Mnyika: Mapambano yamewezesha Faye kushinda Uchaguzi wa Rais Senegal, November 2023 nilikuwa Senegal kusaidia Harakati za Upinzani!

Toba, I smell a stinking fish...Kama alikwenda Kusaidia then anatipa taarifa Kuna a force behind this change...Pengine mabeberu Wana recruit new agents...Nimewaza tu mwenzenu kwakua vyama vyetu vina support ya Hawa ma bwana badala ya kujisimamia vyenyewe

Kama kuna sapoti ya kutoka nje kwaajili ya kuonfoa udikteta Afrika, ni jambo jema sana. Tuwashukuru sana hao wanaosapoti. Afrika inadidimia kwa sababu ya watawala hovyo, wanaojimilikisha uongozi ilihali hawana uwezo. Fikiria mijitu ambayo haitaki hata tume huru ya uchaguzi. Halafu inatumia vyombo vya dola kuwadhibiti wanaohoji. Wanaohoji hawana nguvu ya vyombo vya dola, watafanikiwa vipi kuwaondoa mashetani wanaoiangamiza Afrika kwa mifumo ya hovyo ya utawala?

Tunasaidiwa na mataifa ya nje kwenye uchumi, ni muhimu zaidi kusaidiwa katika ujenzi wa mifumo ya demokrasia na utawala bora.
 
HATA HUYO RAIS ALIYESHINDWA....Mark Sally alikuwa ni kiongozi wa Upinzani hapo awali na akashinda uchaguzi 2019 akitokea Upinzani.
Lakini alpoingia Ikulu Pakawa Patamu na kilichotokea ndio tulichoshuhudia akigeuka Kuwa Dikteta akiwafunga jela wapinzani wake hao kina Sonko&Company.

Kwa hiyo kuwa mpinzani hakugeuzi Roho kuwa ya Malaika!
Ukitaka kujua tabia ya mtu, mpatie Pesa na Madaraka!

Hata Samia alianza akiwa humble,leo hii kuna watu wamefungwa Magerezani sababu tu wamemsema Samia au kumuimba asivyotaka yeye!
Pesa za umma zimegeuka na kuwa za Samia!
 
Rais aliyetoka nayeye alikuwa mpinzani ila, ghafla akataka kuinajisi Katiba, ngoja tuone wengi waafrica wanaingia ikulu very humble ila wakionja madaraka wanageuka na kusahau movement zote
Alikuwa Waziri Mkuu serikali ya zamani baada ya kung'atuka uwaziri mkuu aligombea urais mara mbili nadhani ya tatu ndiyo akashinda.
 
Sasa Mnyika si awezeshe na hapa Tanzania???! Kwanini anaeezesesha Senegal tu??
 
Mtaendelea kufurahia na kushangilia ushindi wa wengine.
Ninyi hapa nchini kushinda; labda baada ya miaka 100 ijayo.
Watanzania wana imani kubwa na CCM.
Na kwa sasa wana imani kubwa sana na Rais Samia Suluhu Hassan. Mama yetu kipenzi cha wote.
 
Tulia ww muumini wa chama la majizi.
Mara 1000 ushindi akapewa ACT na siyo CDM. Binadamu anayepinga kila jambo (barabara anaziona na kutembelea lkn anapinga, umeme anapinga, mikopo elimu ya juu anapinga,).....

CDM siyo chama cha kupewa hati ya ushindi
 
Ukiwa bendera fuata upepo lazima uje na hoja hizi za kitoto. Unadhani hatujui cdm wanapinga nini, na kwa wakati gani? Hata hivyo wapiga kura ndio huchagua mgombea na sio kupeana. Kama nu kupewa wapeni ACT maana hao wanategemea hisani ya ccm. Cdm wana wapiga kura wa kutosha, hawategemei hisani ya yoyote.
 
Mara 1000 ushindi akapewa ACT na siyo CDM. Binadamu anayepinga kila jambo (barabara anaziona na kutembelea lkn anapinga, umeme anapinga, mikopo elimu ya juu anapinga,).....

CDM siyo chama cha kupewa hati ya ushindi
Takataka kama wewe ni wa kupuuzwa tu.
 
