Mnakumbuka haya Mafiati, na Madereva wake walikuwa Wasomali!!!!!

Hizi gari si mchezo zimekaa kiume,nina mshua wangu mdogo alikuwa ni dereva wa kampuni ya mafuta pale Moshi mjini almaarufu kwa jina la Cassacrand miaka ya 90 to 95,tulitoka dar to moshi jmoc tukafika j3 mchana ila barabara ilikuwa ni mbovu ajabu na unafika salama hata spring haivunjiki....
 
tairi rimu zake ni mariseto,ukipata pancha lazima usimame mara 7 njian kukaza stadi,matingo walikuwa vijeba vp unamkumbuka omary pumbu yule dereva aliyekuwa anaondoka na mkasi/sprinta? alikuwa noma huyu jamaa wasomali wakimuuzi anaondoka na mkasi
 
Wewe ukishuka wengine wanaendelea na safari

wow.jpg

Hii nimeona HYDOM bana!!
 
mkuu ni gia 8 tu yaani ni 2X4 unaweka gia unainua mkasi inakuwa HI,unashusha mkasi inakuwa LO kaka nimepiga gia sana hapo dar nimeendesha sana kubeba cement wazo na kubeba I.D.O bandarini kwenda IPTL kunduchi mitambo ya umeme,upo hapo? pia kuchukua molases mtibwa au kagera sugar kwenda kiteto
 
Zikipanda kitonga utingo anatembea pembeni. Ya tairi la nyuma na gogo tayari kuzuiya kama likgoma kupanda.na ndani kuna joto utafikiria upo bekary
 
kwanza gia zake lazima uwe na nizam,zina low and uper gear!!break km treni pia kukata kona km umesimama mpaka uajili msaidizi kw vijana wa kileo maana haitumii hydoric kitu mechanical
 
Nakumbuka katika nyumba ya mzee (dingi) pale Changombe karibu na Sigara Club, alimpangisha singa singa mmoja ambaye alikua anafanya kazi kampuni moja kule kule maeneo ya Changombe viwandani ilijulikana kama MOUNT CARMEL RUBBER FACTORY,ya Muisrael mmoja. Huyu singa singa alibuni kutengeneza deflatory rubber tanks katika hizo lori za FIAT ambazo zilipeleka mafuta Zambia na baada ya kupakua mafuta, kwa kuwa yalikuwa matenki ya mpira (rubber tanks),yalikunjwa na hizo mbaula ziliweza kupakia shaba ili zibebe ipite katika bandari yetu kusafirishwa nje. Gari hizi zilikuwa imara sana.Kama tutakumbuka sisi wengine wakati huo, Zambia chini ya kiongozi wake jasiri KK, iliwekewekeana vikwazo na Afika ya Kusini kusafirisha bidhaa yeyote kupitia hiko. Ila yule mzee wa kisinga snga alikuwa na tatizo moja: Kuchafua hewa. kutokana na vyakula vyao. Jioni tumekaa (tumetoka shule) anawaelezeni habari za kazi n.k mara hewa inachafuka!
:rant:
 
Enzi hizo wale madereva wa kisomali walikuwa na tabia ya kulichezesha tela unapoanza kuwa overtake katika hiyo barabara nya TANZAM HIGHWAY kama ilivyojulikana hapo zamani.. walikuwa wanawasababishia ajali za kusudi ili wawa sachi majeruhi na maliokufa. They were very notorius for that. na hizo mbaula zao. kudadadeki! jamaa zetu wengi yaliwakuta hayo.
 
nakumbuka wakati wezi pale kizota enzi hizo wanawavizia wasomali na kupakua mizigo kwa sababu ya mwendo mdogo wasomali walimkamata jamaa mmoja wakampiga pampu ya grisi kuanzia ma.takoni,puani masikioni na mdomoni na kumtupa porini hoi hadi akafariki dunia.
wasomali walikuwa noma.
 
wow.jpg
Hivi kuna kijana wa leo anayeweza sukuma gari hiyo?
Kwanza aseme ina gea ngapi 682 ?

imagejpeg

Gari hii ina gia 12 high na 12 low.
Gearbox yake ilikuwa kiboko, a mechanical marvel iliweza kupanda mlima wowote ikiwa low gear range.
 
Pale Mbeya walikuwa na sehemu ya kupaki hayo magari kwa mapumziko ya safari pakaitwa Mafiati hilo jina linadumu mpaka leo Kijana wa leo hawezi kujua kwa nini sehemu hiyo iliitwa hivyo .

Hii ni habari ya kweli kabisa, kwa sababu nimekulia ktk kitongoji hicho na hayo 'mafiat' nimeyaona. Ni kitambo sana
 
Back
Top Bottom