwa vina umuhimu kwa BLACK SEPTEMBER. Haya yote yalikamilishwa na WILL VOLTZ ambaye alikuwa mwanachama wa RAF kwa kipindi hicho.

SIKU YA TUKIO

Ilkuwa ni september 5 1972 majira ya saa 10 alfajiri kikundi cha watu waliokuwa wamevaa mask waliingia katika kijiji cha olympic na kuanza kutafuta wanamichezo wa Israel ambao walikuwa tayari wameshawasili katika kambi. Huku wakiwa katika usingizi mzito, wanamichezo tisa wa israel walikamatwa na magaidi hayo.

Magaidi hayo walianza kuwaua kinyama kwa kumpiga risasi mwanamichezo mmojammoja huku wenzake wakiangalia na kushuhudia. Walikuwa wakitekeleza mauaji ya kinyama kwani walikuwa wakiua mateka mmojammoja katika muda uliopishana lisaa. Magaidi wale wa BLACK SEPTEMBER waliendelea kuwashikilia mateka wanamichezo hao huku wakipaza sauti kwa serikali ya Israel na jumuiya ya kimataifa isikilize matakwa yao.

Kwa upande mwengine asubuhi hiyo ya september 5, Taarifa hizo za mauaji na mateka ya wanamichezo wakizayuni zilifika mezani kwa aliyekuwa waziri mkuu wa israel kwa kipindi hicho aliyekuwa akijulikana kwa jina la Bi GOLDE MEIR. Taarifa hizi zilimshtusha na kumfanya akumbuke unyama wa HOLLOCOUST waliofanywa waisraeli na serikali ya HITLER.

Na kwa haraka Bi MEIR aliliweka tukio hilo la Munich katika kundi la matukio ya kigaidi, na aliona kuwa suluhu ya kukabiliana na tukio hilo haikuwa nyingine bali ni kulipa kisasi kwa wote waliotekeleza unyama huo. Bila kupoteza muda, Bi MEIR alifanya mawasiliano na Bw ZVI ZAMIR aliyekuwa mkurugenzi wa taasisi ya ujasusi (SPY CHIEF) wa nchi hiyo iliyojulikana kwa jina MOSSAD , Hakuishia hapo kwani pia alifanya mawasiliano General AHARON YARIV aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ujasusi wa jeshi (Military inteligence) ili kuona kama kuna uwezekano wa kuokoa mateka.

View attachment 442812
Bi. Golde Meir

Ilipofika majira ya saa 8 mchana siku hiyo, tayari ZVI ZAMIR(Mossad spy chief) alikuwa ameshatua jijini Munich kuomba kutoa msaada kwa serikali ya ujerumani kukabiliana na tukio hili. Bila kupoteza muda akapelekwa katika eneo la tukio ambapo mateka walikuwa wameshikiliwa. Wakati bwana ZAMIR na waandishi wa habari wakiwa wamezunguka jengo ambamo ndani yake walikuwa wameshikwa mateka, magaidi wale walitumia nafasi hiyo kupaza sauti ya kutaka waliokuwa takribani wafungwa 240 wa Kipalestina na Kijerumani(RAF) waachiwe huru. Baada ya madai hayo kufika kwa bwana ZAMIR, moja kwa moja aliandika Telegram na kuituma Tel aviv kwa Bi Meir.

Kwa hali ya ushujaa, Bi MEIR hakukubali madai hayo na alikataa kabisa kuingia katika meza ya majadiliano na magaidi hayo na badala yake alitaka wanamichezo wake waachiwe huru bila masharti yoyote.

...muendelezo ilipoishia(Part 2)

Ncini israel habari kuu kwa siku hiyo ilikuwa ni juu ya habari ya kutekwa kwa wanamichezo wao, Wananchi walijawa hofu na kuonekana wakifuatilia kwa makini kisa hicho katika vyombo mbalimbali vya habari. Katika hali ya kuonekana kuwa wataonekana dhaifu, Serikali ya ujerumani ilikataa msaada wa israel katika kukabiliana na tukio hilo. Badala yake waliagiza vikosi vyao vya usalama na ujasusi kwenda kufanya kazi ya kuwaokoa mateka na kuwakamata magaidi hao.

Kabla hilo halijafanyika, jioni ilikuwa imeshaingia na magaidi wakatoa madai ya kutaka wasindikizwe kwenda uwanja wa ndege wakiwa na mateka hao. Hii iliwafanya polisi kuibuka na mbinu kwamba wakubali maombi hayo na kuwategea watakapofika uwanja wa ndege basi wawashambulie na kuwakamata magaidi hao. Kwa bahati mbaya wakati magaidi wanafika uwanja wa ndege polisi waliwavamia na kuwashambulia.