HATA HUYO RAIS ALIYESHINDWA....Mark Sally alikuwa ni kiongozi wa Upinzani hapo awali na akashinda uchaguzi 2019 akitokea Upinzani.
Lakini alpoingia Ikulu Pakawa Patamu na kilichotokea ndio tulichoshuhudia akigeuka Kuwa Dikteta akiwafunga jela wapinzani wake hao kina Sonko&Company.

Kwa hiyo kuwa mpinzani hakugeuzi Roho kuwa ya Malaika!
Ukitaka kujua tabia ya mtu, mpatie Pesa na Madaraka!

Hata Samia alianza akiwa humble,leo hii kuna watu wamefungwa Magerezani sababu tu wamemsema Samia au kumuimba asivyotaka yeye!
Pesa za umma zimegeuka na kuwa za Samia!
Hakuna kitu kama roho ya malaika katika uongozi wa nchi. Lazima kuwe na katiba na mfumo wa sheria unaohakikisha watu wote pamoja na viongozi wanaishi kwa kuheshimu katiba na sheria, period. Kuwa chama tawala au upinzani hizo ni nafasi tu zinazobadilika. Mpinzani akiingia madarakani anakuwa mtawala. Akitoka anakuwa mpinzani.

NI KOSA KUBWA SANA kutarajia kuwa na binadamu ambaye atakuwa kiongozi bora muda wote kwa hulka yake tu kiasi cha kumpa madaraka yote (absolute power). HAKUNA BINADAMU WA AINA HIYO. Binadamu, kwa asili, usipomuwekea udhibiti wa kisheria ataweka maslahi yake binafsi mbele muda wote. Hata kama yanaangamiza taifa.

Hata Marekani na Ulaya wanajua hilo. Ndio maana utawala wa Katiba na sheria unahesimiwa kuliko kitu chochote.

Tatizo la Afrika ni kuabudu watu na kutarajia watakuwa wema kwa utashi wao tu. Huo ni ugonjwa wa akili.
 
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema Mapambano yamewezesha mh Faye kushinda Uchaguzi wa Rais Senegal

Mnyika anasema November 2023 alikuwa Nchini Senegal kama sehemu ya Ujumbe kutaka kiongozi wa Upinzani mh Sonko na mwenzake waachiwe Huru

Mnyika ameeleza ukurasani Kwake X

Mlale Unono
---
Katika ukurasa wake wa X Mnyika anaandika yafutatyo:

Mapambano yamewezesha Bassirou #Diomaye Faye (44) kushinda uchaguzi wa urais kwenye vituo vingi #SenegalElections .

Mwezi Novemba 2023 nilikuwa #Senegal kama sehemu ya ujumbe wa kutaka Kiongozi wa Upinzani Ousmane Sonko ambaye pamoja na mwenzake Diomaye waachiwe huru na chao Chao cha #PASTEF ambacho wakati huo kimefutwa na Serikali kirejeshwe na wote wapewe haki ya kushiriki uchaguzi wa 2024.

Nilichobaini wakati huo ni kuwa yalikuwepo mapambano toka mwaka 2021 wakati Rais Macky Sally alipoonyesha mwelekeo wa kutaka kugombea muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Uamuzi huo na ugumu wa maisha kwa wananchi, ukosefu wa ajira kwa vijana, madai ya mikataba mibovu ya mafuta na gesi, matumizi ya CFA frank na ufisadi Serikali vikawa kichocheo mapambano kupitia maandamano. Uamuzi wa Rais wa Senegal kuzima maandamano hayo kwa vyombo vya dola kuua raia, kuwaweka Sonko na wenzake gerezani na kufuta Chama chao ukaamsha mapambano zaidi na kusambaza moto wa mabadiliko kwa wadau wengi zaidi ya Chama cha PASTEF.

Mwezi Februari mwaka huu Rais Wa Senegal akataka kusogeza mbele uchaguzi, hata hivyo Baraza la Katiba la nchi hiyo likamkatalia na kuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya muhula wake kuisha tarehe 2 Aprili 2024. Uamuzi huo ilitanguliwa na maandamano mengine ya umma kupinga uamuzi wa Rais na kutaka uchaguzi ufanyike sanjari na wafungwa wa kisiasa kuachiwa huru.

Rais akalazimika kufanya mambo mawili kwa haraka: kutangaza uchaguzi na kupeleka Bungeni amnesty bill.

Hapo ndio ikaendelea safari ya mapambano kwa #OusmaneSonko na #Diomaye kutoka na kujitokeza kwa umma tarehe 15 Machi 2024 kuanza kampeni na hatimaye #DiomayePresident kupigiwa kura 24 Machi 2024. Imekuwa ni mapambano na kampeni ya miaka takribani mitatu kama utaanzia 2021, ama zaidi ya hiyo kama utaanzia Sonko alipogombea mara ya kwanza 2019 au wawili hao na wenzao walipounda Chama cha PASTEF 2014 baada ya kutoka Serikalini wakiwa wakaguzi wa kodi.

Mgombea wa coalition Yao iliyoundwa baada ya PASTEF kufutwa alipaswa kuwa Sonko. Hata hivyo tofauti na mwenzake ambaye alikuwa mahabusu, Sonko alishapatikana na hatia kwenye kesi kadhaa za kisiasa na mojawapo ikasababisha aondolewe kwenye orodha ya wagombea urais. Haraka akamuunga mkono mwenzake ambaye alikuwa Katibu Mkuu wake kwenye Chama. Na Bassirou D. Faye maarufu kama Diamaye akaogelea kwenye mawimbi ya mapambano na mabadiliko yaliyofunguliwa na Sonko. Ndio maana kauli mbiu ya waSenegal katika uchaguzi huu imekuwa kwa lugha yao ya kiWolof #DiomayemMooySonko yaani Diomaye ni Sonko.

Nimeshuhudia nguvu ya pamoja ya wawili hawa sio tu katika mabango, bali katika vituo vya kupigia kura nilivyotembelea jana asubuhi mpaka wakati wa matokeo jioni. Sasa kinachusubiriwa ni Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kukamilisha mchakato wa majumuisho na kumtangaza mshindi. Mapambano yameshinda Senegali, ni vyema nchi hiyo sasa ikajifunza kwenye mapito ya Marais Wade na Sally na kizazi hiki kipya kilete mabadiliko kwenye maisha ya watu. Kwetu Tanzania tuendeleze mapambano ya kikatiba na kisheria kuwezesha chaguzi huru na haki. Tujiandae kwa #WikiYaMaandamano 22 mpaka 28 Aprili 2024.

Pia soma:
- Senagal imechagua Rais kijana kuliko nchi yoyote Africa
Sasa wao nguvu za kukaa mezani na CCM kujadili mambo yasiyowezekana kwa CCM ni nini!!
 
Kama kuna sapoti ya kutoka nje kwaajili ya kuonfoa udikteta Afrika, ni jambo jema sana. Tuwashukuru sana hao wanaosapoti. Afrika inadidimia kwa sababu ya watawala hovyo, wanaojimilikisha uongozi ilihali hawana uwezo. Fikiria mijitu ambayo haitaki hata tume huru ya uchaguzi. Halafu inatumia vyombo vya dola kuwadhibiti wanaohoji. Wanaohoji hawana nguvu ya vyombo vya dola, watafanikiwa vipi kuwaondoa mashetani wanaoiangamiza Afrika kwa mifumo ya hovyo ya utawala?

Tunasaidiwa na mataifa ya nje kwenye uchumi, ni muhimu zaidi kusaidiwa katika ujenzi wa mifumo ya demokrasia na utawala bora.
Hivi mataifa hayo yanatusaidia kwenye uchumi kumbe? Tell me!
 
Mbona mnyika na Mbowe mnaridhika na nusu mkate!!?
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema Mapambano yamewezesha mh Faye kushinda Uchaguzi wa Rais Senegal

Mnyika anasema November 2023 alikuwa Nchini Senegal kama sehemu ya Ujumbe kutaka kiongozi wa Upinzani mh Sonko na mwenzake waachiwe Huru

Mnyika ameeleza ukurasani Kwake X

Mlale Unono 😄
---
Katika ukurasa wake wa X Mnyika anaandika yafutatyo:

Mapambano yamewezesha Bassirou #Diomaye Faye (44) kushinda uchaguzi wa urais kwenye vituo vingi #SenegalElections .

Mwezi Novemba 2023 nilikuwa #Senegal kama sehemu ya ujumbe wa kutaka Kiongozi wa Upinzani Ousmane Sonko ambaye pamoja na mwenzake Diomaye waachiwe huru na chao Chao cha #PASTEF ambacho wakati huo kimefutwa na Serikali kirejeshwe na wote wapewe haki ya kushiriki uchaguzi wa 2024.

