Mmiliki na Dereva wa gari yenye usajili T 546 DGV wachukuliwe hatua kali za Kisheria

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Habari wakuu,

Hali yangu kiafya siyo njema sana, nikiwa natoka kutibiwa kwenye mojawapo ya hospitali humu jijini Dsm nimekutana na jambo baya linalosikitisha sana.

Dereva mmoja mwenye gari iliyo na usajiri wa T 546 DGV (Mimi sio mtaalamu sana wa magari, sijaweza kugundua upesi ni gari aina gani) ametaka kusababisha msiba mkubwa kwa Taifa kwenye kona ya kwanza iliyo na mteremko wa kasi wa Barabara inayoelekea Saranga kutokea Kimara Temboni.

Dereva huyu kalewa sana, akiwa na speed kubwa kashindwa kuhimili kona iliyopo kwenye mteremko huo hivyo kuvivaa vibanda vya wanawake wajasiriamali wanaofanya kazi zao za urembo, stationery n.k

Bila gari ile kugonga nguzo mojawapo ya fremu zile na kusimama mtaroni ni dhahiri kuwa eneo hilo kwa leo lingeshuhudia mauaji makubwa yanayoweza kuepukika.

Kibaya zaidi, katika hali ile ya taharuki huku manusura wakiwa na wenge kubwa la kusalimika, dereva anaanza kumwagia watu pombe zilizobaki kwenye gari huku akiwafukuza wasitoe msaada.

Najua baadae trafiki mtafika hapo. Chukueni hatua kali dhidi ya kijana huyo mwenye tabia ya hovyo isiyoelezeka.

IMG_7425.jpeg

IMG_7424.jpeg
IMG_7427.jpeg
IMG_7428.jpeg

Picha ya Mwisho: Kijana aliyevaa suruali ya khaki na shati jeusi mikono mirefu ndiye dereva.

Uhai ukipotea haurudi. Usiendeshe gari ukiwa umelewa.
 
Habari wakuu,

Hali yangu kiafya siyo njema sana, nikiwa natoka kutibiwa kwenye mojawapo ya hospitali humu jijini Dsm nimekutana na jambo baya linalosikitisha sana.

Dereva mmoja mwenye gari iliyo na usajiri wa T 546 DGV (Mimi sio mtaalamu sana wa magari, sijaweza kugundua upesi ni gari aina gani) ametaka kusababisha msiba mkubwa kwa Taifa kwenye kona ya kwanza iliyo na mteremko wa kasi wa Barabara inayoelekea Saranga kutokea Kimara Temboni.

Dereva huyu kalewa sana, akiwa na speed kubwa kashindwa kuhumili kona iliyopo kwenye mteremko huo hivyo kuvivaa vibanda vya wanawake wajasiriamali wanaofanya kazi zao za urembo, stationery n.k

Bila gari ile kugonga nguzo mojawapo ya fremu zile na kusimama mtaroni ni dhahiri kuwa eneo hilo kwa leo lingeshuhudia mauaji makubwa yanayoweza kuepukika.

Kibaya zaidi, katika hali ile ya taharuki huku manusura wakiwa na wenge kubwa la kusalimika, dereva anaanza kumwagia watu pombe zilizobaki kwenye gari huku akiwafukuza wasitoe msaada.

Najua baadae trafiki mtafika hapo. Chukueni hatua kali dhidi ya kijana huyo mwenye tabia ya hovyo isiyoelezeka.

Uhai ukipotea haurudi. Usiendeshe gari ukiwa umelewa.

View attachment 2644467
View attachment 2644469View attachment 2644470View attachment 2644471
Picha ya Mwisho: Kijana aliyevaa suruali ya khaki na shati jeusi mikono mirefu ndiye dereva.
Kwa kuanza hii gari ni toyota cami ..
 
Habari wakuu,

Hali yangu kiafya siyo njema sana, nikiwa natoka kutibiwa kwenye mojawapo ya hospitali humu jijini Dsm nimekutana na jambo baya linalosikitisha sana.

Dereva mmoja mwenye gari iliyo na usajiri wa T 546 DGV (Mimi sio mtaalamu sana wa magari, sijaweza kugundua upesi ni gari aina gani) ametaka kusababisha msiba mkubwa kwa Taifa kwenye kona ya kwanza iliyo na mteremko wa kasi wa Barabara inayoelekea Saranga kutokea Kimara Temboni.

Dereva huyu kalewa sana, akiwa na speed kubwa kashindwa kuhimili kona iliyopo kwenye mteremko huo hivyo kuvivaa vibanda vya wanawake wajasiriamali wanaofanya kazi zao za urembo, stationery n.k

Bila gari ile kugonga nguzo mojawapo ya fremu zile na kusimama mtaroni ni dhahiri kuwa eneo hilo kwa leo lingeshuhudia mauaji makubwa yanayoweza kuepukika.

Kibaya zaidi, katika hali ile ya taharuki huku manusura wakiwa na wenge kubwa la kusalimika, dereva anaanza kumwagia watu pombe zilizobaki kwenye gari huku akiwafukuza wasitoe msaada.

Najua baadae trafiki mtafika hapo. Chukueni hatua kali dhidi ya kijana huyo mwenye tabia ya hovyo isiyoelezeka.

View attachment 2644467
View attachment 2644469View attachment 2644470View attachment 2644471
Picha ya Mwisho: Kijana aliyevaa suruali ya khaki na shati jeusi mikono mirefu ndiye dereva.

Uhai ukipotea haurudi. Usiendeshe gari ukiwa umelewa.
Hata hivyo anaonekana sio yake ..mwenye gari anajulikana tu..poleni
 
Wanasema ajali haina kinga ila kwa Tanzania/Afrika ajali nyingi huchangiwa na Uzembe.

Poleni kwa kadhia hiyo, kama pana majeruhi basi tuwaombee uponyaji wa haraka
 
Back
Top Bottom