Mohamed Ali, alipowaadhibu waliokataa kumuita Mohamed Ali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Bondia wa Marekani, Mohamed Ali alipitia majanga mengi sana kabla ya kuwa bondia anayeheshimika duniani kwa rekodi yake ya kuwa bondia bora wa muda wote.

Alizaliwa Januari 17, 1942 Louisville, Kentucky, U.S na aliitwa Cassius Marcellus Clay Jr. Katika maisha yake alipata majanga mawili makubwa ambayo kwa namna au nyingine yaliathiri kazi yake ya ubondia. Moja ya changamoto aliyoipata maishani ni kupinga vita vya Marekani na Vietnman na kukataa kwenda vitani kama mwanajeshi wa Marekani ambapo aliporwa leseni yake ya ubondia kuanzia mwaka 1967 hadi mwaka 1970.

Miaka ya 1970 Cassius Clay alianza kusoma Quran, kipindi hiko Nation of Islam iliyokuwa inaongozwa na Elijah Mohamed ilikuwa juu sana, naye alijiunga nao. Kama ilivyo kwa wengine, suala la kubadili jina ilikuwa ni kawaida ili kuukataa utumwa. Si unakumbuka Malcolm Little alijiita Malcolm X, ili kukataa jina la master wake kwa kuwa hakuwa mtumwa tena. Basi Cassius alijiita Mohamed Ali.

Baadhi ya watu walikuwa hawataki kumuita jina hilo, suala lililokuwa linamkasirisha Mohamed Ali kwa kuwa hakutaka tena kuitwa kwa jina la kitumwa. Ernie Terrell mmoja kati ya mabondia wa Marekani alikuwa mmoja kati ya waliokataa kumuita Mohamed Ali kama Mohamed Ali bali Cassius Clay.

Februari 1967, Mohamed Ali alipambana na Ernie Terrell ambaye tangu kwenye Face Off alikuwa akimuita Clay badala ya Mohamed, na Mohamed alimwambia utataja jina langu ulingoni au nitakuabisha dunia nzima ijue. Mbali na Mohamed Ali kusifiwa kwa kuwa na nidhamu ulingoni, kuheshimu anayepigana naye na waamuzi, kwa mara ya kwanza pambano hilo alipigana kwa hasira, na round za mwisho alikuwa anapiga huku anamwambia Ernell ataje jina lake.

Now You know!
 
Back
Top Bottom