Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,848
- 15,253
Hali ya taharuki imetokea katika shule ya msingi Narumu, katika Kijiji cha Narumu wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya mama mmoja ajulikanae kwa jina la Valentina Kweka, kuingia ofisi ya walimu na kumpiga Mwalimu.
Mwalimu huyo ambaye ni wa kike (jina limehifadhiwa) alijeruhiwa hivyo kupelekea kutoka damu puani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumchapa mwanafunzi huyo wa darasa la tano fimbo moja kwa kosa la kukataa kudeki darasa.
Mtoto huyo alienda kusema kwa mamake huku akilia ndipo mzazi huyo alipochukua jukumu la kwenda hadi shuleni na kumpiga mwalimu huyo na kumjeruhi.
Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Ismael Urassa pamoja na diwani wa kata hiyo wamethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limefika ofisi ya kata na linashughukiwa.