Mlisema Hayati Magufuli amekata miti milioni 3 mvua hazitanyesha

Mkiulizwa vitu vigumu, badala ya kujibu huwa mnakimbilia manejo kama haya;

1. Umetumwa

2. Umetumwa na mabeberu

3. Siyo mzalendo

4. Mpinzani

etc
Kwani wewe Ulikimbilia kuniuliza nini? Kwangu haikuwa vigumu kukujibu nilivyokujibu.

Nitarudia, Kapande treni la kupindisha.
Ahsante, nyingine.
 
Sasa hivi sehemu za Marekani na Japan zina baridi ambayo haijawahi kuonekana. Mwaka huu Uingereza ilikumbwa na joto ambalo lilisababisha mataruma kupinda.

Tunaposema kuwa tabia nchi itabadilika tunamaanisha kuwa kutakuwa na ukame ambao hatutarajii, mara moja moja zitanyesha mvua kubwa kuliko tulivyozea, tutakuwa na vimbunga kuliko kawaida. Athari nyingine ni kuwa kutokana na kukatwa miti maji yanayoingia mtoni yanakuwa na matope mengi hivyo kupelekea mabwawa kujaa mapema. Mtera na Kiwira zinakosa maji kutokana na matope kujaa. Nyie endeleeni kubisha maana majuto ni mjukuu.

Amandla.....
Wape wape vidonge vyao.........................................shauri yao
 
Ni nani alisema kuwa mvua hazitanyesha tena? Mjinga na lofa ni wewe ambae unashindwa kutambua kuwa kinachozungumziwa ni kuwa uwapo wa mvua sio wa uhakika tena.

Hata baada ya kupitia ukosefu wa maji na mgao mkubwa wa umeme bado unadhani hii hali ni ya kawaida?

Amandla....
 
Nakuambia huna lolote ujualo zaidi ya kupiga siasa za kitoto. Sheria inasema kufungua kesi ya kupinga matokeo ni ndani ya miezi 6 baada ya uchaguzi. Sasa unaposema afungue sasa kuna chochote unajua kuhusu siasa au ni utoto unakusumbua?
Kwanini msingefungua ndani ya hiyo miezi sita!?
 
Kulwa nakusihi nakushauri, isijaribu tena kushiriki kuleta madam majukwani, hata mimi ni mwana CCM mwenzio na nilipenda baadhi za siasa za Marehemu Magufuli, Ndugu unetuaibisha kwa ma UTOPOLA NA UJINGA ULIOUANIKA HUMU JUKWANI, hata Magufuli huko Kaburini anasikitika sana na kuona aibu, kuwa na vijana wazembe kama.wewe.
 
Kulwa nakusihi nakushauri, isijaribu tena kushiriki kuleta madam majukwani, hata mimi ni mwana CCM mwenzio na nilipenda baadhi za siasa za Marehemu Magufuli, Ndugu unetuaibisha kwa ma UTOPOLA NA UJINGA ULIOUANIKA HUMU JUKWANI, hata Magufuli huko Kaburini anasikitika sana na kuona aibu, kuwa na vijana wazembe kama.wewe.
Haujamtendea haki mleta mada.
badala yake nawewe umedandia treni la wadhalimu.

Binafsi sijauona uzembe wake.

Mjibu alivyokuwa anategemea badala ya kumtupia madongo.
 
Kuna watu walitumia kodi za watanzania kusoma lakini bado ni wajinga na malofa ya kutupwa yasiyoweza kutumia akili zao hata kidogo.

Yapo mengine Ubelgiji na mengine Ufipa ambayo watoto wao ni raia wa Marekani yalitangaza kwamba kwa kuwa Magufuli amekata miti milioni 3 ili kujenga bwawa la umeme kwenye mbuga ya Selous basi mvua hazitanyesha tena Tanzania!

Lakini sasa mvua inanyesha kila mahali tena kwa wingi sana lakini kwa aibu hayo majitu yapo Ubelgiji yakifakamia vyakula vya wazungu bila aibu kabisa.
Kweli ni jalala kama ulivo!
 
Uliowataja kama watakuwa wajinga, basi wewe utakuwa mwehu.

Kwanza hakuna mtu aliyewahi kutamka kuwa mvua hazitanyesha kwa sababu ya ukataji miti mioni 3. Leta ushahidi.

Watu wamekuwa wakiongelea zaidi juu ya kutotabirika kwa mvua za uhakika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, na hivyo kutokuwa na uhakika wa kupata umeme wakati wote kutokana na hilo bwawa.

Wengine, hasa watu wa hifadhi walielezea kuwa kutakuwa na upungufu wa maji kwaajili ya wanyama kwa sababu maji yote yataishia bwawani.

Na wengine walielezea athari za kimazingira kwa sababu mradi utasababisha ukataji wa miti zaidi ya milioni 3.

Wengine waliongelea hekima ya kuanzisha mradi mpya unaotumia maji wakati kulikuwa na miradi iliyokwishaanza inayotumia gas ambayo haiathiriwi na matatizo ya ukame.

Sasa wewe, huenda kutokana na tatizo na uwezo mdogo wa akili, uliishia kusikia tu miti milioni 3, na upungufu wa mvua, ukaona ni sawa na kutokuwa na mvua nchi nzima. Kwanza ni lazima uwe mpu.mbavu hasa kufikiria kuwa ukataji wa miti milioni 3 utasababisha mvua isinyeshe kabisa nchi nzima, japo ni kweli tendo hilo linakuwa na mchango wake katika kuchangia ukosefu wa mvua za uhakika na ongezeko la joto linalotokana na hewa ukaa kutokana na kukosekana mazingira asilia ya kuinyonya hewa ukaa na kutoa hewa nzuri ya oksijeni.
 
Wajinga na malofa wapo ufipa tu? Nchi hii inashindwa kuendelea kwasababu CCM (wanakula pesa za kodi) inashughulika na vyama vya upinzani kuliko maendeleo ya wananchi.

Tangu 1961 bado tunahangaika na umeme wa mgao, maji ya mgao, matundu ya choo, madawati na afya. Baada ya kugundua mvua imenyesha imekusaidia nini?

Kwa ujinga wa CCM wanapandisha bei za bando ili watu wasiongelee CCM mitandaoni.
Mbina ninyi Chadema tangu 1992 mnahangaika kujenga Ofisi ya Makao Makuu na mpaka leo hata jiwe moja hamjaweka?
 
Hawana akili
Nyie mnaakili sana ndiyo maana tangu 1961 mpaka sasa mnahangaika na madawati na matundu ya choo shuleni. Wakati hivi ni vitu dogo sana ambapo ndani ya miezi 6 umeshamaliza watoto wana madawati na vyoo. Ila tangu 1961 mpk sasa ni miaka mingapi? Mnaa akili sana
 
Nyie mnaakili sana ndiyo maana tangu 1961 mpaka sasa mnahangaika na madawati na matundu ya choo shuleni. Wakati hivi ni vitu dogo sana ambapo ndani ya miezi 6 umeshamaliza watoto wana madawati na vyoo. Ila tangu 1961 mpk sasa ni miaka mingapi? Mnaa akili sana
Chadema miaka 30 inahangaika kupanga ufipa
 
Ila hii mnvua, mi natabiri katoto ka ernino msimu huu, Nina muda mrefu sijaona mvua za mfululizo kiasi hiki
 
Back
Top Bottom