Morogoro Day Trip: Kwa Wakazi wa Dar & Pwani

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
19,095
49,894
Salam wakuu.

Hii special kwa wakazi wa Dar na Pwani.

Najua mnakuaga busy sana, sana na kuna muda mnakosa ata muda wa kupumzisha akili na mwili, sababu ya muda na kipato kwa wengine.

Kuna hii Hiking Day trip ya kwenda Morogoro na kurudi, unaweza have some fun na uka relax sana mwili na akili.

Maandazi.
Kwakua muda mwingi itakua ni kupanda milima, vaa tu nguo utakazo kua comfortable mfano raba, Tshirt, buti. Mfano my outfit ilikua hivi:

PXL_20231119_071239192.jpg


ila kama utakua na earpods kama unapenda podcast & music, na mfuko wa rambo kwaajili ya kuweka cm incase mvua ikikuchapa. Vingine labda maji au kopo la maji na hela ya emergency ata buku 5.

Mwanzo.
Unatoka Dar au Pwani na kwenda Moro kwa Bus, na ukifika Moro Msamvu unachukua bajaji hadi town then boda hadi kwa Mkuu wa Mkoa hapo ndio hiking itapoanzia.

Kama utakua na private car, unaweza enda hadi pale kwa mkuu wa mkoa kuna walinzi wanaweza kukuangalizia gari hadi utakaposhuka.

Safari
Utaanza mdogo mdogo kupanda milima ya Uluguru utapishana na vijiji mbalimbali ambapo utaona na kujifunza shughuli mbalimbali wanazofanya sana sana za kilimo.

PXL_20231119_113658836.jpg


Vitu utakavyofanya.
1. Kwanza hiking.
PXL_20231119_082108736.PORTRAIT.jpg


2. Pili, Forest walking.
PXL_20231119_093425363.jpg


3. Tatu, utaona water falls mbalimbali maarufu zaidi ikiwa Choma waterfalls ila sikwenda kwasababu ya usalama kipindi cha mvua. Hii ni ndogo.
PXL_20231119_093647855.jpg


4. Nne, kama utataka camping kuna mahala Wanafanya camping unaweza lala msituni lakini tuassume hii ni day trip kwahiyo hii hatutaidiscuss sana.
PXL_20231119_110107921.jpg


5, Tano utakaa mbali na makelele ya mji.
PXL_20231119_071657602.jpg


6, Sita, utakutana na wakazi wa uko wengi ni wakulima na wako friendly sana.
PXL_20231119_114636377.jpg

Mfano wa mashamba zaidi:
PXL_20231119_113037279.jpg

7. Saba, unaweza kuogelea. Maji ya baridi sana.

8. Nane, utajifunza jinsi wanavyo sambaza maji (kama DAWASA) ila kwa gravity. Aisee.

9, Tisa uta enjoy sana kama mtu wa nature.

PXL_20231119_112255007.jpg

PXL_20231119_120259580.jpg

Gharama.
Safari ya Dar to Moro ni Elfu 10 kwenda na 10 kurudi jumla 20.

Bodaboda na bajaji kutoka Msamvu to Town haizidi elfu 5 jumla.

Kula na snacks itategemea na tumbo lako tuassume elfu 10.

Jumla kuu 35 elfu.

Muda:
Ukifika kwa mkuu wa Mkoa saa 4 Tegemea kuspend kama masaa 6-8 kuanzia kupanda hadi kushuka. Kutegemea speed yako na jinsi utakavopenda kuzunguka.

Vitu vya kunote:
Chukua kopo la maji, yakiisha utayakuta uko juu ya mtoni.
Mkiwa wawili poa zaidi kupeana company ila ata solo unaweza.
Mtandao sio wa kuutegemea sana.
Msimu wa mvua hautabiriki dakika yoyote inamwagika.

PXL_20231119_091726509.PORTRAIT.jpg

PXL_20231119_120910833.jpg

Njia zinateleza sana, kuanguka muda wowote.
PXL_20231119_131242110.jpg

PXL_20231119_093008626.jpg

Hitimisho.
Hiking na nature sio ya kila mtu ila siku ukitaka kujaribu, jaribu.