Katika hali ya kupanic, majibizano ya risasi baina ya polisi na magaidi yakaibuka. Wakiwa wanaelekea kushindwa, Magaidi waliona hakuna njia nyingine zaidi ya kujitoa muhanga. Mmoja wa magaidi alichukua bomu la kutupa kwa mkono na kulilipua. Hii ilipelekea magaidi watano pamoja na mateka wote kupoteza maisha papo hapo. Magaidi watatu walibaki hai, na polisi waliwakamata na kuwaweka korokoroni.

Ni simanzi na majonzi vilitanda jijini Munich kufuatia tukio hilo, kamati ya olympic iligoma kusitisha mashindano hayo kwani ingeonekana ni woga uliokithiri. Hivyo baada ya maombolezo, Mashindano yaliendelea bila ushiriki wa wanamichezo wa Israel. Wanamichezo wa israel waliosalimika walirejea israel na simanzi.

Wakati magaidi wakishangilia ushindi huo, nchini israel Bi MEIR aliitisha kikao cha usiri mkubwa (Top secret) cha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Waliunda kamati waliyoipatia jina "COMITEE X" kiongozi wake akiwa ni mkuu wa kitengo cha ujasusi cha jeshi la Israel (millitary inteligence) bw. AHARON YARIV. Kamati hiyo iliibuka na ajenda ya kulipa kisasi cha unyama waliofanyiwa ama kwa lugha nyingine waweza sema "terrorizing the terrorists". Bw. YARIV ni muumini wa kulipa kisasi kwa njia ya kimya na kutojulikana (quiet and clean revenge). Njia hii ilikuja kuridhiwa na kamati hiyo, kwani ndani ya miezi miwili toka tukio hilo la mateka wa olympic litokee, Wapalestina waliteka ndege ya shirika la Lufthansa wakidai kuachiliwa huru kwa wale magaidi watatu. Serikali ya Ujerumani ilitii sharti hilo, na kuwaachia magaidi wale.

Kitendo hicho kilifanya Israel ione haina mshirika, na hivyo kupanga kulipa kisasi yenyewe kama yenyewe kimya kimya na bila kutambulika (Quiet and Clean revenge). COMITEE X ilichagua kikundi maalum cha mashushushu wa mossad ambao wangekamilisha kuwatafuta popote walipo wafanikishaji na washiriki wote tukio lile la september 5. Ndani ya mossad kazi ya kukusanya taarifa za wahusika ilianza huku bi MEIR akipewa taarifa ya kila hatua kwa ukaribu.

Katika taarifa hizo, Jina la ALI HASSAN SALAMEH likaibuka kama ndo mpangaji mkuu na mfanikishaji wa tukio hilo. Baada ya taarifa hizo kuibuka, Bi MEIR alimchagua jasusi mkongwe wa mossad MIKE HARARI kuongoza timu ya mashushushu wenzake waliochaguliwa ili kufanikisha lengo hilo la kulipa kisasi. Majasusi hao waliondolewa official links zote ambazo zingeweza kuwahusisha na israel pindi watakaposhtukiwa.

Hivyo walipewa passport za nchi nyingine na nyaraka mataifa mengine kwa ajili ya utambulisho. MIKE HARARI alichagua jiji la Paris kama makao makuu yake ya kuendeshea oparesheni hiyo. Alikaa Paris na kujifanya mfanyabishara kwa jina la EDWARD LATSKI. Hapo alipanga vikosi kazi vyake kwa ajili ya kutekeleza visasi.

View attachment 442873
Bw. Michael Harari.

KULIPIZA VISASI

Kufikia mwezi october, taarifa zilikuwa zimekusanywa kwa kiwango kikubwa na majasusi wa mossad zilianza kufanyiwa kazi. October 16 timu ya assasins wa mossad walitua jijini Roma, Italia. mtu wao wa kwanza kuuliwa katika list alikuwa ABDELWAHEL ZULETA. ZULETA alikuwa ni mkarimani katika ubalozi wa Libya nchini Italia. Bwana ZULETA alikuwa na mahusiano ya karibu na PLO. Mossad walikuwa na taarifa kuwa ZULETA alihusika na Logistic ya tukio la Munich. takriban majira ya saa 4 usiku, ZULETA akiwa anarejea nyumbani kwake toka kazini alipigwa risasi 11 zilizomuingia kisawasawa mwilini. ZULETA alikufa papo hapo, na taarifa za kifo chake zikatumwa kwa Bi MEIR. mamlaka ya polisi ya italia walifika eneo la tukio na kukuta maganda ya risasi zilizotumika. Maganda yale baada ya kuchunguzwa yalionekana kutoka katika bunduki aina ya BARETTA. Bunduki iliyopendelewa kutumiwa sana na Mossad. Lakini polisi hawakufanikiwa kung'amua lolote kuhusu wahusika wa mauaji ya bwana ZULETA .

DECEMBER 1972, Ufaransa. Dr MAHMOUD HAMSHARI, msemaji wa PLO nchini Ufaransa alikuwa akiishi katika nyumba namba 175 LUDA LESSIA na familia yake. Kutokana na kazi yake, ilikuwa ni kawaida kwa Dr HAMSHARI kukutana na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari. Siku moja mwezi huo alipokea maombi toka kwa mtu aliyejifanya ni muandishi wa habari akitaka kumuhoji. Masikini Dr Hamshari alishindwa kugundua kwamba mtu aliyeomba kukutana naye hakuwa mwandishi wa habari kama ayeye alivyodhani. Ila mtu huyo alikuwa ni Jasusi wa Mossad. Interview hiyo ilifanyika mahali alipokuwa akiishi, Wakati interview ikiendelea, yule shushushu alikuwa akiangalia na kuchunguza kwa makini nyumba ya Bw HAMSHARI na kukusanya taarifa muhimu ambazo zingewasaidia kutekeleza mauaji ya msemaji huyo wa PLO na baada ya mahojiano jasusi yule aliondoka. Siku inayofuata jasusi yule aliamkia katika mgahawa mmoja uliokuwa karibu na alipokuwa akiishi Dr. HAMSHARI na kuanza kuangalia movements zote za watu wanaoingia na kutoka katika jengo alilokuwa kapanga Bw. HAMSHARI. Alipoona mke na mtoto wa Dr Hamshari wametoka kwa mizunguko, Alipiga simu katika simu ya mezani iliyokuwa katika nyumba ya Dr HAMSHARI. Pasipo kujua Dr HAMSHARI alipokea simu ile, na hiyo ilipelekea vilipuzi vilivyokuwa vimepandikizwa katika simu ile kulipuka na kujeruhiwa vibaya hali iliyopelekea kupoteza maisha mwezi mmoja baadae.

..... Itaendelea

naongezea mkuu....!! huyo jasusi aliyefanya interview na hamshari baada ya kuchunguza mazingira ya nyumba kesho yake alikuja na van karibu na nyumba yake ndani kukiwa huyo jasusi na vifaa vya kuweza kujiunganisha moja kwa moja na simu ya hamshari, baada ya kujiunganisha walianza kutibua simu alizokua anawasilina na watu wengine baada ya muda alipiga simu kwenye kampuni ya simu ili waje warekebishe jamaa akawa anakata mawasiliano mpaka baadae ndipo walimpigia na kujitamblisha kwamba wanampigia kutoka kampuni ya simu. hamshari alielezea shida yake na jamaa walimwambia kwamba wangetuma mtu siku ya pili lakini hamshari alikataa na kusisitiza alihitaji arekebishiwe siku hiyo hiyo ndipo hatimae asubiri fundi atakwenda. ikumbukwe hawa jamaa walikuwa umbali sio mrefu kutoka nyumbani kwake, waliona kila aneingia na kutoka. walipoona watoto na mke wametoka, ndipo huyo jasusi alikwenda akiwa kavalia sawa sawa na mfanyakazi wa kampuni ya simu, alifika pale na kujitambulisha kwa mlinzi, mlinzi alipouliza aliambiwa ni kweli amewapigia, hamshari alikuwa na ulinzi mkali. jamaa aliingia ndani na alipoonyeshwa simu ilipo alienda na kuanza kuifanyia kazi ya kuweka bomu. jamaa kwenye van walizuia simu zote kwa wakati huo, bomu lilikua lilipuke baada ya kupokea simu. jamaa baada kumaliza na kuaga, alirudi kwenye van ndipo walimpigia simu alipopokea tu, likalipuka na kumchana chana vibaya kuanzia tumboni mpaka kwenye mapaja, alifariki baada ya siku chache....
 
Kisa kizuri sana, hivi visa kama hivi mnavipataje? maana sie wengine isingekuwa wewe na mtu kama The bold hakika tusingekuwa tunajua chochote.
 
Historia nzuri sana tunashukuru sana kiongozi kwa kazi nzuri, nimepata heshima kwa baadhi ya wanajamii yangu kuwapa sehem tu ya visa vya namna hii. Ombi langu ni kwamba, kama unaweza nipa list ya documentaries, Vitabu au Movies zinazoelezea harakati mbali mbali za WanaIsrael ili nizitafute na kupata ujuzi zaidi juu ya harakati zao. Natanguliza shukrani.
 
Naskiaga yule mmoroco baada ya kuuwawa mke wake wakimlipa fidia hela nyingi lakini hawakumuomba msamaha.

baadaye walimtumia mwanamke kuja kumuua yule waliokuwa wanamtafuta. walimuua kwa bomu la garini ambalo lilikuwa linatumia remote.

kaktika operation iliyoharibu sifa ya MOSSAD ni hii. maana kuna maafisa wake walikamatwa huko norway kama sijakosea.

nadhani sijaharibu ila nakumbuka tu hapa
 
Upo sahihi kabisa boss
 
Kisa kizuri sana, hivi visa kama hivi mnavipataje? maana sie wengine isingekuwa wewe na mtu kama The bold hakika tusingekuwa tunajua chochote.

Mkuu visa kama hivi huwa vipo documented kwa njia ya vitabu ama documentry ya video.
 
Back
Top Bottom