Mmoja wa wanawake wa mfano, huyu hapa.

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,780
Habari zenu, mkiwa kwenye Jumapili inayoelekea I. C.U kwa kasi sana.
Nimekua naguswa sana na wanawake wenye upevu wa kiakili na maarifa na hasa yale yanayoendana na mahusiano.
Hidaya (22 yrs) ni mwanafunzi katika chuo kimoja hapa nchini.
Kaka wa Hidaya anaishi mjini, ni muajiriwa kazi nzuri, na ameshajenga nyumba yake.
Kaka huyo anaishi na mchumba wake hapo kwake , ambapo wanataraji kuowana mda si mrefu ujao.
Hidaya ni mwanachuo , na mara baada ya chuo kufungwa alikuja kwa kaka yake.
Akiwa hapo wifi yake alimfanyia karaha, vituko, vibweka, maudhi chungu ya namna tele .
Haikutokea Hidaya aslani kuthubutu kumueleza kakaake yale afanyiwayo na wifi yake.
Alijua jaribio lolote la kumwambia kakaake linaweza kuivunja ndoa ya kakaake , na hakuhitaji yeye kua chanzo.
Alivumilia hadi mda wake wa kuondoka ukafika akarudi zake chuoni.
Ni nadra sana kuwapata wanawake wenye uvumilivu, subira na silka ya Hidaya.
Mimi nawapenda sana.
Wewe je ?
Humu Jf sijui wamo ?
Labda !
 
ni kweli kwa dunia ya leo ni wanawake wachache ambao wana tabia kama hiyo, huyo Hidaya ni wa aina yake, ni mchamungu
 
Back
Top Bottom