Mnyika: Polisi hushughulika na Jinai siyo lugha za Staha ambalo ni suala la Kijamii ambalo ni Madai!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,994
Katibu mkuu wa Chadema John Mnyika amesema kwa uelewa wake Jeshi la polisi hushughulika na Jinai siyo Lugha za Staha ambalo Kimsingi ni swala la Kijamii ambalo hushughulikiwa kimadai

Mnyika amesema Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu yuko nje ya Nchi na hawezi kuripoti kwa DCI Kesho kama barua ilivyomtaka na ameshaahidi kuripoti pindi atakaporejea nyumbani.
---

Siku moja mara baada ya barua ya wito kusambaa mitandaoni ikimtaka makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) Mh. Tundu Lissu kufika ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai Dar es salam kwa ajili ya mahojiano.

Katibu mkuu wa chama hicho Mnyika amekosoa kitendo hicho huku akilitaka jeshi la polisi kutoka hadharani na kuueleza Uma kama lina haki ya kushughulika na makosa ya lugha za staha.

Akizungumza na Watetezi tv Mnyika amesema anachokijua ni kuwa kila kitu kina utaratibu wake na kuwa jeshi hilo halina haki hiyo.“Tumeisoma hiyo barua ya wito,wanazungumza kwamba anaitwa kwa sababu ya kutoa lugha isiyokuwa na staha,sasa polisi hawashughuliki na lugha isiyokuwa na staha.

suala la kuwa na staha au kutokuwa na staha inategemea anayetafsiri staha ni kitu gani, lakini polisi na mahakama kazi yao ni kutafsiri mambo ambayo ni ya kijinai” Amesema Mnyika.

Source: Watetezi Tv

Mlale Unono 😃
 
Kila mtu afanye kazi yake... haya ni matokeo ya utawala mbovu... Mengi yatafuata... mtawala asiyefanya kazi zake sawa akiambiwa hufura... wengi wao wanaweka pamba masikioni ndio asili ya ule msemo wa Aambiliki.. hawa wote ni motoni akhera...
 
Back
Top Bottom