mjasiri na mali
JF-Expert Member
- Aug 2, 2018
- 1,178
- 2,169
Mkuu cheki pm yanguWanabodi,
Hii ni thread ya swali, nikipendekeza kwa kuuliza, maana siku hizi, ukiuliza kitu,, watu hawaonagi alama za kuuliza, wakadhani nimetoa statement.
Baada ya Mo kupatikana, baada ya juhudi kubwa sana za jeshi letu la polisi, baada ya ile ahadi ya motivation iliyopelekea hadi IGP kufanya press conference ya jana, hii imethibitisha kuwa kumbe Jeshi letu la polisi, linaweza, wala hatuhitaji wachunguzi wa nje. Jeshi letu la polisi sasa ndio linauwezo, au kama lilikuwa nao siku zote, then, likiamua, linaweza, ukijumlisha na ile ahadi ya motivation ya familia, bali limeweza kwa sababu, sasa ndio limeonyesha uwezo huo kwa kufanikisha Mo kupatikana akiwa mzima, salama uu salmini na bukheri wa Afya.
Sasa kwa vile familia tayari iliishatenga shilingi billion moja kwa atayefanikisha kupatikana kwa Mo, na waliofanikisha ni IGP Kamanda Sirro, na vijana wake, kwa ile Press Conference muhimu ya jana. Mimi Napendekeza hizo pesa apewe Kamanda Sirro na vijana wake, ili zitumike kuboresha jeshi letu la polisi nchini kwa kulijengea uwezo kuzuia matukio ya utekaji, kwa kuwa motivate, siku zote, mtu yoyote akitekwa au kushambuliwa na wasiojulikana, juhudi kama hizi za kumsaka MO, ikiwemo kuitisha press conference, zifanyike. Tena laiti kama tungelijua kabla namna ya kuwa motivate polisi wetu watimize wajibu wao, usikute hata Ben Saanane alipotoweka, tungejichanga tukatangaza dau, angepatikana,
Aliposhambuliwa Lissu, tungejichanga tukatangaza dau, wasiojulikana wale, wangepatikana, na alipopotea Azori Gwanda, sisi media tungejichanga tukatangaza dau, angepatikana, huwezi jua!, Bilioni moja jameni sii mchezo!.
Zamani tulizoea ahadi za motivation ni kwenye kutafutia kura tuu, lakini sasa, hata katika kutimiza wajibu!, tena naombeni msinielewe vibaya kwa hii hoja ya motivation, kwa the difference between Mo, Ben Saanane na Azori Gwanda ni status tuu, Mo ana motivational status iliyopelekea kuhangaikiwa kulikopelekea kupatikana.
Mungu Mkubwa, Pesa ndio kila kitu!, Mkono Mtupu Haulambwi!. Masikini Ben Saanane, masikini Azori Gwanda
Jumamosi Njema
P.