Nilichobaini wakati huo ni kuwa yalikuwepo mapambano toka mwaka 2021 wakati Rais Macky Sally alipoonyesha mwelekeo wa kutaka kugombea muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Uamuzi huo na ugumu wa maisha kwa wananchi, ukosefu wa ajira kwa vijana, madai ya mikataba mibovu ya mafuta na gesi, matumizi ya CFA frank na ufisadi Serikali vikawa kichocheo mapambano kupitia maandamano. Uamuzi wa Rais wa Senegal kuzima maandamano hayo kwa vyombo vya dola kuua raia, kuwaweka Sonko na wenzake gerezani na kufuta Chama chao ukaamsha mapambano zaidi na kusambaza moto wa mabadiliko kwa wadau wengi zaidi ya Chama cha PASTEF.

Mwezi Februari mwaka huu Rais Wa Senegal akataka kusogeza mbele uchaguzi, hata hivyo Baraza la Katiba la nchi hiyo likamkatalia na kuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya muhula wake kuisha tarehe 2 Aprili 2024. Uamuzi huo ilitanguliwa na maandamano mengine ya umma kupinga uamuzi wa Rais na kutaka uchaguzi ufanyike sanjari na wafungwa wa kisiasa kuachiwa huru.

Rais akalazimika kufanya mambo mawili kwa haraka: kutangaza uchaguzi na kupeleka Bungeni amnesty bill.

Hapo ndio ikaendelea safari ya mapambano kwa #OusmaneSonko na #Diomaye kutoka na kujitokeza kwa umma tarehe 15 Machi 2024 kuanza kampeni na hatimaye #DiomayePresident kupigiwa kura 24 Machi 2024. Imekuwa ni mapambano na kampeni ya miaka takribani mitatu kama utaanzia 2021, ama zaidi ya hiyo kama utaanzia Sonko alipogombea mara ya kwanza 2019 au wawili hao na wenzao walipounda Chama cha PASTEF 2014 baada ya kutoka Serikalini wakiwa wakaguzi wa kodi.

Mgombea wa coalition Yao iliyoundwa baada ya PASTEF kufutwa alipaswa kuwa Sonko. Hata hivyo tofauti na mwenzake ambaye alikuwa mahabusu, Sonko alishapatikana na hatia kwenye kesi kadhaa za kisiasa na mojawapo ikasababisha aondolewe kwenye orodha ya wagombea urais. Haraka akamuunga mkono mwenzake ambaye alikuwa Katibu Mkuu wake kwenye Chama. Na Bassirou D. Faye maarufu kama Diamaye akaogelea kwenye mawimbi ya mapambano na mabadiliko yaliyofunguliwa na Sonko. Ndio maana kauli mbiu ya waSenegal katika uchaguzi huu imekuwa kwa lugha yao ya kiWolof #DiomayemMooySonko yaani Diomaye ni Sonko.

Nimeshuhudia nguvu ya pamoja ya wawili hawa sio tu katika mabango, bali katika vituo vya kupigia kura nilivyotembelea jana asubuhi mpaka wakati wa matokeo jioni. Sasa kinachusubiriwa ni Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kukamilisha mchakato wa majumuisho na kumtangaza mshindi. Mapambano yameshinda Senegali, ni vyema nchi hiyo sasa ikajifunza kwenye mapito ya Marais Wade na Sally na kizazi hiki kipya kilete mabadiliko kwenye maisha ya watu. Kwetu Tanzania tuendeleze mapambano ya kikatiba na kisheria kuwezesha chaguzi huru na haki. Tujiandae kwa #WikiYaMaandamano 22 mpaka 28 Aprili 2024.

Pia soma:
- Senagal imechagua Rais kijana kuliko nchi yoyote Africa
 
Wapinzani wa Senegal siyo pinga pinga wa maendeleo ya wananchi ndiyo maana wamefanikiwa .

Mnyika rudini kwenye msitari
Sio kweli kabisa, shida ya Tanzania ni mijitu bogus kama nyie kutwa ni kuiabudu tu ccm kisa mnapata milo yenu kwa njia za haramu na kwa idhini yao. Bure kabisa.
 
Chadema ni chama kilichoamin8ka sana na watanzania kabla ya 2015 kutokana na maono yao. Ila baada ya kuanza kuyakana yake waliyoyaamini walipoteza mvuto.
 
Back
Top Bottom