DOKEZO Wahusika! Huyu dereva wa basi la Mwendokasi T 557 DWR ni nani kwenye hii nchi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,526
14,399
Wakuu!

Jana asubuhi nilikuwa maeneo ya Kimara Temboni Upande wa kuelekea Mbezi huwa zinapaki Bajaji pamoja na Bodaboda kwa wingi, Kwa ndani kidogo kuna round about halafu kuna Mgahawa, nilienda kujipatia kifungua kinywa. Baada ya muda mfupi lilikuja basi la Mwendokasi lenye namba T 557 DWR halina abiria hata mmoja yupo dereva tu akashuka mule kwenye basi baada ya kulipaki.

Yaani alilipaki kwenye Kona na akauziba mpaka ule Mgahawa, aliposhuka kuna Jamaa akasema huyu naye kila Siku na huwa anamfuata Mwanamke na kweli baada ya kama dk 10 hivi akaja Mwanamke wakasallimia kwa kukumbatiana na alikuwa na Kishikwambi akampa yule Mwanamke , Yeye akaenda kwenye friji akachukua Pepsi baridi na Egg Chop akawa anakula , huko kwenye kona ikaanza foleni na yule Mwanamke aliyemfuata yupo kwenye gari kakaa. Na dereva alitumia karibu dakika 25 pale kwenye Mgahawa , anazunguzunguka anapiga porojo tu na wale Wafanyakazi wa ule Mgahawa.

Maswali yangu.
1. Huyu Dereva ni nani? Mbona anafanya vitu ambavyo kama Dereva anayeendesha usafiri wa abiria hasitahili kufanya?

2. Na yule Mwanamke aliyemfuata ni nani? Maana inasemekana mara nyingi sana huwa anaenda kumfuata pale?

3. Kwanini huyu Dereva analitoa basi la Mwendokasi na kulipeleka kwenye Barabara ambayo sio njia yake ? karibu 300 mita kutoka Morogoro road njia ya kuu na njia ya mwendokasi.

4. Kuna sheria gani inayomlinda huyu Dereva maana Sheria zilizopo kazivunja kwa makusudi

5. Je huyu ndio wale Wazee wa unanijua Mi nani?

6. Au ni ndugu wa Kigogo Mkubwa Serikalini?

Naomba Wahusika mlifuatilie pale Kimara Temboni, Upande wa kuelekea Mbezi unaingia ndani kidogo kuna round about na Mgahawamjaribu kupata maelezo ya kutosha. Anachokifanya huyo dereva sio sahihi kabisa.

Nawasilisha
 
Huyo ni limbukeni fulani hivi aliyekulia kijijini mvumilieni tu
Ni limbukeni sawa lakini kwanini analitoa gari kwenye njia yake na kuliingiza kwenye njia isiyo yake? kwanza alikuwa anasababisha foleni kwa watu wengine na vyombo vyao vya usafiri.

Halafu anaenda kuchukua kumbeba Mwanamke na sio Mfanyakazi wa UDA na ni kila mara huwa anafanya hivyo kwa mujibu wa jamaa aliekuwepo pale na huwa anakerwa sana na tabia ya huyo Dereva
 
Ni limbukeni sawa lakini kwanini analitoa gari kwenye njia yake na kuliingiza kwenye njia isiyo yake? kwanza alikuwa anasababisha foleni kwa watu wengine na vyombo vyao vya usafiri. Halafu anaenda kuchukua kumbeba Mwanamke na sio Mfanyakazi wa UDA na ni kila mara huwa anafanya hivyo kwa mujibu wa jamaa aliekuwepo pale na huwa anakerwa sana na tabia ya huyo Dereva
Ulishindwa nini kumhoji haya yote mkuu au ndio wanaume wa Dar mmejaa uoga uoga tu mnakuja kulia mitandaoni.

hata picha UKAOGOPA kupiga masikini😅😅😅
 
Ni limbukeni sawa lakini kwanini analitoa gari kwenye njia yake na kuliingiza kwenye njia isiyo yake? kwanza alikuwa anasababisha foleni kwa watu wengine na vyombo vyao vya usafiri. Halafu anaenda kuchukua kumbeba Mwanamke na sio Mfanyakazi wa UDA na ni kila mara huwa anafanya hivyo kwa mujibu wa jamaa aliekuwepo pale na huwa anakerwa sana na tabia ya huyo Dereva
Ni wale malimbukeni wa unanijua Mimi nani,
 
Kuna anayefuata sheria na taratibu Tz? Hasa akiwa serikalini, tukianza na rais?

Hayo mabasi ya mwendokasi katika jamii ya mabasi ya kubeba raia, ni sawa na gari ya jwtz au polisi Kati ya magari barabarani. Hayaguswi, na ukiligusa basi wewe wa kawaida ndio mwenye kosa!

Madereba wa serikali wanaendesha hovyo, wanatanua na kupita upande usio wao, hawaguswi, si wanawaendesha wazalendo wenye nchi?
 
Mkuu, minilidhani utaleta thread kwamba umemtandika makofi dereva wa mwendo kasi baada ya kuziba barabara.

Kumbe nawewe umekuja kulala mika tu, sasa na wanawake wafanyeje.

Huo mkoa wanaume mna shida gani lakini?

Juzi niliskia mmejifungia ndani eti vitoto vimewakimbiza sijui mnaitwa wenyewe rodi panya.

Jana nimeskia mmefika 2,000 mlio kimbia nyumba zenu eti kwasababu ya ndoa.

Leo mnamuangalia mwanaume mmoja anaziba njia na wanaume zaidi ya 50 mpo mnamuangalia tu.
 
Mkuu, minilidhani utaleta thread kwamba umemtandika makofi dereva wa mwendo kasi baada ya kuziba barabara.
Kumbe nawewe umekuja kulala mika tu, sasa na wanawake wafanyeje...
Mkuu huu Mtandao unafuatiliwa na watu wengi na wakati mwingine kama huna cha kuchangia Mkuu ni bora kupita kimya.

Wakati mwingine habari zinazotumwa humu huwa zinaisadia sana Serikali kupata taarifa, Kwa sababu tumezoea majukwaa ya Sports and Entertainment basi kila muda ni utani na Masikhara tu.
 
Back
Top Bottom