MNYIKA: Spika aunde kamati ya gesi

Atakapopatikana Mzalendo wa Ukweli aipendaye ARDHI hii ya TANGANYIKA,ndie atakayetunasua kwenye Masuala ya Mikataba MIBOVU na KUTUFANYA HURU; na KUENDELEA... Na Sio POROJO za Wanasiasa Wenye NIA MBALIMBALI za KIBINAFSI...
 
Mungu tunusuru kwani waliosoma na wasiosoma lengo ni moja la kujinufaisha tu,wazalendo hiuonekana waasi wa watanganyika a.k.a wadanganyika,mmh!
 
Aah maskini Tanzania wanakugombania kama mpira wa kona! Huku wenye mali wamelala fofo!Nani awaamshe?Wakiamka!Mi si mtabiri!
 
Mnyika Ongea na Watanzania...Achana na Spika, nunua airtime ITV tupe mipango mbadala then sisi tutafanya the needful...si muda wa kulalama kaka..tukiwaachia hawa magamba tutakuja vuna mabua...
 
Hivi kwa nini hizo sera zisiwekwe wazi Bungeni mpaka hao mawaziri wachache ndiyo wahusike kuzitunga??
Huu ni Uhuni na ubakaji wa mali za umma kwa kuwekewa sera, sheria na watu fulani tu ambao wote wanaangalia maslahi ya utawala wao badala ya utaifa kwanza.
Tujikumbushe nani waliingia mikataba mibovu na makampuni ya madini hapa Tanzania?
 
Mtwara mafuta yanachimbwa, lakini wachimbaji hawatangazi kuwa mafuta yamepatikana. Nchi hii inakufa kwa kutokuwa na udhibiti mahsusi (control)
 
mie nikisoma habar za hayo madin mafuta gesi n.k hazinipi hamasa kwani nafahamu wengi wapo kimaslah zaid wanatokwa povu weeh mwisho wa siku wananunuliwa kama wengine!
 

Kwa kipindi cha muda wa miezi kadhaa sasa kumekuwepo na sakata la mjadala mkali juu ya sheria mpya inayohusiana na umri wa kujitoa (kuchukua mafao yako) katika mifuko hii ya Kijamii hapa Nchini mara baada ya mtu kukatisha ajira yake. Sheria hii mpya iliwasilishwa na na Shirika baba la mifuko hii SSRA katika kikao cha tisa cha Bunge letu tukufu lililokaa mwezi wa nne mwaka huu kwa minajili ya kufanyia marekebisho mbalimbali , na kubwa ya hayo ikiwa ni umri kikomo cha mstaafu kuruhusiwa kuchukua mafao yake mara baada ya kuacha kazi, kusitisha mkataba na au kustaafu kazi kwa wale wenye ajira za kudumu (Japokuwa sina hakika kama kuna ajira ya kudumu!).

Kwa mjibu wa maelezo ya awali kutoka kwa wabunge wetu, inasemekana kuwa wakati wa kuwasilishwa kwa ombi la marekebisho hayo, katika jedwali lake haikuelezwa bayana ni nini hasa ambacho wanataka kukifanyia marekebisho (bali waliomba kibali kwa mjibu wa sheria na kanuni za bunge za mashirika ya umma!). Kwa kibali hicho, sasa sheria ilifanyiwa marekebisho haraka haraka na kuwasilishwa kwa mheshimiwa Rais ambaye naye kama kawaida alikurupuka na kuibariki kisha kuirejesha kwa (waheshimiwa?!!) wabunge waweze kuipitisha na kuanza kutumika kama sheria mpya kwa wanachama wote wa mifuko hiyo, ambayo hata hivyo walengwa waliipokea kwa kuizomea kwa nguvu kubwa.

Aibu yao hiyo!!
Ipo haja ya kujiuliza swali moja la msingi! je, Ilikuwaje Rais awe mwepesi wa kuwekea saini sheria hiyo kandamizi haraka haraka hata bila ya kujiridhisha mwenyewe kwanza na au kuirudisha kwa waheshimiwa wabunge ili wadadavue vizuri kabla ya kuja kumpaka matope?? au ndio tuendelee kuamini kuwa yeye ni mzee wa kupokea taarifa za mdomo zaidi kuliko kujisomea mwenyewe kama alivyokuwa Mwalimu?
Au tuseme kuwa yaelekea rais alikuwa akijua ni nini kilichokuwa nyuma ya pazia. Aidha kwa manufaa ya wanachama wa mifuko au kwa manufaa ya baadhi ya wateule! Tafakari.

