Mmiliki wa mabasi ya Zakaria amenidhulumu mali yangu na kutishia kuniua

.kuna mpuuzi mwingine alinitapeli cement.ni fundi.nikaenda site anayojenga.nikaanza kuangusha kuta za ndani.alitamani kulia.bosi wake akanifuata nikamwambia muulize fundi wako.kwa nini nyumba ina bomolewa wakati yeye hana ugomvi na MTU?boss akanywea.
Nimeipenda style yako
 
Ni Yule tajiri wa mabasi ya Zakaria yanayotoka Mwanza hadi Silari mpakani mwa Kenya, na kada mkubwa wa chama cha mapinduzi (ccm).

Wiki tatu zilizopita nilinunua mzigo wa viatu kutoka Kenya na nilikuwa na vibali vyote vinavyoniruhusu kufanya biashara bila Shaka yoyote.

Kwa miaka mingi nimekuwa mteja wa mabasi ya Zakaria, uteja wangu ukahitimishwa wiki tatu zilizopita baada ya Zakaria mwenyewe tajiri wa mabasi hayo kanifuata stendi ya Tarime akiwa kaongozana na mfanyakazi wake mmoja turn boy wa mabasi yake na kisha kunipora mzigo wangu wa viatu wenye thamani ya sh 2,800,000.

Akidai kuwa mzigo huo ungekaa kwenye buti la basi yake ungeiunguza hiyo gari yake.
Nilishangaa Sana, ni mara nyingi Sana nimekuwa naweka viatu kwenye buti lakini hakuna basi lililowahi kuungua.

Nilidhani ni masihara kumbe ni kweli Zakaria alikuwa amedhamiria kunipora mzigo wangu.

Niliteseka Sana kupata mtaji leo hii mtu ambaye tayari kashatajirika ananidhulumu viatu vyangu vya biashara bila aibu yoyote.

Nilimfuata kumbembeleza Zakaria anipatie mzigo wangu akaniambia kuwa Nikiendelea kumsumbua atavichoma moto viatu vyangu.

Sikuishia hapo, nilimfuata padri wa kanisa lake ili ambembeleze Zakaria anirushie mzigo wangu lakini haikuwezekana.

Nikamfuata tena rafiki yake Gachuma ili amsihi anirudishie mzigo wangu lakini pia haikuwezekana kabisa.

Nikaamua kwenda police, huko ndo nilichoka kabisa ,Police waliniambia wao hawamuwezi Zakaria, inatakiwa nirudi tu kumbembeleza, niliporudi kumbembeleza Zakaria akanionya nisijaribu tena kumfuatafuata maana atanipiga risasi.

Mali yangu mwenyewe natishiwa kuuawa bila? Au ni Kwa Sababu Zakaria ni kada Wa chama dola?
6e07f7addf3fd8e2f5e627e2f40af75b.jpg


Nimeambiwa mimi siyo wa kwanza kuporwa mali na Zakaria, ni wengi sana wameporwa ila tu Hawana pa kusemea, hadi Nimeamua kuja humu kutoa malalamiko yangu na jinsi maisha yangu yalivyo hatarini endapo tu nitaendelea kudai haki yangu, ni kwamba imeshindikana kabisa kila njia kupewa mzigo wangu na tajiri Zakaria.

Ni Kwa Sababu ya utajiri wake ndo aninyime haki yangu na kutaka Kuniua?
Nataka nimwambie Zakaria kuwa, haya ni maisha tu, asidhani atakuwa juu Siku zote, yuko wapi J4 na mabasi yake? Yuko wapi Ndugu?

Zakaria kula huo mzigo ila Mungu yupo atanilipia, jasho la mnyonge huwa haliendi bure, sikuwahi kufikiria Kama Zakaria ni mtu wa aina hii.
Pole sana, kama umemfuata Mzee Gachuma na zakaria akakomaa huna pa kwenda. Zakaria ni Dora tarime.
 
Uckate tamaa endelea kudai haki yako nenda kamuone mkuu wa wilaya ambaye ni mwekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya atakusaidia tu!
Fanya hivyo kaka ucpuuze cha mcngi uwe na maelezo na vielelezo kamili!
Unamjua Zakaria au unamsikia? Mkuu wa wilaya?! Hata RC na RPC hawafui dafu.
 