Wakazi wa Moro wanaweza ongezea baadhi ya vitu nilivyosahau.

Pamoja.
 
Safi kabisaaa...!

Napenda hiking na niliwahi kupanda M.uluguru 3 years nyuma huko ila si kwa mkuu wa mkoa,ni kupitia chuo cha ualimu-bigwa/old Dsm road

Lengo letu lilikuwa kufika kwenye namba ya kirumi juu ya mlima iliyowekwa kipindi cha utawala kama history unavyojieleza

Nilifanikiwa kufanya forest walking,water falls nzuri niliona

lakini safari iliishia njiani baada ya kuporonyoka kwenye jiwe na kusababisha jeraha kwenye begani hivyo waliendelea wengine ikabidi nirudi ilikuwa ni mbaya hadi kushindwa kuendelea.

Kuna usalama camping hapo?vipi accommodation?
 
Ahsante sana kwa ku-share uzoefu wako.

Je, kuna huduma ya kwanza iwapo mtu atapata tatizo huko kwenye hiking? Au kila kitu ni utawala binafsi?
Mkuu, huduma ya kwanza labda wanakijiji wa jirani wakusaidie maana iyo kitu unafanya solo.

Tunaweza ongeza kwenye mahitaji ukawa na simple First Aid Kit ingawa hatuombei ayo yatokee.

Nilianguka mahala ila ilikua issue ndogo.

PXL_20231119_093012585.jpg
 
Je nikihitaji kulala huko juu ni kiasi gani kwa kukadiria? Je kuna Kambi au sehemu maalumu ya kulala
Kulala kuna sehemu wana offer tents ni Tsh 15,000 per tent ambayo mnaweza lala hadi watu wawili.

Ila kuna cottage (kama nimeandika vema) ni 40k per night.

Ukiwa vyema unaweza fanya weekend getaway ukalala ata siku mbili.
 
Safi kabisaaa...!

Napenda hiking na niliwahi kupanda M.uluguru 3 years nyuma huko ila si kwa mkuu wa mkoa,ni kupitia chuo cha ualimu-bigwa/old Dsm road

Lengo letu lilikuwa kufika kwenye namba ya kirumi juu ya mlima iliyowekwa kipindi cha utawala kama history unavyojieleza

Nilifanikiwa kufanya forest walking,water falls nzuri niliona

lakini safari iliishia njiani baada ya kuporonyoka kwenye jiwe na kusababisha jeraha kwenye begani hivyo waliendelea wengine ikabidi nirudi ilikuwa ni mbaya hadi kushindwa kuendelea.

Kuna usalama camping hapo?vipi accommodation?
Dah safi sana na pole mzee. Natumai utarudia tena kwa taadhali zaidi.

Camping za tent zipo ila hapo itabidi ushirikishe local tour guides (itaongeza kidogo gharama), au ukaamua kukaa kwenye nyumba.

Mfano hii hapa, ambayo nilipiga cm nikaambiwa 40-50 hivi per night.
PXL_20231119_110110811.jpg
 
Hii issues imenivutia. Gharama ya chakula na nyumba za wageni kwa wale wanaotaka kulala huko huko ni bei/kiasi gani?
Chakula labda upikiwe na local au uliwacheki tour guides. Sikufanya research kubwa sana ya lodge au guest ila niliona kuna hostels za SUA sijui gharama na kuna watu wana miliki cottage mfano nilioweka post iliopita.
 
Umenikumbusha mbali. Kwakweli ni ka experience kazuuuri japo nilitaka kufika morning site ila nikakata moto njiani🤣

Mandhari, hewa saaafi, kaubaridi kwa mbali.
Ukienda msimu wa kiangazi dah kufika juu shughuli ila huu msimu fresh unafika.

Kuna watu wanapanda na bodaboda ila gharama isio na maana. Kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na kurudi boda anaweza kukuambia 15k hadi 20k wanaona we kishua mtalii kumbe mpambanaji umechoka makelele ya Kariakoo tu.
 
Back
Top Bottom