Sasa sakata limekuja mara baada ya sheria hiyo kuanikwa hadharani kwa washika dau wenyewe ambao ndio wachangiaji. Kwangu mimi naweza kusema kuwa sheria hii imeletwa na SSRA, lakini ukienda kwa undani zaidi utagundua kuwa sheria hii imetengenezwa na mifuko yenyewe kisha wakamtumia baba yao SSRA kama msemaji wao!. Kwa nini nasema hivyo? Ndiyo! Ni hivyo kwa kuwa mifuko hii imekuwepo kwa miaka mingi sasa na mifumo yake ya uendeshaji wa mifuko hii imekuwa hivyo tangu kuundwa kwake.

Sasa kinachoonekana kwa sasa ni kuwa baada ya mifuko hii kutumika kibiashara na kisiasa zaidi, imepiga darubini na kugundua kuwa huko tuendako inawezekana ikakosa pesa za kulipa mafao ya wanachama wake. hilo ni angalizo langu!.
Moja ya sababu kubwa ni kuwa, ikumbukwe kuwa mifuko hii imejiingiza kwenye biashara kubwa (hata bila kuwashirikisha wanachama) kana kwamba mifuko hii ni ya viongozi pekee waliowekwa pale kuisimamia. Kitendo cha kujenga majengo makubwa ya kifahari na mikataba ya ujenzi wa daraja la Kigamboni ni matumizi mengine ambayo wanachama wanastahili kuyahoji!

Leo hii kama mifuko hiyo ingeamua kujenga nyumba za gharama nafuu kwa wanachama wote ambao wamechangia mifuko hiyo kwa kipindi fulani kisha kuutangazia umma kuwa mifuko itasitisha kutoa mafao hayo hadi mtu anapofikisha umri huo, hakika ingekuwa na tija! Na hakuna mtu ambaye angeweza kukataa sheria hiyo isiwepo kwa kuwa hata sababu za msingi zingekuwa wazi.

Lakini unapomwambia kuwa mafao yake atayachukua baada ya kufikisha miaka 55 – 60 wakati bado anaishi katika nyumba ya kupanga, hilo haliingii akilini ukizingatia kuwa hata umri wa sasa wa kuishi kwa mtanzania wa leo kuifikia ni nadla sana.

Ni mifuko hii ambayo imekuwa ikilalamikiwa kusaidia chama tawala katika masuala mbalimbali ya kisiasa hasa nyakati za uchaguzi kama zilivyovuma habari za chini ya zuria kuwa bwana Mkuro wakati akiwa mkurugenzi wa NSSF aliivutia CCM billion nne ili ziwasaidie wakati wa kampeni za mwaka 2010 na hicho ndicho kilichopelekea yeye kupewa zawadi ya uwaziri wa fedha mara baada ya uchaguzi.

Haya na mambo mengine ndiyo ambayo yamekuwa yakipelekea wanachama wengi kupatwa na ghadhabu ya kutaka pindi muda wa ajira yake inapokoma, basi na yeye aondoke na chake. (Pia inasemekana kuwa Mkuro huyo huyo ndiye anayemiliki kampuni ya mabasi ya BM Coach) wenye taarifa kamili watujuze.

Kwa kuwa jambo hili nimeonelea nilipitishe kwa wanajamii wenzangu kupitia mtandao wetu huu wa kijamii, naamini kuwa nanyi mtachangia mawazo yenu kwa manufaa ya watanzania wote. Lakini naomba nihitimishe kwa kutoa ushauri kwa mashirika haya kwa kuyashauri kuwa, kwa kuwa wafanyakazi wengi ambao ndiyo wanachama wa mifuko hii ni masikini sana, ingefaa yafanye haya yafuatayo;

Waorodheshe idadi ya wanachama wao wote ili wale ambao maisha yao yapo chini wawajengee nyumba za bei nafuu ili hata kama wakistaafu kusubiri hiyo miaka 55 au 60 ifike, basi wawe na sehemu ya uhakika ya kulaza mbavu zao zilizochoka.

Mifuko hii iwasilishe sheria ya kutoa mikopo kwa wanachama wake ambapo michango yao ya kila mwezi inabaki kama dhamana ya mikopo hiyo ili pamoja na kufanya kazi lakini wawe na njia nyingine ya kujiongezea kipato, kuliko vile ilivyo sasa ambapo masikini wanaochangia mifuko hiyo hawaifaidi badala yake wanakopeshwa watu kama akina Manji.
Naomba kuwasilisha.
Miwatamu.
 
Gesi na mafuta yagunduliwe kwingine, watu tayari wanataka waunde kamati za kula fedha za umma badala ya kuwakwamua wananchi wanaovizunguka visima hivyo!
 
Back
Top Bottom