Mnatuingiza kwenye nishati safi kama nchi ya dunia ya kwanza!

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
19,118
22,874
Kabla ya kuanza kutuingiza wananchi kwenye kutumia nishati safi serikali ingejikita kwanza kwenye maisha ya watumiaji na mapishi yao, pia mpango huo usingefanywa kibiashara zaidi, ungezingatia kuangalia jinsi gani baadhi ya wananchi wangeweza kupata nishati ya gesi bila kutumia fedha mfano wafugaji na wakulima, hawa wanaweza kupata gesi kutokana na mifugo yao na mabaki ya vyakula ambapo kwa sasa nao wamepewa mitungi ya gesi!
Upande wa wananchi wa mijini hawa utafiti wa kina unahitajika kuliko sheria na shuruti, wengi wa hawa hawana vipato vyovyote kiasi hata mlo mmoja kwa siku ni shida kuupata. Baadhi ya wakazi hata huo mkaa huwa ni shida kuupata kiasi wanaokoteza vijikuni na vifuu vya nazi, hawa uwezo wa kununua gesi hata kwa bei nafuu hawana.
Nihitimishe kwa kuishauri serikali ishirikiane na India kuangalia utaalamu wa kutengeneza nishati mbadala na majiko yenye ubora kuliko haya yetu, pia iagize mifuko ya kutengeneza gesi ya samadi toka Kenya.
 
Back
Top Bottom