Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Somalia kawa mbunge

byeyombo

JF-Expert Member
Sep 3, 2015
2,223
3,578
ilhan_omar-clintonkaine-2jpg-jpg.432061

lhan Omar, mwenye umri wa miaka 34, ameweka historia kwa kuwa mbunge wa kwanza mwenye asili ya Kisomalia nchini Marekani.

Mwanamke huyo Muislamu mwenye asili ya Somali na Marekani ndio raia wa kwanza wa Kisomali kuchaguliwa katika wadhfa mkuu kama huo nchini Marekani.

Uchaguzi wake unajiri siku chache tu baada ya rais mteule Donald Trump kushtumu wahamiaji wa Kisomali mjini Minnesota kwa kueneza maoni ya itikadi kali.

Akisherehekea ushindi wake bi Omar amesema kuwa atakuwa sauti ya waliotengwa katika bunge la jimbo hilo.

''Nadhani nimeleta sauti ya akina mama vijana wanaotafuta fursa''.

Redio ya uma katika jimbo hilo ilimnukuu akisema kuwa alitoroka nchini Somalia na familia yake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati alipokuwa na umri wa miaka minane pekee.

Waliishi nchini Kenya kama wakimbizi kwa takriban miaka minne kabla ya kuelekea Marekani na kuishi katika jimbo lenye Wasomalia wengi la Minnesota.
 
Ilhan Omar( 34 ) awa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Somalia aliyeingia Marekani kama mkimbizi kuchaguliwa kuwa mbunge nchini humo,anawakilisha Minneapolis.

Ilhan_Omar+ClintonKaine.2jpg.jpg

maxresdefault.jpg
 
_92372405_ilhan.jpg

Ilhan Omar, mwenye umri wa miaka 34, ameweka historia kwa kuwa mbunge wa kwanza mwenye asili ya Kisomalia nchini Marekani.

Mwanamke huyo Muislamu mwenye asili ya Somali na Marekani ndio raia wa kwanza wa Kisomali kuchaguliwa katika wadhfa mkuu kama huo nchini Marekani.

Uchaguzi wake unajiri siku chache tu baada ya rais mteule Donald Trump kushtumu wahamiaji wa Kisomali mjini Minnesota kwa kueneza maoni ya itikadi kali.

Akisherehekea ushindi wake bi Omar amesema kuwa atakuwa sauti ya waliotengwa katika bunge la jimbo hilo.

''Nadhani nimeleta sauti ya akina mama vijana wanaotafuta fursa''.

Redio ya uma katika jimbo hilo ilimnukuu akisema kuwa alitoroka nchini Somalia na familia yake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati alipokuwa na umri wa miaka minane pekee.

Waliishi nchini Kenya kama wakimbizi kwa takriban miaka minne kabla ya kuelekea Marekani na kuishi katika jimbo lenye Wasomalia wengi la Minnesota

Msomali achaguliwa katika bunge la Marekani - BBC Swahili
 
Bila shaka Somalia watapanga siku ya mapumziko kitaifa kwa ajili ya kusherekea ndugu yao kupata shavu huko USA
 
Le akili kubwazii, angeendelea kukaa lazima wangemchagua kuwa presidaa wao.

Maana sasa hv wanachagua tu mabilionea, na yeye ni mmojawapo wa bilioneaz...
 
Diaspora wa KiTanzania hata ardhi mmetunyima kununua.... Hata kumiliki uwanja haturuhusiwi....!!
Raia Mzalendo kaenda nje kutafuta masilahi ili alete nyumbani...Waziri anatukashifu!!!
 
Diaspora wa KiTanzania hata ardhi mmetunyima kununua.... Hata kumiliki uwanja haturuhusiwi....!!
Raia Mzalendo kaenda nje kutafuta masilahi ili alete nyumbani...Waziri anatukashifu!!!
Shida kubwa ya sisi waafrika ni kutojitambua,chuki za ajabuajabu uwezo mdogo wa kuona mambo,mwafrika anatakiwa aamke ajikung'ute vumbi vumbi halafu tusonge mbele.
 
Trump kaingia madarakani kupitia mlango wa uwani...kwa sera ya ubaguzi , jimbo la Minisota lina wageni wengi wahamiaji inaonekana uchaguzi uligubikwa na ubaguzi waminisota wakapiga kura kwa kubaguliwa na Trump

Mwelekeo wa Dunia hivi sasa ni wa kubaguana ndio dili

walianza waingereza katikati ya mwaka huu walipopiga kura ya kujitoa jumuiya ya ulaya na sasa wamerekani wamefuata nyayo zile zile

wakubwa wameanza bado sisi kula nyama ya sera mbaya ya kubaguana kwa misingi ya Dini , kikabila na kikanda...

sera ya marekani ya New World Order iko katika majaribu makubwa hivi sasa watamzuia nani wakati barabara wameionyesha ya kubaguana huko kwao kama ndio njia bora kabisa ya kushika madaraka makubwa ya kiuongozii...?
 
sera ya marekani ya New World Order iko katika majaribu makubwa hivi sasa watamzuia nani wakati barabara wameionyesha ya kubaguana huko kwao kama ndio njia bora kabisa ya kushika madaraka makubwa ya kiuongozii
Nani atamrudisha "jini"kwenye chupa!naona dunia inarudi kwenye miaka ya 40.
 
Back
Top Bottom