Mohammed Dewji ashinda Tuzo ya Viwanda Afrika, amshukuru Rais Samia

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya Afrika ya mzalishaji bora wa bidhaa za viwandani.

Mo ambaye ni bilionea namba moja Afrika Mashariki na Kati alitangazwa mshindi jana, nchini Afrika kusini katika kilele cha tuzo za viongozi wa biashara barani Afrika (All Afrika Business Leaders Awards).

Katika ukumbi wa King's Ballroom, Sun City Jijini Johannesburg Mo alihudhuria na tuzo yake alikabidhiwa na Kiongozi wa Shirika la Maendeleo ya viwanda wa Afrika Kusini.

Katika ukurasa wao wa Twitter AABLA walimpongeza Mo na kampuni anayoiongoza ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) ambayo inafanya shughuli zake katika nchi 11 barani Afrika.

Mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mo alieleza kuwa amepokea tuzo hiyo kwa unyenyekevu mkubwa huku shukrani akizitoa kwa Rais Samia Suluhu.

“Shukrani zangu ni kwa Rais Samia Suluhu kwa kujenga mazingira rafiki na chanya yanayoruhusu maendeleo ya viwanda kitaifa,” alisema Mo.
FzVhr7AXoAEC2pw.jpeg
 
View attachment 2667355
Yaani Moo ashinde zawadi halafu shukrani ziende kwa Saa100
Kweli ccm ni kutuko cha karne hii.
Mmeshinddwa kuendeleza Bandari na kuuwauzia matapeli wenzenu mnadandia vitu msivyo viweza.
 
Back
Top Bottom