Mnyika: Mbunge anayejitangaza Bungeni yeye ni CHAWA wa Mama atawezaje Kuisimamia Serikali? Mwendazake alituweza sana 2020!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,994
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema Mwaka 2006 DP World walimrubuni Rais George Bush wa Marekani ili waweze kuendesha Bandari za USA lakini Bunge likamkatalia Bush na DP World wakatimuliwa

Mnyika amesema katika Bunge ambalo mbunge anasimama bungeni na kutamba Kuwa yeye ni CHAWA wa Mama haliwezi kutenda kama wabunge wa Marekani

Mnyika alikuwa anahutubia Wananchi Kwenye mkutano wa hadhara Manzese Jijini DSM

Mlale Unono!

=========

Akihutubia katika Mkutano wa Hadhara eneo la Manzese, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika ameshauri Wananchi kupambania Katiba Mpya itakayowapa nguvu ya kuiwajibisha Serikali kuliko kutegemea Bunge.

Amesema udhaifu wa Bunge unachangiwa na namna Wabunge walivyopatikana ikiwemo kupitishwa kwa hujuma dhidi ya Upinzani na ndio maana wanalipa fadhila na sio kusimama kwa niaba ya Wananchi.

Akigusia suala la DP World na Bandari, amesema kama Bunge lingewajibika Kikatiba, lingekataa Makubaliano hayo kama Bunge la Marekani lilivyoikatalia kuendesha Bandari zake mwaka 2006 licha ya Rais Bush kushinikiza DP World ipewe Mkataba.
 
Daah, hii kali...!

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

Nimemsikiliza Dr Slaa kuanzia mwanzo hadi Mwisho ,amezungumza vyema sana kuhusu Mkataba wa DP world na Serikali ,ningependa Zembwela ,Tivu Ake ,Baba Levo ,Mwijaku na Kitenge wamsikilize vizuri huenda wakapata kitu.

Dr Slaa amesema wanayozungumza Msigwa na Katelephone ni propaganda hazipo kwenye mkataba ,pia chawa wanavyosema ule siyo mkataba bali ni makubaliano ,makubaliano means ni Agreement wagugo maana ya agreement kwanza.

Ameongea mambo mengi sana ya msingi inabidi yawekwe wazi kwenye mkataba ,waweke wazi wataongeza ajira ngapi ,TZ itafiadika na nini kuwekwe figures ,kwenye hayo makubaliono DP world wamepewa haki ya kuchukua bandari zote za bara na sio hayo wanaysema sijui kapewa sijui gati namba ngapi na ngapi ni propaganda tu ,mwarabu kapewa kila kitu.

Mwarabu kapewa haki ya kujenga reli kutoka Bandari hadi airport na haijawekwa wazi kwamba maeneo yatakayopita reli wananchi watalipwaje inatakiwa iwekwe wazi kwenye hayo makubaliano...Kitenge,zembwela,tivuake,mwijaku na baba levo ebu kaangalieni kipindi youtube ili mpate kidogo ABCs na si kusikiliza propaganda ambazo hazipo kwenye hayo makubaliano.
 
Amesema Waandishi wa Tanzania ni wa ajabu kila kitu wanasubiri kusimuliwa badala ya wao wenyewe kuusoma Mkataba ambao umetapakaa Africa Mashariki!
 
Bunge la Magufuli limekua bunge la hovyo haijawahi kutokea.

Hayati atuombe msamaha Watanzania.
Tushasema km unamuhitaji mfate pale alipolala uongee nae.
Yeye anahusika vp na mambo yanayoendelea leo?
Aisee mnakera sana
 
Amesema Waandishi wa Tanzania ni wa ajabu kila kitu wanasubiri kusimuliwa badala ya wao wenyewe kuusoma Mkataba ambao umetapakaa Africa Mashariki!
Nikweli hawasomi hivi unamuuliza mtu nyinyi kazi yenu kupinga kila kitu, baada yakumuuliza yaliyomo katika mkataba
 
Back
Top Bottom