WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Wanaume ni viongozi nje na ndani ya nyumba si ndiyo?
Kiongozi anaangaliwa na waongozwa kama kioo na dira ya kila kitu.
Katika setting ya nyumbani/familia wanaume aghalabu hujichukulia kama ni kichwa na wengi wetu tunakubali hilo bila ubishi wowote na kama mamlaka basi hatuna budi kuiheshimu.
Inakuwaje nyumba nyingi na familia nyingi zimekumbwa na mitafaruku, mizozo, ukengeufu na kila aina ya ubaya? Kuna thread imeanzishwa na mwana mama mmoja hapa akikiri kuwa amefanya kinyume na matarajio kama mke. Kilichovutia katika mjadala huo ni kuona akina kaka/baba wakiwa mstari wa mbele kabisa kumpasha na kuzodoa kwa kitendo alichokifanya cha kuwa na mwanaume wa pembeni baada ya mumewe kumsaliti.Hapa inaonyesha kuwa kweli akina baba wanashika ile hatamu ya uongozi kwa kukemea maovu katika jamii.Lakini je, ni akina baba wangapi wanaonyesha kukereka na tabia hizi kwa vitendo ukiachilia mbali maneno matupu?Wangeonyesha kwa mfano nadhani familia nyingi zingesimama imara na matatizo mengi ya kijamii yangepungua sana.
Je Viongozi hawa wameshindwa wajibu wao?
Familia zingekuwa ni nchi, hawa viongozi tungewachagua na kuwarudisha tena madarakani?