Uchaguzi 2020 Moshi mjini: Mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli. Asema atafufua viwanda vilivyolala

Kampuni za mabasi za Mtei, Machame, Lim safari na Costline zimekesha zinasomba watu kutoka Simanjiro, Mwanga, Hai, Siha, Rombo, Same na Arusha.
Hivi hii punieto ya kisiasa bado tu wanaamini itawanusuru na kipigo.
 
jibu lako wiki ijayo tu wala sio mbali
mpungue jamii forums ibakie watu wachache baada ya tarehe hiyo tunajua mtatokomea gizani
Wewe ulikuja na upepo wa uchaguzi wa ENL ,sie tupo tangia Chadema wana Dr Slaa humu,wewe ndio utakimbia.
 
Huu uzi ume mute sana. Wekeni na picha. Kuna eneo fulani walijipanga kumpokea naona watu wakakosekana kabisa peupe. Chezea wachagga wewe. Salute shemeji zangu.
 
Kampuni za mabasi za Mtei, Machame, Lim safari na Costline zimekesha zinasomba watu kutoka Simanjiro, Mwanga, Hai, Siha, Rombo, Same na Arusha.
Sawa...kwani tatizo liko wapi?! Chadema tembeeni kwa miguu...nyie haya ya kubebwa na malori, pickups, punda, mikokoteni, bodaboda na bajaji hayawahusu...msiteseke bure...
 
Shekhe Ponda Issa Ponda amesema Kuleni pesa za CCM lakini kura zote Chadema
 
Ila Moshi Kuna watoto wazuri bwana...pisi kali kinoma nawaona kwa Tv
 
Jamani Magu anaua Moshi ni hatari jaribuni kumzuia anatupa mawe wazi wazi tanadondokea katika tusi za watu anaua jamani
 
Lakini ni juzi tu ulipokuwa ukisema, kanda hiyo haidanganyiki!!

Vipi Leo, kunabakora zilipita majumbani kwenu kulazimisha watu wapande hayo mabasi?

October 28 is only next week, after which JPM will be sworn in again at Mkapa Stadium
UKIANGALIA HUKU MOSHI MJINI KWA SIKU YA LEO KILA MTU ANAENDELEA NA SHUGHULI ZAKE NI TOFAUTI NA SIKU ALIOKUJA TUNDU LISU, YANI SHUGHULI ZILISIMAMA KWA MUDA NA BODABODA ZOTE NA BAJAJI ZILIKUA NA BENDERA ZA CHADEMA TENA KWA MAPENZI YAO,
ILA LEO HAPA MJINI SIJAONA SHAMRA SHAMRA KAMA ZILE ZA TUNDU LISU.
 
MAGUFULI: Nawashukuru viongozi wa dini kwa Dua na Sala zao. Ninajua wagombe wenzangu wa ubunge wameeleza yote na mikakati mbalimbali ya chama cha mapinduzi kama ilivyofafanuliwa kwenye Ilani. Nchi yetu imebarikiwa kwa mambo mengi sana, binadamu wa kwanza, mti mrefu, mlima mrefu kuliko yote Afrika, madini ya Tanzanite, Tanzania ni nchi ya pili kuwa na mifugo wengi. ya tatu kwa kuvumbua kiwango kikubwa cha gesi asili na nne kwa kuzalisha dhahabu barani Afrika.

Zaidi ya kilomita 1422 tunapakana na bahari, ina maziwa, mito, misitu, ina vitu mbalimbali. Nchi hii imebarikiwa sana na Mungu. Nchi yetu ni tajiri, miaka mitano iliyopita tumedhihirisha sisi sio masikini, sisi ni matajiri. Tumefanya mambo mengi makubwa tena kwa nguvu zetu wenyewe, najua mengi mnayafahamu.

