Elections 2010 Mo Dewji apita bila kupingwa!

Status
Not open for further replies.
aaaah! Siasa za bongo hata sina hamu nazo..

mimi kwenye jimbo langu la kawe nilihudhuria kikao kimoja cha ccm, sikuweza kuamini macho yaangu
kama unadhani wabunge wa tz ni watu waajabu, nenda wilayani utachanganyikiwa.......
 
Mkuu Macho_mdiliko si kila mtu mweupe (Mhindi) ni fisadi.... japo pia kila binadamu anaq udhaifu wake. Ukimlinganisha huyu jamaa na wenzake anajitahidi sana kuukimbia ufisadi, mengine ni matatizo yetu sisi Wazalendo kulazimisha kupewa vijizawadi na hiyo inamfanya mtu atumie akili sana hata kutoa hiyo misaada hasa kwa watendaji na wanasiasa wetu ili kuepuka mitego. Angekuwa ametumia fedha hata hao wapinzani wasingeweka pingamizi na pengine wasingeudisha hata fomu kwa ninavyoijua Singida.
Mkuu Halisi!
Uliyosema ni kweli ... ila kwangu mimi kiongozi yeyote anayetumia ujinga na umaskini wa wananchi kujipatia madaraka huku akijua hana nia thabiti ya kuwakomboa ni fisadi.... period. Mali za nchi zinakombwa kila siku sijamsikia akionyesha walau kusikitika. Yeye anasubiri Wanyaturu wapate majanga ndio ajifanye kuwatupia vifuko vya unga! Hawa ndugu zangu wa Kihindi sijaona hata mmoja anayetaka kumkomboa Mtanzania kwa nia. Ukilinganisha population yao hapa Tanzania na idadi ya wanaojitokeza kugombea uongozi sehemu mbalimbali ndio utaelewa si watu wa kukenulia meno! Tena wabaguzi wakubwa.. wanakupenda wanapoona wanaweza kukutumia tu. Najua kuna wachache ni wema lakini sio huyu Mohamed.
 
Habari nilizozipata muda mfupi uliopita zinadai Mhe. Mohammed Dewji mbunge wa Singida Mjini ameshinda kesi iliyokuwa imefunguliwa na wapinzani wake na yeye kuwashinda katika pingamizi alilowawekea hivyo kubakia pekee kwenye kinyang'anyiro cha nafasi ya ubunge kwa jimbo hilo, hIi inamaanisha njia ni nyeupe kurejea mjengoni. Habari zaidi tutapeana kadiri muda unavyosonga

Ni kweli kuwa Lau Masha,william Ngeleja na Nimrod Mkono,Prof Mwakyusa na Prof Mwandosya nao wamepita bila kupingwa na kufanya CCM hadi sasa iwe na wabunge zaidi ya 17 wa kuchaguliwa waliopita bila kupingwa?

Nihabarisheni tafadhali maana kama kweli sio jambo zuri hata kidogo kwa wana mageuzi maana hawa waliopita bila kupingwa watatumwa kwenye majimbo korofi ili kuongeza nguvu ya CCM!

Iweje basi CHADEMA isipate hata jimbo moja bila kupingwa likiwepo lile la Nzega na ZNZ kwa Masauni ambalo ni wazi ksbisa wagombea wa CCM walidanganya kwenye hati zao za viapo?

CHADEMA makao makuu wamejipanga vipi kuhakikisha majimbo kama Singida ambayo wagombea wao walienguliwa kufanya warudishwe kwenye mchakato wa uchaguzi huu?
 
Yaani inavunja moyo hasa, nimesikia na Mkono kapita huko Musoma vijijini na Prof. Anna Tibaijuka naye tayari, aaaagh!!!...come on guys, what kind of opposition parties we have?
 
Ni kweli kuwa Lau Masha,william Ngeleja na Nimrod Mkono,Prof Mwakyusa na Prof Mwandosya nao wamepita bila kupingwa na kufanya CCM hadi sasa iwe na wabunge zaidi ya 17 wa kuchaguliwa waliopita bila kupingwa?

