Hakuna mtu ambae alikuwa hajui kuwa Ngorika ipo siku litauwa,nadhani hata police na vyombo vingine vya barabarani vilikuwa vinasubiri tu siku.ngorika ni kampuni ya mabasi ambayo tangu enzi ilikuwa inasifika kwa speed kali barabarani nahata baadhi ya askari wanajua hilo na walikuwa hata wakidiriki kusifia mwendo wa yale mabasi.binafsi nilishaapa kutopanda lile basi milele baada ya kuona jinsi linavyoenda na hata ukiangalia wahudumu wa bus lile kuanzia conductor hadi dereva ni mirungi tu kwa kwenda mbele,kwa ufupi ni mabasi ambayo yanaonekana matatizo yake yameanzia kwa tajiri wao.Asubuhi hii basi la Ngorika lililokuwa linatoka arusha kwenda dar limegongana na Hiace imeandika Shalom katika daraja la Makumira nje kidogo ya jiji la Arusha watu wamekufa na wengine wamejeruhiwa..
Mungu aziwe mahali pema roho za marehemu.. Amen
Madereva wa ngorika na chakito ndo wanaongoza kwa mwendo kasi ili wafike wa kwanza.wamewekewa utaratibu na maajenti wa tiketi kuwa gari ya kwanza kufika ubungo driver anapewa 50,000 ili kuvutia abiria wafanyabiashara wanaopenda kuwahi...
imetokea ajali mbaya maeneo ya makumira Arusha kati ya hiace na ngorika...watu 9 wamekufa hapohapo..!habari zaidi zitawajia..!
this is really shocking kama ni kweli mkuu... Yani wanachezea maisha ya watu hivi hivi kisa 50,000??... Na hao polisi wa kudhibiti mwendo kasi wapo wapi?? Si huwa naskia kila basi huwa linapewa time chart yake na expected time of arrival?? Mbn inakua ivyo sasa??
Ni kweli kabisa, na pia mpaka pale wamiliki wa mabasi watakapoamua kupunguza hizo ajali.Hapo inabidi idara nzima ya polisi wa usalama barabarani wajivue gamba.Kazi yao ni kukinga mikono wapate pesa na sio kutekeleza majukumu yao.
tatizo ni serekali kutotaka kufana upanuzi wa barabara, si rahisi kumaliza ajali za barabarani bila kuwa na utatuzi wa barabara. imefika wakati nchi yetu iwe na double rod za kwenda na kurudi, apo tunaweza kupunguza ajali.
Pole sana mkuu, heri umetoka mzima..Hata mimi leo nilikuwemo katika gari lililopata ajali maeneo ya Mbezi kwa Yusuph asubuhi hii.Tunamshukuru Mungu kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha.Jamani hizi ajali....