Katika kipindi cha miaka mitano tuliweza kuanza kukusanya kodi kwa mwezi kutoka bilioni 850 mpaka trilioni 1.5 na kuna baadhi ya miezi tumefika trilioni 1.6. Tumeweza kujenga vituo vya afya, zahanati, kupeleka umeme kwenye vijiji. Kwa kudhihirisha Tanzania ni tajiri tumeanzisha miradi mikubwa. Tumejenga barabara za lami zaidi ya kilomita 3,500 na tunaendelea kujenga kilomita 2,500. Ndege 11, kununua na kujenga radar katika viwanja viwanja vyetu vikubwa kwa kutumia fedha zetu. Tumeanzisha mradi wa kujenga reli ya umeme, treni ambazo zinatumika Ulaya. Ninaweza kutaja miradi mingi langi lengo ni kuwathibitishia wanamoshi tuko pazuri na tunaenda vizuri.

Tumebarikiwa kuwa na nchi tajiri, kinachohitajika ni kupata kiongozi atakaeweza kuutumia utajiri huu kwa manufaa ya watanzania wote. Na mimi naamini hiyo kazi inanifa kwa sababu nimeonesha katika miaka mitano iliyopita. Mimi naamini kazi hiyo inawafaa wabunge wa CCM, madiwani wa CCM kwa sababu tumeiandaa vizuri katika ilani ya uchaguzi.

Lengo kubwa la kushusha bei ya umeme, tunataka tuwe na viwanda vingi. Tunataka viwanda vilivyolala tuvifufue vyote na kwa hapa Kilimanjaro, Moshi tumeanza, palikuwa na kiwanda cha ngozi nafikiri Karanga kilichokuwa chini ya Magereza.

Leo ukienda kwenye kiwanda hicho utafikiri umefika Ulaya, kitakuwa kinatengeneza pea ya viatu kwa mwaka milioni 1.2, bado hujaweka mikufu, mtaitaje ile? Mikoba, unajua sijamnunulia mke wangu mkoba tangu nimuoe kwa hiyo msishangae nikisahau, kwa hiyo mikoba, mikanda na vitu vingine vitaanza kutengenezwa hapa.

===============


Naona Kilimanjaro inamfanya kitu mbaya "Anti" kwisha kazi
 
Ila moshi Kuna watoto wazuri bwana...pisi kali kinoma nawaona kwa Tv
Ni pesa yako tu na usiwe umezubaa huna maendeleo utawapata kibao.Huwa hawataki mtu asiye na maendeleo na ambaye hajui kutafuta pesa
 
UKIANGALIA HUKU MOSHI MJINI KWA SIKU YA LEO KILA MTU ANAENDELEA NA SHUGHULI ZAKE NI TOFAUTI NA SIKU ALIOKUJA TUNDU LISU, YANI SHUGHULI ZILISIMAMA KWA MUDA NA BODABODA ZOTE NA BAJAJI ZILIKUA NA BENDERA ZA CHADEMA TENA KWA MAPENZI YAO,
ILA LEO HAPA MJINI SIJAONA SHAMRA SHAMRA KAMA ZILE ZA TUNDU LISU.
Bahati mbaya unajidanya wewe mwenyewe, siyo mbaya

Yote Kwa yote, tukutane hapa baada ya uchaguzi, JPM mpaka huu muda tayari keshashinda zaidi ya 76%
 
UKIANGALIA HUKU MOSHI MJINI KWA SIKU YA LEO KILA MTU ANAENDELEA NA SHUGHULI ZAKE NI TOFAUTI NA SIKU ALIOKUJA TUNDU LISU, YANI SHUGHULI ZILISIMAMA KWA MUDA NA BODABODA ZOTE NA BAJAJI ZILIKUA NA BENDERA ZA CHADEMA TENA KWA MAPENZI YAO,
ILA LEO HAPA MJINI SIJAONA SHAMRA SHAMRA KAMA ZILE ZA TUNDU LISU.
Kwa hiyo unataka kusema Nini..maana inaelekea unateseka Sana..
 
Back
Top Bottom