Mei Mosi: Upo uhusiano kati ya maslahi Bora na mfanyakazi kuwa na kitambi?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,352
12,687
Niliowaona kwenye maandano siku ya mei Mosi, 85% ya wafanyakazi walioandamana mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Rais walikuwa na vitambi, viribatumbo. Yaani body mass index (BMI) zao ziko juu, kwa maana nyingine walikuwa na uzito mkubwa kuliko matarajio.

Maswali ni, je, wafanyakazi walioandamana:
1. Wanawakilisha wafanyakazi walio wengi?
2. Kwa vitambi hivi ni kweli wafanyakazi wano kipato kidogo?
kikubwa?
3. Wanakula rushwa?
4. Wanawaibia waajili wao mali au muda wa mwajili kupata ziada?
5. Wanahitaji nyongeza?
6. hakuna uhusiano kati ya mshahara mkubwa na kuwa na kitambi?

====

Pia soma:
Dkt. Mpango: Serikali imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni zake
 
Hahaha! 🤣
Ni kutozingatia milo sahihi mkuu. Angalia madereva bajaji wengi Wana vitambi
 
Hahaha. Nipo hapa Arusha, umesema kweli. Vitambi kedekede.
 
Walimu ndio kundi pekee ambalo wengi wao sikuona vitambi vingi kwao. Kuna uhusiano kati ya kula na kitambi. Kama huli chakula kingi kuliko mahitaji ya mwili huwezi kupata kitambi. Mfanyakazi anafanya kazi anatumia ngumu/chakula nyingi.
 
Back
Top Bottom