Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,734
- 6,292
Kuna mzee mmoja ni Jaji mstaafu kwa sasa, alishawahi kutuambia kuwa ukienda Mahakamani basi mlalamikaji na mlalamikiwa wote wanona wana haki. Hata kesi za jinai ukisikiliza upande wa mtuhumiwa ni ama anaonewa au ama anaalalamika kosa limekuzwa.
Nirejee hapa, sualal la Fei kihuruma linatazama upande mmoja tu wa mchezaji lakini watu hawajui kuwa kwa klabu mchezaji ni bidhaa. Yes, ni bidhaa na klabu imeingiza gharama kubwa sana kumlea na kumpandisha thamani huku ikimtimizia matakwa yake ya kimkataba ikiwemo kumlipa mshahara na posho.
Sijasikia kama Fei ana malimbikizo ya mishahara yake kuwa hajalipwa. Hivyo watu wapo tayari Fei apewe anachokitaka na kufinya haki ya klabu iliyompandisha thamaniambayo imemlipa kama walivyokubaliana.
Hoja ni kuwa kulinda kipaji cha mchezaji. Lakini hatuangalii kuwa klabu ilikuwa na mipango na mchezaji na wakati wa usajili hawakumuuza. Sasa kuondoka ghafla bila mipango au kuipa klabu muda wa kufanya replacement ambao si haraka hivyo si jambo litakaloiumiza Klabu?
Sasa TFF yenyewe imekaa kati kwenye Mzani ikiangalia maslahi ya mchezaji lakini pia ikilinda maslahi ya mwanachama wake (Klabu) pia yasidhulumiwe. TFF pia inafahamu uhuni wa Feisal ukipelekwa kisiasa na akaachiwa huru kama anavyotaka, je, madhara yake nini huko baadaye?
Kuna wanaoibeza TFF katika hili na kuamini hawajui kitu hasa watu wakiandika vitu kibao kuonesha kuwa TFF wamekosea. Jana pia baada ya Review bado watu wamekazana kuwa wamekosea na ikisisistizwa Fei aende CAS, bila kujua kuwa TFF wana semina nyingi wana uzoefu mwingi na wana wanasheria pia nguli kwenye maswala haya ya mpira. Fei na genge lake wanaujua ukweli kwa mbali kuliko sisi wapambe.
Taswira iliyopo ni kuwa TFF wamefanya hovyo au wanafanyaga hovyo na hawaaminiki katika hizi hukumu. Nachofahamu mimi labda wengine mnisaidie ni kuwa sijawahi kusikia hukumu ya TFF imewahi kubatilishwa CAS, CAF au FIFA kwa kiwango cha kusema kuwa jamaa siyo wakweli katika hukumu zao zaidi zaidi ni kelele za 'watuhumiwa' hasa Simba na Yanga ambao ili iitwe haki imetolewa ni lazima matakwa yao yashinde.
Kabla ya kumshauri Feisal aende CAS na kulipa hizo Dollar kadhaa, mwenye kumbukumbu ya kuonesha kuwa TFF wanahukumu kiubabaishaji waniletee memory lane ya maamuzi yao mawili kubatilishwa Kimataifa ili na mimi nianze kuwatilia mashaka.