THK DJAYZZ
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 2,167
- 175
Watu 14 wamekufa baada ya gari kupinduka eneo la msangamwelu barabara ya Mbalizi wakitokea mnadani. Source ITV.
Jumla ya watu 11 wamepoteza maisha na watu 43 kujeruhiwa vibaya baada ya ajali ya lori aina ya Fuso kupinduka huko wilayani chunya mkoani Mbeya.Lori hilo lilikuwa likifanya safari kutoka chunya kwenda Mbeya mjini na chanzo cha ajali ni mwendo mkali aliokuwa akiendesha dereva wa lori hilo bwana Kapufi.Source;STAR TV.
Watu 14 wamekufa baada ya gari kupinduka eneo la msangamwelu barabara ya Mbalizi wakitokea mnadani. Source ITV.
Sawa,hao 14 ni kwa mujibu wa ITV,mi nimeipata star tv.mkuu waliokufa ni 14.roho zilazwe mahali pema peponi.
Msanga Mwelu napajua sana, ni njia ya kwenda Chunya. Eneo hilo lina ujambazi sana. Majambazi hutega mawe makubwa sana barabarani kisha huvamia wakiwa na mibunduki yao.
Hebu tusubiri maelezo zaidi kutoka kwa mashuhuda
Mungu zilaze roho za marehemu mahali pema peponi.