Mnyika aishukia EWURA

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), ametoa siku saba kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), kutoa kauli kwa umma kuhusu bei elekezi ya maji kama inavyofanya kwenye bei ya mafuta.

Mnyika alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu ziara aliyofanya katika kata saba ya kuangalia kero ya upatikanaji wa maji katika jimbo lake na Jiji la Dar es Salaam kwa ujumla.
Alisema ni vema EWURA ikasimamia bei ya maji na biashara ya maji, kwani sasa imekuwa kama biashara haramu na kuuzwa kwa bei ya juu bila kuzingatia kipato cha mwananchi wa kawaida.

“Kutokutoa bei elekezi kwa wafanyabiashara wa maji inaweza kuwa moja ya sababu inayoshawishi watu kujiingiza katika biashara hiyo na kujipangia bei wanayotaka.
“Hali hiyo imesababisha kundi kubwa la wafanyabiashara wasio waaminifu kuingia katika biashara hiyo kwa ajili ya kujipatia faida kubwa, EWURA ambao ndio wenye dhamana wa kuandaa kanuni za kudhibiti na kutoa bei elekezi hadi sasa hawajaueleza umma wamefikia wapi,” alisema Mnyika.

Aidha, alitoa wiki moja kwa Wizara ya Maji na Kampuni ya maji ya Dar es Salaam (Dawasa) kutoa maelezo ndani ya wiki moja wamefikia wapi kushughulikia miundombinu ya Ruvu Juu, ili kupunguza kero ya maji mkoani Dar es Salaam na endapo hawatatekeleza atachukua hatua nyingine za kibunge na kuuelekeza umma cha kufanya

Source: Sheha Semtawa
 
Back
Top Bottom