Morogoro: Mapokezi ya aina yake ya viongozi wa BAVICHA

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Picha mbalimbali zikionesha mapokezi ya viongozi wa BAVICHA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, John Heche, siku walipowasili mjini Morogoro kwa ajili ya mafunzo ya uongozi kwa Kamati ya Utendaji ya Baraza hilo, ambayo yatafuatiwa na kikao cha kikatiba, kitakachofanyika Jumatatu, Septemba 17, 2012. Polisi walikuwepo tangu mwanzo wa mapokezi hayo yaliyoanzia nje ya mji kidogo, eneo la Nanenane, hadi Ofisi za CHADEMA Mkoa wa Morogoro. Ingawa baadhi ya waendesha pikipiki waliojumuika katika mapokezi hayo walilalamika kwa vyombo vya habari kuwa askari waliokuwa kwenye gari la chama walikuwa wanachukua namba za pikipiki zao. Haikujulikana kwa sababu gani (kubambikiwa kesi?).

Maandamano hayo ya kimya kimya ya pikipiki na magari, yakipita katikati kabisa ya mji, yawasisimua wananchi wa Morogoro ambao walitokezea barabarani kuona chama chao kina shughuli gani mjini kwa siku hiyo, wengi wakiulizia 'mkutano wapi leo'.

1.jpg

2.jpg

3.jpg

4.jpg

5.jpg

6.jpg

7.jpg
 
dahaa kweli wakati ni hakimu mzuri sana, muda wa mabadiliko ukifika umefika tu.. hata uzuie vipi! ASANTE MUNGU.
 
Unaeweza kuona hapo, watu ni watulivu yaani full amani... Hakuna hata sisismizi aliyekufa... Sasa polisi wangesikiliza tu maagizo ya shemejiyake na jk (said mwema) tayari mtu angekuwa ameshamwangwa utumbo na firigisi..... Kwa hiyo somo liko wazi, chadema hawana vurugu kabisa, tatizo ni nyinyiemu kutoa maagizo ya kishetani kwa polisi kuua
 
Kumbe polisi nao walikuwepo !!
Ila safari hii hakuna maafa yoyote yale.
Hii ni ushahidi tosha kabisa kuwa Chadema ni watu wa amani saaana, Wahalifu ni polisi !!Big-up Chadema, Big-up Watanzania wote wapenda mabadiliko, maana hakuna kunyamazishwa hata kwa vitisho vya polisi.
 
Nilishasema na nitaendelea kusema polisi always ndio source ya vurugu!
 
kweli risasi siyo dawa, na Watanzania hawaogopi risasi tena.
nilidhani baada ya polisi kuuwa mtu maandamano yaliyopita, leo watu wasingejitokeza.

Kila mara tumekumbushwa na historia kwamba risasi za moto na mabomu ama vifaru havijawahi kushinda nguvu ya umma.
Ni wiki mbili tu tangu policcm wamuue kijana muuza magazeti hapo morogoro lakini bado tu pamoja na kuwa na kumbukumbu ya tukio hilo la kinyama bado wananchi wamejitokeza kwa wingi kuwapokea vijana wa Chadema.

Hiyo ni salamu tosha kwa policcm kwamba huko tunakoelekea wanalazimika kubadilisha strategy yao ya kutumika kwa maslahi ya ccm kwani sasa wananchi hawatishiki wala kuogopa risasi na mabomu yao.
 
dahaa kweli wakati ni hakimu mzuri sana, muda wa mabadiliko ukifika umefika tu.. hata uzuie vipi! ASANTE MUNGU.
Magamba sasa hawana ujanja, polisi wao wameua wee, wakawa wanasingizia kuwa mauaji hayo yanasababishwa na viongozi wa Chadema, lakini penye ukweli, uongo hujitenga, shughuli yoyote ya CDM, isiyoingiliwa na vyombo vya dola, kama vule, UWT na Polisi, shughuli huisha kwa amani kubwa, kama unavyoona hapo Moro, sasa ni dhahiri siku za magamba kuwa madarakani, zinaanza kuheshibika! ni kweli, tunapaswa kumshukuru Mungu, na kama inavyojieleza slogan ya CDM,wao wana vyombo vya dola, CDM tunaye Mungu wetu, anayetuongoza kwenye haya mapambano!
 
kweli risasi siyo dawa, na Watanzania hawaogopi risasi tena.


nilidhani baada ya polisi kuuwa mtu maandamano yaliyopita, leo watu wasingejitokeza.
Nani kakuambia? mabadiliko ni kama nature uwezi kuyazuia! CCM watake wasitake oneday lazima wang'oke madarakani
 
Yaani CDM ni chama kubwa, kijana mdogo tu kama Heche, Moro imetaharuki! Nimeona kwenye TV sikuamini, je angeshuka Kamanda wa Anga au Kamanda wa Kikosi cha Ardhi ingekuwaje?

Ndio maana CCM, na CUF wanataharuki. Polisi adabu mliyoionyesha leo endeleeni nayo, waacheni CCM wajitetee wenyewe.
 
mi nilikuwepo,lakini nilishaacha utumbo wangu nyumban kwa usalama zaid,ALUTA CONTINUA!!!!!
 
picha mbalimbali zikionesha mapokezi ya viongozi wa bavicha wakiongozwa na mwenyekiti wa taifa, john heche, siku walipowasili mjini morogoro kwa ajili ya mafunzo ya uongozi kwa kamati ya utendaji ya baraza hilo, ambayo yatafuatiwa na kikao cha kikatiba, kitakachofanyika jumatatu, septemba 17, 2012. Polisi walikuwepo tangu mwanzo wa mapokezi hayo yaliyoanzia nje ya mji kidogo, eneo la nanenane, hadi ofisi za chadema mkoa wa morogoro. Ingawa baadhi ya waendesha pikipiki waliojumuika katika mapokezi hayo walilalamika kwa vyombo vya habari kuwa askari waliokuwa kwenye gari la chama walikuwa wanachukua namba za pikipiki zao. Haikujulikana kwa sababu gani (kubambikiwa kesi?).

Maandamano hayo ya kimya kimya ya pikipiki na magari, yakipita katikati kabisa ya mji, yawasisimua wananchi wa morogoro ambao walitokezea barabarani kuona chama chao kina shughuli gani mjini kwa siku hiyo, wengi wakiulizia 'mkutano wapi leo'.

View attachment 65218

View attachment 65219

View attachment 65220

View attachment 65221

View attachment 65222

View attachment 65223

View attachment 65224


taifa mbelee....mabadiliko mbelee....Bavicha Mhimili wa Mabadiliko....'wezi na mafisadi nyumaaaaaa!

Yes we can!
 
Back
Top Bottom