Mnaotaka kuingia USA pitieni BAHAMAS 🇧🇸

Tatizo vijana mnajazana ujinga sana huko ughaibuni bila makaratasi siyo rahisi kutoboa utaishia kufanya kazi za chini ya meza, na hata hayo makaratasi kuyapata siyo rahisi kama mnavyodanganyana lazima usote kwanza na ukiingia kichwa kichwa deportation inakuhusu, tatizo watu wakiambiwa ukweli wanadai wanakatishwa tamaa mara sijui we mtoto wa mama hujui kitu yani ujuaji tu utafikiri wao ndio kwanza kuwa na hiyo mipango ya kufika huko
Kwahiyo wewe unataka waende vp USA zaidi ya kuzamia? Maana hawa diaspora 98% ni wazamiaji..habari ya karatasi utaijua ukiwa kiwanja
 
Beverly Hills-carfornia
images%20(77).jpg
 
Mpwayungu acha mawazo yako ya vijiwe vya kahawa hapo Chamwino, USA sio kama Chipogoro tulia uelekezwe acha ubishi,kwanza nani atakupa kazi ukiwa huna work permit hata moja?! Usione wale wanaolala barabaran wanapenda, Hupewi hata kazi ya kuzibua vyoo ukiea huna kibali hata kimoja na ukianza process za kutafuta hivyo vibali ndio zitaanza hizo kesi za ulifika vipi hapa USA, Matokeo yake ni deportation au kifungo ndani ya USA
Uoga wako ndo umasikini wako
 
Kwahiyo wewe unataka waende vp USA zaidi ya kuzamia? Maana hawa diaspora 98% ni wazamiaji..habari ya karatasi utaijua ukiwa kiwanja
Soma tena vizuri comment yangu, sijakataza watu wazamie ila wasiwadanganye wenzao kwamba ni rahisi kiasi hicho, tena ukizingatia kwa nchi yetu ambayo haina uraia pacha na passport tu kupata ni ishu
 
Ukifika USA kazi za kumwaga tu broo, usitegemee kazi ikufate apo kwa Bibi ako, ukishafika USA Kuna wakongwe wanakupa njia za kupata makaratasi
USA kama huna Social security number sahau kufanya kazi legally.

Utafanya kazi illegally chini ya maji na mshahara wako itategemea maamuzi ya aliyekupa kazi kinyume na sheria.

Na Incase ukadakwa derpotation ina kuhusu na huyo aliyekupa kazi bila kufata sheria mahakama inamhusu.
 
Unatania aisee? Yaani uzamie Marekani sababu umeshindwa kwenda legally, alafu hapohapo uende kuishi sehemu expensive duniani kama New York?

Kama alikuwa na uwezo wa kuishi New York then kwanini azamie sasa? Unajua kuna watu wanaamini hizi stori bila kufikiria alafu mwisho wa siku wanakuja kufa kizembe kama wale watanzania kule Israel.
 
Mjinga kweli ww, kama hata passport kupata kwako bado ishu kumbe we jamaa unakaa maporini
Acha kujitoa ufahamu mpuuzi wewe ni wapi nimesema kwamba hapa najiongelea mimi au kwamba mimi sina passport, wewe huoni nyuzi zinazoanzishwa karibu kila siku za kuwalalamikia uhamiaji, wanavyowazungusha watu kuwapa passports sababu ya kutaka rushwa

Wewe sikushangai huwa ni mjuaji na unabisha kila kitu hata vitu usivyoyafahamu na mbaya zaidi ukiambiwa ukweli unaishia kutukana, nakumbuka uliwahi kuleta uzi kuhusu ile green card lottery ya marekani ukawa unakomaa kwamba wanaoshinda ile lottery, serikali ya marekani inawalipia gharama zote kuanzia visa hadi safari

Wanaojua wakawa wanakuambia kwamba huo ni uongo ukishinda kila kitu unajigharamia mwenyewe ila ukawa unawabishia kama hivi, na kwa maneno uliyotumia watu wasiojua walikuamini na kuona wewe ndio unasema ukweli kumbe wewe ndio ulikuwa muongo, na mada zako nyingi huwa unaandika uongo na wajinga wenzio tu ndio wanaokusupport ila sisi tunaofahamu uhalisia tunakuona mjuaji tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom