Mohamed Janabi, endelea kuelimisha

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,102
5,096
Mohamed Janabi umeitendea haki elimu yako kwa kuwaelimisha Watanzania na walimwengu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza ambayo mengi yameongezeka kutokana na mwenendo wetu wa Maisha.

Pamoja na kejeli na kawaida yetu waswahili kupuuza kila kitu mpaka kikukute alkini hujakata tamaa.Umetumia kila aina ya jukwaa kufikisha ujumbe.HONGERA SANA.

Wakati unafanya haya wataaalamu wenzio waliobobea wapo kimya huku jamii ikiumizwa na magonjwa mbalimbali na pia ikihujumiwa na wajanja wasio na huruma.

Wakati unafanya haya wataalamu wenzio wa mionzi wapo kimya huku jamii zikilipia 20-50000 kupimwa mwili wote kwa computer!

Wakati ukitenda haya wataalamu wa kinywa wapo kimya huku watu wanakatwa vimeo kila kukicha.Wazee tunapigwa na dawa za tezi dume huku madaktari bingwa wa mkojo wakiwa kimya.

Hongera Janabi na endelea bila kuchoka.
 
Ukweli lazima usemwe. Jamaa ni gwiji la udaktari. Hongera zake.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo letu huwa hatuoni ukubwa na hatari ya ugonjwa mpaka utukute, tukianza kuyasikia maumivu ndio tunakumbuka ushauri wa wataalamu waliokuwa wakiutoa.

Wataalamu wa aina ya Janabi kuwafikia ni vigumu, utatakiwa kulipa gharama za kumuona, ajabu anapojitokeza hadharani na kutoa ushauri bila gharama yoyote, kwa ujinga wetu bado tunafanya utani, tena tunafanya utani tukiwa tumetoka kulalamikia gharama za kuwaona madaktari bingwa mahospitalini.

Ujinga ni kipaji.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Wangapi leo asubuhi mmekunywa chai? Mlikunywa chai kwasababu mlikua mnaskia njaa au kwasababu ni mazoea tu lazima mnywe chai? Inabidi tubadilike ule pale tu unaposkia njaa na siyo kula hovyo bila mpangilio

Maneno Janabi akiwashauri waandishi wa habari
 
Kama afya Iko vizuri ukosefu wa finyango usikusumbue. Wengine Wana asili ya unene lakini afya mbovu, nasie wengine miili haina shukrani ila afya ipo sawa.
Acha vipimo vitoe majibu ya afya na sio muonekano Kwa macho.
Kwamba miili haina shukrani ahahahahaha
Kula kitimoto na lites Mkuu utaongeza ongeza vinyama
 
Mohamed Janabi umeitendea haki elimu yako kwa kuwaelimisha Watanzania na walimwengu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza ambayo mengi yameongezeka kutokana na mwenendo wetu wa Maisha.

Pamoja na kejeli na kawaida yetu waswahili kupuuza kila kitu mpaka kikukute alkini hujakata tamaa.Umetumia kila aina ya jukwaa kufikisha ujumbe.HONGERA SANA.

Wakati unafanya haya wataaalamu wenzio waliobobea wapo kimya huku jamii ikiumizwa na magonjwa mbalimbali na pia ikihujumiwa na wajanja wasio na huruma.

Wakati unafanya haya wataalamu wenzio wa mionzi wapo kimya huku jamii zikilipia 20-50000 kupimwa mwili wote kwa computer!

Wakati ukitenda haya wataalamu wa kinywa wapo kimya huku watu wanakatwa vimeo kila kukicha.Wazee tunapigwa na dawa za tezi dume huku madaktari bingwa wa mkojo wakiwa kimya.

Hongera Janabi na endelea bila kuchoka.
Hongera sana Dr. Janabi, ni kati ya watanzania wachache sana wanatoa mafunzo yenye mashiko mitandaoni. Naomba aongeze umaridadi wa muonekano wa "presentation " zake zitavutia zaidi.
 
Hiyo itakua kuharibu afya kiongozi. Suala ni kuwa mzima mwenye afya na sio unene au kuwa na nyama.
Shauri yako, maisha ndo hayahaya bro, kula KTM na lites angalau mbili tatu kila siku..

Utakuja kunyonyoka kama Janab mwishowe unakufa tu kama kuku hawa wasio na jinsia
 
Shauri yako, maisha ndo hayahaya bro, kula KTM na lites angalau mbili tatu kila siku..

Utakuja kunyonyoka kama Janab mwishowe unakufa tu kama kuku hawa wasio na jinsia

Siufuati sana ushauri wa Dr Bingwa lakini ukimbaumbau wangu ni asili hauna mahusiano kabisa na kufuata maelekezo ya kiafya japo najali afya yangu. Lites sinywi Kwa sababu binafsi na haihusiani na afya. Yaani hata unitumbukize kwenye pipa la korie, natoka vilevile
 
Back
Top Bottom