Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,305
- 33,924
Nimeamua kuandika mada hii kutokana na utafiti wangu mdogo niliofanya kupitia hapa JF na mahala kwingine. Na bandiko hili linasimama kuitaka jamii yetu ya watanzania isimame kwenye kile inachoamini kwa kujenga juu ya kweli na siyo hisia.
Suala la Ushoga hapa JF na Tanzania linatumika kisiasa zaidi na pia katika mlengo wa vita dhidi ya Marekani na Ulaya. Kisiasa suala hili linahusishwa kiuongo uongo na CHADEMA. Na kwa Marekani inatengenezwa picha kwamba Marekani pekee ndiko kuna mashoga na Marekani wanataka kulazimisha dunia nzima wawe mashoga.
Lakini mada hii inahusu zaidi mitizamo ya watanzania kuhusu kitendo chenyewe cha kishoga. Watu wengi wanachukia sana mashoga na ushoga, lakini watu hao hao huoni wala kusikia wakitumia nguvu kubwa kusema hadharani kwamba kitendo cha kumuingilia kinyume cha maumbile mwanamke ni makosa.
Kama ushoga ni jambo baya ni kwa nini basi hatuoni harakati pia za kupiga vita wanaume kuwaingilia kinyume cha maumbile wanawake? Jee wanawake wao ni sawa tu kufanya ngono kwa mtindo huu ila tatizo ni kwa wanaume kwa wanaume? Maana kwenye mada hata humu JF utaona kuna mashabiki wengi sana wa tabia hiyo dhidi ya wanawake na hakuna mtu anayesema watu hao ni CHADEMA au ni CCM!!
Sera yetu kuhusu mwanamke kuingiliwa kinyume cha maumbile ikoje? Nimeona watu wanasema akija Haris Kamala Makamu Rais wa Marekani, aambiwe kwamba hatutaki ushoga. Jee ataambiwa pia kwamba hatutaki wanawake kuingiliwa kinyume cha maumbile?