Mnyika na nguvu ya Umma wachafua hali ya hewa DAWASCO

Buyaka

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
1,643
1,786


Mbunge, wananchi wavamia Dawasco


dvam.jpg


Mkurugenzi wa Kampuni inayosambaza majisafi katika Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani, (Dawasco), Jakson Midala. akizungumza na wakazi wa Jimbo la Ubungo waliongozwa na mbunge wao John Mnyika (katikati) katika kuvamia makao makuu ya Dawasco jana. Picha na Pamela Chilongola


MWANANCHI
Pamela Chilongola

BAADHI ya wananchi wa Ubungo katika Manispaa ya Kinondoni, jana wavamia Ofisi za Kampuni inayosambaza maji katika Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani (Dawasco), kulalamikia kukosa huduma za maji. Katika tukio hilo, wananchi hao waliongozwa na mbunge wao John Mnyika na kwa mujibu wa maelezo yao, hatua hiyo ilikuja baada ya kampuni hiyo kutowapa majibu kuhusu malalamiko ya kukosa huduma .

Walisema miezi nane iliyopita, waliiandika kampuni hiyo kutaka kujuia sababu za wao kukosa huduma za maji katika maeneo yao, lakini hawakujibiwa. Mmoja wa wananchi hao Msafiri Shabani wa Mabibo, alielezea kushangazwa kwake na hatua ya wananchi katika eneo hilo kukosa maji wakati huko nyuma walikuwa wanapata huduma.

“Huko nyuma tulikuwa tunapa huduma angalau wiki mara tatu lakini kwa sasa tunapata mara moja na yanafunguliwa kwa saa mbili tu, nadhani kuna mchezo fulani unafanyika, ili tukosema maji,” alisema. Akijibu tuhuma hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Dawasco, Mhandisi Jackson Midala alikiri ofisi yake kupokea malalamiko ya wananchi hao kuhusu kukosa huduma ya maji, lakini alisema hiyo inatokana na upungufu wa maji yanayohitajika.

Alisema si kweli kwamba Dawasco inashirikiana na watu wanaodaiwa kuuza maji na hivyo wakati mwingine kukuta wakiwafungia watu mabomba ili wafanye biashara.

Kuhusu suala la mabomba maarufu ya kichina ambao ni mradi uliotekelezwa na Wachina, alisema ni kweli baadhi ya sehemu hayatoi maji, lakini wanakwenda hatu kwa hatua ili hatimaye waweze kutoa huduma za ukakika.. Hata hivyo alisema hawezi kuzungumzia tuhuma zilizotolewa na wananchi hao dhidi ya meneja wa Dawasco Boko, lakini akasema kwamba inabidi azifanyie kazi .

Kuhusu mgawo wa maji alisema hauepukiki kwani wakati mwingine wanaamua kufanya mgawo wa maji mfano Manzese siku tatu ili wengine pia wapate mwisho

---------------------------------------

Laiti Watanzania wote tungekuwa tuna uthubutu wa kukataa upuuzi, nchi hii ingekuwa mbali saaaana! Ee Mungu Mwenyezi, tunashukuru kwa kutuletea upinzani Tanzania.
 
Wameenda kufanya fujo hapo. FFU walikuwa wapi kuwadunda?
Hata awakufanya fujo yoyoye walipokelewa vizuri wakazungumza na mkurugenzi na jana walikuwa na kipindi redio one,kuhusu tatizo la maji,walijadiliana vizuri watu waliuliza maswali yakajibiwa na mkurugenzi pamoja na Mh.mnyika.
 
Mbona sijaona hali ya hewa kuchafuka. Mbunge wangu Mnyika ni muungwana alifanya mikutano ya kikata na akaomba baadhi ya watu wamsindikize ili wakasikie anachoambiwa na watu wa DAWASCO. Haikuwa maandamano wala ghasia wala vitisho. Watu wakanena na kusikilizana bila mawe wala vitisho vya kumwaga damu.
 
Maongezi kati ya midala(mkurugenzi wa maji)na mh.mnyika yalifanyika vizuri na kwa amani,sasa sijui NN swala la FFU kuwadunda wananchi linatoka wapi?Tusipende kutumia nguvu kubwa sana kwa ajili ya swala dogo tu,kwa sababu kulikuwa hakuna uvunjifu wa amani kwa hiyo kulikuwa hakuna haja ya FFU kuhusika kwa namna mmoja au nyingine.
 
Mbona sijaona hali ya hewa kuchafuka. Mbunge wangu Mnyika ni muungwana alifanya mikutano ya kikata na akaomba baadhi ya watu wamsindikize ili wakasikie anachoambiwa na watu wa DAWASCO. Haikuwa maandamano wala ghasia wala vitisho. Watu wakanena na kusikilizana bila mawe wala vitisho vya kumwaga damu.

Mleta thridi ametumia heading ambayo sio nzuri ndio maana NN anasema kwa nini FFU awakuwadunda.
 
Katika historia sijui kama kuna Mbunge wa chama tawala aliyeweza kuvamia ofisi ya serikali kupinga uzembe.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Mnyika ni shwine cos hata hapa sinza D maji yalikuwa yanatoka Kama kawa lakini saizi kuna miezi mitatu hata tone hatujaina.

Kazi Yao kutoka wakati wa hotuba ya Rais na kutoa pointing za kutafuta umaarufu huku mimi nanunua maji 500. Hi ndo kazi ya mbunge, ndio maji mgao lakini 3 months.

Mnyika fanya kazi niione hapa sinza sip kelele za katiba. Shwine
 
Back
Top Bottom