Pole sana mkubwa najua ni kweli Wambura Zakaria kakudhurum maana namfahamu vizuri na Ana Manyoka (wapambe) wengi sana pale Tarime mjini, Nimefanya kazi kwake miaka mitatu na kiburi hicho anakipata kutoka kwa CMG (MWITA GACHUMA) Huyo Zakaria kiboko yake alikua Marehemu Muruga mdogo wake Gachuma lkn mkoa mzima hakuna tena wa kumtingisha Zaka, ata mimi wakati fulani nilipanda kwenye bus la BATCO na mtungi mdogo wa gesi lkn walinieleza vizuri tu kuwa hizo gari za YUTONG kuna mizigo haziwezi kubeba maana zinaweza kulipuka,
Nikashuka nikaenda kupanda gari ingine wala sikunyang'anywa mzigo wangu,
Huyo Zakaria labda ujaribu kuwasisiliana na Mwiguru lkn ata mzee Gachuma mwenyewe hawezi kumwambia kitu.
 
kwa sisi watu wa logic ukisoma post yako vizuri ni kama kuna kitu umekificha hujakisema na inaonekana unamjua huyo zakaria vizuri zaidi na unavyotaka kutuaminisha kuwa unamjua kijuu juu.pili inaonekana unafanya bisahara ya magendo ndio maana naye anapata nguvu anajua fika huna cha kufanya
 
Huyu ameleta uongo kwa style mbaya, tz kuna matajiri wangapi na wote walishakamatwa na polisi wote wanamzidi Zakaria utajiri?? Kuna kauli huwezi kuzisikia kutoka polisi
Tembea mikoani ndo Utajua Kuna watu ni Serikali. Zacharia ni tofauti sana labda JPM mdhibiti.

Yule jamaa ana vijana ukimkosea unapelekwa lockup polisi stend wanakuweka ndani. Ikifika jioni inabidi wampigie ili wajue uandikiwe kosa gani. Akikuhurumia Atasema pumbavu zake muachie aende zake. Akiamua anaweza kusema tafuta kosa lolote na litatafutwa.

Jamaa huyu ana Nguvu sana na ana pesa nyingi sana kuliko hata hao matajiri wengi wa dar
 
stori hii si ya kweli, Polis hawawezi kusema wamemshindwa mtu, huuu ni uongo na kuaribiana sifa, husimchafue zakaria na husichafue polis
Hivi we unamjua Zakaria au unamsikia?? Kuna Matrafiki waliwahi kusimamisha gari lake akapigiwa simu akaja akawapiga piga makofi akaondoka na gari.......hili la mleta mada linaweza kuwa kweli kabisa kwa tabia za jamaa.....tena wanasema siku hizi kapunguza!
 
Muone mh. RC Mara atakusaidia au fungua file la madai mahakamani. Hawezi kukushinda wallahi....utajiri na haki ni vitu viwili todauti
 
kwa sisi watu wa logic ukisoma post yako vizuri ni kama kuna kitu umekificha hujakisema na inaonekana unamjua huyo zakaria vizuri zaidi na unavyotaka kutuaminisha kuwa unamjua kijuu juu.pili inaonekana unafanya bisahara ya magendo ndio maana naye anapata nguvu anajua fika huna cha kufanya
Nikweli mkuu Kuna kitu anaficha huyu pia. Inawezekana alitaka kupitisha mzigo bila kulipia. Yule jamaa ukimuibia elfu moja tu unalipa mamilioni. Huwa hachezewi. Lakini hii haindoi ukweli kuwa Zackaria ni anayetumia utajiri, mtandao na Nguvu zake vibaya.
 
Ilikuwa zamani co sasa mtu hawezi kunyanyaswa hvo kisa vijisenti bana kwani Zakaria kitu gan!? Nampata sana cox me mwenyewe n mtu wa Tarime
Zakaria ni hatari kama alivyodai mleta mada hata sisi aliwahi kutufanyia unyama baada ya gari lake (bus) kutugonga darajani . Aligoma hata kutoa taarifa bima ili tuhudumiwe na bima zaidi ya kutuuliza kwa nini hatukufa kwenye ajali hiyo !!!.
 
Back
Top Bottom