Nihabarisheni tafadhali maana kama kweli sio jambo zuri hata kidogo kwa wana mageuzi maana hawa waliopita bila kupingwa watatumwa kwenye majimbo korofi ili kuongeza nguvu ya CCM!

Iweje basi CHADEMA isipate hata jimbo moja bila kupingwa likiwepo lile la Nzega na ZNZ kwa Masauni ambalo ni wazi ksbisa wagombea wa CCM walidanganya kwenye hati zao za viapo?

CHADEMA makao makuu wamejipanga vipi kuhakikisha majimbo kama Singida ambayo wagombea wao walienguliwa kufanya warudishwe kwenye mchakato wa uchaguzi huu?

Ni kweli Mkuu mpaka sasa ni Wabunge 18 wa CCM ndio hawana wapinzani katika Majimbo yao,Wabunge hao ni.
1;Anne Makinda (Njombe kusini)
2;William Lukuvi (Ismani)
3;Celina Kombani (Ulanga Mashariki)
4;Mizengo Pinda (Mpanda Mashariki)
5;Christopher Ole Sendeka (Simanjiro)
6;William Ngereja (Sengerema)
7;January Makamba (Bumbuli)
8;Deo Filikunjombe (Ludewa)
9;Job Ndugai (Kongwa)
10;Philip Mulugo (Songwe)
11;Gregory Teu (Mpwapwa)
13;Nimrod Mkono (Musoma Vijijini)
14;Lau Masha (Nyamagana)
15;Mohammed Dewji (Singida Mjini)
16;Prof.Anna Tibaijuka (Muleba)
17;Prof.David Mwakyusa (Rungwe Magharibi))
18;Prof. Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki)

Chadema Wamesimamisha Wabunge katika Majimbo 167 kati ya majimbo 239.
 
Ni kweli Mkuu mpaka sasa ni Wabunge 18 wa CCM ndio hawana wapinzani katika Majimbo yao,Wabunge hao ni.
Chadema Wamesimamisha Wabunge katika Majimbo 167 kati ya majimbo 239.

chadema haina wagombea kwenye majimbo 72! kisha tunadhani Dr.Slaa atashinda kitu cha uraisi?

ccm hawatashinda kwa ushindi wa tsunami, lakini kwa taarifa hizi zinazoibuka, inaonyesha ccm itashinda kirahisi hivi.
 
Duh kaongezeka mwingine wa Bahi huko Dodoma... Kwa mtaji huu mbona chama cha Ma**mbazi... Kinatashinda majimbo kiulaini mengi...
 
Ni kweli Mkuu mpaka sasa ni Wabunge 18 wa CCM ndio hawana wapinzani katika Majimbo yao,Wabunge hao ni.
1;Anne Makinda (Njombe kusini)
2;William Lukuvi (Ismani)
3;Celina Kombani (Ulanga Mashariki)
4;Mizengo Pinda (Mpanda Mashariki)
5;Christopher Ole Sendeka (Simanjiro)
6;William Ngereja (Sengerema)
7;January Makamba (Bumbuli)
8;Deo Filikunjombe (Ludewa)
9;Job Ndugai (Kongwa)
10;Philip Mulugo (Songwe)
11;Gregory Teu (Mpwapwa)
13;Nimrod Mkono (Musoma Vijijini)
14;Lau Masha (Nyamagana)
15;Mohammed Dewji (Singida Mjini)
16;Prof.Anna Tibaijuka (Muleba)
17;Prof.David Mwakyusa (Rungwe Magharibi))
18;Prof. Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki)

Chadema Wamesimamisha Wabunge katika Majimbo 167 kati ya majimbo 239.

Kwa kasi hii ikifika tarehe ya uchaguzi Chadema watakuwa wamepoteza nusu ya viti
vya Wabunge na Madiwani. Sasa suala la kujiuliza walikuwa makini katika uteuzi?
au waliteua wababaishaji na waganga njaa?.
 
Huu mkakati wa kuwapokea waliokataliwa CCM hauwasaidii sana Chadema sana sana itachangia kuwaagusha; na wengi wao wamekimbilia kule kama "CHEAP ALTERNATIVE" ingawa upinzani halikuwa chaguo lao la kwanza.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom