Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,150
Mnada wa samaki waliokamatwa kwa wavuvi haramu wadoda
Peter Edson na Aika Mushi
KAMPUNI ya udalali ya Yono Auction Mart jana ilishindwa kuanza kazi yake ya kuuza tani 70 za samaki waliovuliwa eneo la Tanzania ndani ya Bahari ya Hindi kutokana utofauti mkubwa wa bei.
Hatua hiyo iliilazimu kampuni hiyo kuahirisha mnada huo wa wazi baada ya wafanyabiashara wengi waliofika katika mnada huo kutaka kununua samaki kwa bei ya Sh1,500 hadi 2,000 kwa kilo chini ya iliyopangwa na serikali ya Sh 7,000.
Katika vuta nikuvute huku idadi ya wachuuzi ikiwa kubwa kuliko ya wafanyabiasha wakubwa wa samaki, uongozi wa Yono uliamua kuitisha kikao cha dharula ambacho hadi mchana kilikuwa kikiendelea kutafuta ufumbuzi baina yake na wafanyabaishara wanaotaka kununua samaki hao kwa bei ya chini.
Akizungumza jana katika eneo la tukio Afisa wa Serikalini, Geofrey Nanyaro alisema suala la kuuza samaki hao kwa bei ya jumla litashindikana kwa kuwa mnunuzi atashindwa kupata kibali cha kuwauza samaki hao katika soko la nje.
Samaki hawa ni wazuri na wenye uzito mkubwa, tunaweza kuwauza kwa wafanyabaishara hawa wanaotaka kununua kwa wingi lakini wao wanataka kwa ajili ya kuwasafirisha nje, jambo ambalo ni vigumu kufanyika, kwani hawatapata vibali, alisema Nanyaro.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Royal Africa, Rabstar Muhamed Alhabase alisema pamoja na kuwa na nia ya kununua samaki wote, ameshindwa kuafikiana na kampuni ya Yono kutokana na tatizo la upatikanaji wa kibali cha kusafirisha nje ya nchi.
Mimi naweza kuwachukua samaki hawa, lakini tatizo liko serikalini, hawana vibali vya kuruhusu samaki hao kuuzwa nje ya nchi, alisema Alhabase.
Naye mfanyabishara maarufu wa samaki jijini Ahmed Kombe alisema kuwa yeye alikwua anahitaji samaki wa Sh9 milioni, lakini ilishikana kufikia muafaka kutokana na bei aliyokuwa anataka auziwe.
Hawa jamaa wanauza kilo moja kwa Sh7,000 mimi nataka tani moja kwa Sh400,000 jambo ambalo limeshindikana kupatiwa ufumbuzi, alisema Kombe.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Yono, Scholastica Kavela, alisema kuwa samki hao wanauzwa kulingana bei ambayo serikali inadhani kuwa haitaweza kuleta hasara wala faida kubwa.
Alisema kufuatia hali hiyo hawataendelea na mnada huo hadi watakapojadiliana na serikali kuhusina na hali hiyo. Hivi karibuni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli alifanikiwa kudhibiti maliasili za baharini baada ya kunasa meli iliyokuwa imebeba tani 70 za samaki waliovuliwa eneo la Tanzania ndani ya Bahari ya Hindi.