n00b
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 1,006
- 2,667
Picha mbalimbali zikionesha mapokezi ya viongozi wa BAVICHA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, John Heche, siku walipowasili mjini Morogoro kwa ajili ya mafunzo ya uongozi kwa Kamati ya Utendaji ya Baraza hilo, ambayo yatafuatiwa na kikao cha kikatiba, kitakachofanyika Jumatatu, Septemba 17, 2012. Polisi walikuwepo tangu mwanzo wa mapokezi hayo yaliyoanzia nje ya mji kidogo, eneo la Nanenane, hadi Ofisi za CHADEMA Mkoa wa Morogoro. Ingawa baadhi ya waendesha pikipiki waliojumuika katika mapokezi hayo walilalamika kwa vyombo vya habari kuwa askari waliokuwa kwenye gari la chama walikuwa wanachukua namba za pikipiki zao. Haikujulikana kwa sababu gani (kubambikiwa kesi?).
Maandamano hayo ya kimya kimya ya pikipiki na magari, yakipita katikati kabisa ya mji, yawasisimua wananchi wa Morogoro ambao walitokezea barabarani kuona chama chao kina shughuli gani mjini kwa siku hiyo, wengi wakiulizia 'mkutano wapi leo'.